Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara,Yusuf Manji (41) na wenzake watatu imeahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aimeiahirisha kesi hiyo leo baada ya Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa, kueleza kuwa ingawa kesi
ilipangwa kutajwa lakini mshtakiwa wa kwanza, Manji, yupo Mahakama Kuu
Manji aliwakilishwa na Mawakili, Mpaya Kamala, Seni Malimi na Hudson Ndusyepo.
Wakili
Kishenyi aliiomba mahakama kesi hiyo itajwe Jumatano ya Agosti 9, 2017
na upande wa utetezi haukuwa na pingamizi. Upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika.
Katika
kesi hiyo, Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya
sheria ya uhujumu uchumi na Usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa
vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye
thamani ya zaidi ya Sh200 milioni na mihuri.
Washtakiwa wengine ambao walikuwapo mahakamani ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).
Awali,
akiwasomea hati ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao, Wakili wa
Serikali, Tulumanywa Majigo alidai kuwa Juni 30, 2017 katika eneo la
Chang’ombe ‘A’ wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa
pamoja walikutwa na askari polisi wakiwa na bunda 35 za vitambaa
vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania vyenye
thamani ya Sh 192.5 milioni na kwamba mali hiyo ilipatikana kinyume cha
sheria.
Katika
shitaka la pili, Majigo alidai kuwa Julai Mosi, 2017 huko Chang’ombe
‘A’ washtakiwa hao walikutwa na polisi wakiwa na mabunda nane ya
vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania
vyenye thamani ya Sh44 milioni mali ambayo ilipatikana isivyohalali.
Katika
shtaka la tatu, inadaiwa pia kuwa katika eneo hilohilo, mnamo Juni 30,
2017, washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa na muhuri wa Jeshi la Wananchi
Tanzania wenye maandishi ‘Mkuu 121 kikosi cha JWTZ’ bila ya kuwa na
uhalali, kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi.
Katika
shitaka la nne, Wakili Majigo anadai kuwa Juni 30, 2017 kwenye eneo
hilo la Chang’ombe ‘A’ Manji na wenzake hao watatu walikutwa wakiwa na
mhuri wenye maandishi ‘Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma’ wakati
hawana uhalali wa kuwa na muhuru huo kitendo ambacho kingehatarisha
usalama wa nchi.
Katika
shitaka la tano, Manji na wenzake hao wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017 huko
Chang’ombe ‘A’ walikutwa na mhuri wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania wenye
maandishi ‘Commanding Officer 835 KJ Mgambo P.0. Box 224 Korogwe’
kinyume cha sheria.
Katika
shtaka la sita, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Julai Mosi,
2017 katika eneo hilo la Chang’ombe ‘A’ walikutwa na askari polisi
wakiwa namba za usajili wa gari SU 383 ambayo ilipatikana kwa njia isiyo
halali.
Kwenye
shtaka la saba washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai Mosi, 2017 kwenye
eneo hilo la Chang’ombe ‘A’ washtakiwa hao walikutwa na askari polisi
wakiwa na namba za usajili wa gari SM 8573 ambayo ilipatikana kwa njia
isiyohalali.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment