Monday, 30 November 2015

#YALIYOJIRI>>>Profesa Lipumba Akutana na Rais John Magufuli Ikulu Dar es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na kumpongeza kwa hotuba nzuri iliyoweka mwelekeo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano. Pia Prof Lipumba amesifu na kuunga mkono Juhudi za Mhe Rais katika kupambana na wakwepa kodi na wahujumu uchumi. Hii hapa...

#YALIYOJIRI>>>Chama cha Mapinduzi CCM yakanusha Zilizosambaa Kwamba Imekubali Kumkabidhi Maalim Seif Ikulu.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano.  Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo...

#YALIYOJIRI>>>Upotevu wa Makontena 349 Bandarini: Watu 12 Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi.Fahamu zaidi hapa.

Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo. Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP)...

#YALIYOJIRI>>Rais John Magufuli Akutana na Mabolozi Wa China na Korea Kusini,Ahakikishiwa Ujenzi wa Daraja la Salender Dar-es-salaam.Fahamu zaidi hapa.

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Vichwa vya habari za...

#YALIYOJIRI>>>Serikali ya Tanzania Yazungumzia Tishio la Marekani Kusitisha Misaada Tanzania.Fahamu zaidi hapa.

Serikali imezungumzia tishio la Serikali ya Marekani la kusitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kukamatwa kwa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Ofisi ya Ikulu jana ilisema masharti yaliyotolewa na Serikali ya Marekani yanatekelezeka na yatamalizwa kabla ya kikao cha Bodi ya Shirika la Maendeleo ya...

#Breaking News>>Sheikh Ponda Aachiwa Huru.Fahamu zaidi hapa.

Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia  Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda. Hati ...

Sunday, 29 November 2015

MATOKEO NA MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA YAKO HAPA.

MICHEZO ILIYOCHEZWA NOVEMBER 28 LIGI KUU UINGEREZA. Aston Villa 2-3 Watford Bournemouth 3-3 Everton  Crystal Palace 5-1 Newcastle  Man City 3-1 Southampton  Sunderland 2-0 Stoke  Leicester 1-1 Man Utd  MICHEZO ILIYOCHEZWA NOVEMBER 29 LIGI KUU UINGEREZA.  Spurs 0-0 Chelsea West Ham 1-1 West Brom Liverpool...

Saturday, 28 November 2015

#YALIYOJIRI>>>Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kufungua duka lake kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu wiki ijayo.Fahamu zaidi hapa.

Medical Store Department of Tanzania (MSD) imeanza kutekeleza kilichosemwa na Rais John Magufuli utaratibu wa kufungua maduka matibabu katika hospitali za serikali, kwa kuanzia na Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatatu ijayo. MSD Mkurugenzi Mkuu, Laurean Bwanakunu walisema kuwa mikakati tayari kuweka kwa ajili ya kufungua maduka na kwamba wao kwa sasa ni kutafuta kibali...

#YALIYOJIRI>>>"Dili Limebumbulika"Magogo ya Milioni 300 Yakamatwa Bandarini Yakipelekwa Nchini China Kinyemela.Fahamu zaidi hapo.

Kontena 37 zenye shehena ya magogo aina ya mninga yenye thamani zaidi ya Sh. milioni 300 zimekamatwa zikiwa zinasafirishwa kuelekea nchini China bila kibali. Katika shehena hiyo, kontena 31 zimekamatiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kati ya hizo mbili zimekamatwa mkoani Mbeya,  na mikoa ya Rukwa na Pwani katika maeneo ya Kibaha na Kongowe, kontena moja...

#YALIYOJIRI>>>Papa Francis Kumfufua Nyerere,Mama Maria Nyerere Atangulia Uganda.Fahamu zaidi hapa.

ZIARA ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis nchini Uganda imetajwa kuwa itafufua mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu. Kwa mujibu wa mtandao wa ETN wa nchini Uganda, ziara hiyo ya kitume ya Papa Francis itamfikisha katika eneo la Namugongo ambalo mashahidi wa imani ya dini ya Kikristu walichomwa moto. Ni ...