Na Regina Mkonde
Chama
cha Chadema kimedai kuwa, serikali bado haijajibu hoja zilizotolewa na
Kamati yake Kuu hivi karibuni, kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi
nchini, huku ikiikomalia kutoa ufafanuzi juu ya hali ya chakula, deni la
taifa, ukusanyaji kodi, vyanzo vya mapato vilivyopokwa halmashauri
pamoja na hali ya uchumi kwa wananchi.
Akizungumza
na Wanahabari, jana Agosti 3, 2017, Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango,
Halima Mdee, alidai kuwa majibu yaliyotolewa na serikali kupitia
Msemaji wake Mkuu Dkt. Hassan Abass, hayajatolea ufafanuzi wa hoja
zilizotolewa na chama hicho, na kutuhumu kwamba ripoti zilizotumiwa
kujibia hoja zao zilikuwa za uongo.
“Muda
wa maneno umepitwa na wakati tunataka watujibu hoja hizi, suala la deni
la taifa halijajibiwa, tunataka serikali iangalie upya sera ya deni la
taifa sababu utaratibu uliopo sasa umepitwa na wakati,” alisema.
Aidha,
aliitaka serikali kupitia Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Fedha na
Mipango itoe majibu kwa nini hali ya chakula inakuwa mzigo kwa wananchi
katika kipindi hiki, pamoja na kutoa ufafanuzi wa sababu ya sekta ya
kilimo iliyoajiri 75% ya watanzania inaporomoka.
“La
kwanza, juu ya akiba ya chakula, tulisema 2015 akiba ya chakula ilikuwa
tani 468,846 wakati Rais Jakaya Kikwete anamaliza muda wake, miaka 2
baadae, akiba iliporomoka kutoka tani zaidi ya laki nne kwenda tani
74,826. Ikumbukwe kuwa,serikali inapokuwa na akiba ya chakula ya kutosha
kwenye ghala la chakula inakuwa na uwezo wa kudhibiti bei holela ya
chakula kutoka kwa wauzaji binafsi,” alisema na kuongeza.
“Katika
kipindi cha Kikwete, malengo yalikuwa kilimo kikue kwa 6% katika mpango
wake wa miaka 5, lakini kiliporomoka kwa 3.5%, baada ya Magufuli
kuingia kimekuwa kwa asilimia 1.7, badala ya kwenda mbele tunarudi
nyuma, tunatarajia serikali ije na majibu hapa, kwa nini kilimo
kinachotoa ajira kinaporomoka, watupe mpango mkakati. Mwaka 2015
tulisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya mbolea ni bilioni 78 na bado
ilikuwa haijitoshelezi, 2017 imeshuka mpaka bilioni 10.”
Kuhusu sekta ya biashara, alidai kuwa,“kwa
mwaka mmoja, kwa jinsi serikali isivyo rafiki na wafanyabishara,
wafanyabiashara wanaambiwa wezi, wananchi wanaaminishwa kuwa
wafanyabiashara wezi, serikali haioni madhara ya kuminya mabenki ya
biashara kwamba kunagandamiza wafanyabiashara, hadi sasa biashara 7,277
zimefungwa, haioni jambo la ajabu kufungwa biashara. Haijajibu sababu ya
kudorola kwa biashara.”
“Tulizungumzia
ukata, wafanyabiashara kushindwa kulipa mikopo serikalini.
kilichozungumzwa juzi, leo kiimezungumzwa na taasisi ya wafanyabishara
na uwekezaji kwamba sababu ya serikali kuondoa fedha katika benki za
biashara na kuziweka BOT ambapo haizalishwi na haizunguki,
“Kumeleta
athari katika sekta ya kibenki inayochangia 30% ya pato la taifa
ikiwemo kukopesha wafanyabiashara, sasa hivi hakuna asiyejua benki
zimepata hasara, mabenki hayakopeshi wafanyabiashara sababu wanajua
mzunguko wa fedha haulipi tunaishia kukopesha wafanyakazi,” alisema.
Mdee
alidai kuwa, serikali inabidi ifanye uchambuzi kuhusu vyanzo vyake
vipya vya mapato na vile vilivyohamishwa kutoka halmashauri kwenda
serikali kuu, pamoja na hali ya maisha ya wananchi wake ili ijiridhishe
kama uchumi wa nchi na wa wananchi unakua au la.
“Uchumi
wa Tanzania kwa miaka 3 uko katika ukuaji usiopungua kwa asilimia 7.
uchumi umeanza kukua tangu awamu ya pili ya Mkapa katika mapinduzi ya
uchumi, majibu tunayotaka, huu uchumi ulio palepale umeweza kujitokeza
vipi kwa maisha ya mtanzania, hayo ndiyo majibu tunayotaka, kwa zaidi ya
miaka 10 uchumi umekua, mkulima maisha yake yamesogea, maji vijijini
yanapatikana. serikali ituambie kwa kiasi gani uchumi unajitafsiri kwa
maisha ya watanzania,”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment