Msanii
wa muziki wa bongo fleva, Dogo Janja kwa mara ya kwanza amefunguka
kuhusu mahusiano yake, na kutoa sintofahamu kuhusu kutoka kimapenzi na
muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya.
Akizungumza
na East Africa Television, Dogo Janja ambaye mara nyingi hapendi
kuzungumzia maisha yake binafsi, ameamua kusema kuwa msanii huyo anafaa.
"Irene
ni mwanamke mzuri, anavutia, kila mwanaume anayejua mwanamke mzuri
anafaa kuwa naye, ila kwa upande wangu mimi namkubali sana Irene Uwoya,
kwani anaigiza vizuri, hivyo namkubali kwa kazi zake pia", alisema Dogo Janja.
Hivi
karibuni kumekuwa na tuhuma za Irene Uwoya kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na msanii Dogo Janja, ambapo watu wengi wamekuwa na mtazamo
tofauti wakisema si sahihi kwani Irene Uwoya ni mkubwa sana kwa Dogo
Janja. Jambo ambalo Dogo Janja anaonekana kutoliafiki.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment