Msanii wa muziki, ambaye ni Mbunge wa Mikuni kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA, Joseph Haule maarufu kama Professa Jay, yupo matatani kukosa hifadhi ya jumba lake la kifahari alilojenga pembezoni mwa barabara ya Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, kwani ni miongoni mwa nyumba ambazo zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.
Nyumba
za kifahari zilizojengwa pembezoni maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya
jijini Dar es salaam zimekumbwa na bomoabomoa kitu ambacho kimeumiza
watu wengi sana, kwani wapo ambao hawana makazi na hawaelewi nyumba zao
zikibomolewa wataanzia wapii na wataishi wapi.
Na nyumba ya Mbunge wa Mikumi ni moja ya nyumba ambazo zimewekewa X kuashiria nayo imo miongoni mwa nyumba za kubomolewa.
Hivi
karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji wa
kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha
ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.
Tayari
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeshaanza kukata umeme kwenye
nyumba nyingi hivyo kuwafanya baadhi ya wenye nyumba kubomoa wenyewe kwa
hiari na kufungasha mizigo yao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment