Sunday, 12 February 2017

Wenzetu Wanateseka Magerezani- Tundu Lissu ..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Tundu Lissu baada ya kufanikiwa kupata dhamana jana amefunguka na kuwashukuru watanzania huku akisema si jambio la kufurahia sana kwani bado wenzao wanapata mateso magerezani.
Mhe. Tundu Lissu ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa twitter 
"Asanteni Watanzania kwa maombi yenu hatuwezi kushangilia kama bado wenzetu wanateseka Magerezani" alindika Tundu Lissu

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

YUSUF MANJI ATOLEWA SENTRO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI MUHIMBILI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekimbizwa hospitali baada ya kuugua akiwa mahabusu.

Taarifa zinaeleza, Manji ambaye alikuwa mahabusu katika kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, alianza kuumwa tokea jana.

“Kweli amekimbizwa hospitali na sasa anapatiwa matibabu,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu.

Manji alikuwa mahabusu ambako amewekwa tokea Alhamisi iliyopita baada ya kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitajwa katika listi ya watu 65 wanaotuhumiwa katika suala la madawa ya kulevya.

Lakini leo ameugua ghafla baada ya kuendelea kubaki rumande kwa siku zote licha ya kwamba hajapelekwa mahakamani.

Kumekuwa na taarifa huenda kesho akafikishwa mahakamani, lakini bado maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa hawataki kulizungumzia suala hilo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Baada ya Kutoka Selo Kwa Dhamana Hii Ndio Post ya Kwanza Aliyoandika Wema Sepetu Instagram.Fahamu zaidi hapa.

Inawezekana kama wewe ni shabiki wa Wema Sepetu ulikua na hamu sana ya kujua post yake ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii itahusu nini baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama kufuatia sakata la dawa za kulevya lililomfanya alale Polisi.

Post ya kwanza ya Mwigizaji huyu haijahusu chochote kuhusu kesi yake ama alichokipitia wiki iliyoisha bali imemuhusu dada yake ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa kama inavyoonekana hapa chini.
Wema Sepetu atarudi tena Mahakamani mwishoni mwa mwezi huu baada ya kupata dhamana Alhamisi ya wiki iliyopita kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Rais Magufuli Akerwa na Kitendo cha Manji na Gwajima Kwenda na Mashabiki wao Polisi.Fahamu zaidi hapa.

 Inaonyesha kila kinachoendelea huwa kinamfikia Rais Magufuli ambapo leo kwenye hotuba yake IKULU Dar es salaam ameongea kuhusu wale Mashabiki wa Yanga walioonekana kulifutafuta vumbi gari la Mfanyabiashara Yusuph Manji baada ya kuingia kuhojiwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
 Pamoja na hilo, rais  pia ameongelea ishu ya Wanakwaya wa Askofu Gwajima kwenda na kusimama nje ya kituo cha kati cha Polisi baada ya Askofu huyo kuingia kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
==> Msikilize hapo chii akiongea


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Yanga yatoa kipigo takatifu Comoro cha NGAYA 1 VS 5 YANGA (FULL TIME).Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Yanga yaanza vizuri michuano ya clab Bingwa Afrika baada ya kuifunga goli Ngaya 1-5 Yanga kwenye uwanja wa wao timu ya Ngaya kutoka Comoro.

Magoli yamefungwa na:-

Dakika ya 43, Haji Mwinyi anapiga mpira wa mrefu, Chirwa anauwahi na kupiga pasi safi kwa Zulu ambaye anaachia mkwaju saafi na kuandika bao moja kwa Yanga.

Dakika ya 45+1, Msuva anaachia mkwaju mkali kutoka pembeni na kuandika bao la pili kwa Yanga.

 Dakika ya 59, Kamusoko anamchambua kipa na kutoa pasi safi kwa Chirwa ambaye anaandika bao saaafi kabisa.

Dakika ya, Tambwe anaunganisha krosi safi ya Juma Abdul na kuandika bao la nne.

Dakika ya 66 Said Khalfan anaachia Mkwaju mkali na kuandika bao kwa Ngaya.
  
Dakika ya73, Kakumusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli unajaa wavuni ilikuwa ni baada ya kupokea pasi ya Niyonzima. Huku upande wa Ngaya, bao lao la kufutia machozi limepachikwa na Said Khalfan dakika ya 66.


KIKOSI CHA YANGA
1. Deogratius Munishi 
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani 
6. Justin Zullu 
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko 
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Haruna Niyonzima 

Akiba
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Emanuel Martin
- Juma Mahadhi 
- Juma Saidi

- Deusi Kaseke


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 11 February 2017

Majaliwa Afunguka Issue ya Madawa ya Kulevya Inayoratibiwa na Makonda.Fahamu zaidi hapa.

JUMLA ya Watanzania 578 wamekamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akiahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitaja nchi ambazo Watanzania hao wamefungwa kuwa ni pamoja na China (200), Brazil (12), Iran (63), Ethiopia (7) na Afrika ya Kusini (296).
Majaliwa pia alisema vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuungwa mkono.
Alisema madawa ya kulevya huingia zaidi kutumia kwa njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi na mabasi yatokayo Kenya, Uganda na Zambia.
“Lengo la serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri - wauzaji na wasambazaji," alisema Majaliwa.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MANENO YA KOCHA GEORGE LWANDAMINA BAADA YA YANGA KUKANYAGA COMORO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kocha George Lwandamina amesema wako vizuri na wanajiandaa kufanya vema katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ngaya ya Comoro.


Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Moron, Comoro, Lwandamina amesema hakuna wanachoweza kulaumu.


“Hadi sasa kila kitu kinakwenda vizuri na tunamshukuru Mungu tulitua salama.


“Hakuna tunachoweza kulalamika, mambo yanakwenda vizuri na tutaendelea na maandalizi ya mwisho,” alisema.



Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kuwavaa wenyeji wake katika mechi ambayo inaonekana haitakuwa rahisi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Makonda Afunguka Kuitwa na Bunge.Fahamu zaidi hapa.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa kuwa hajapokea barua ya kuitwa.
 
Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema hatoweza kwenda mbele ya kamati hiyo bila barua rasmi iliyomtaka kufanya hivyo.
 
Bunge lililokuwa likiendelea na vikao vyake Dodoma kabla ya kuahirishwa juzi, lilipitisha uamuzi wa kuwataka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alaxander Mnyeti, kufika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa kutokana na kauli walizozitoa, zinazodaiwa kuudharau mhimili huo wa dola.
 
Lakini Makonda alisema jana “hilo suala la mimi kuitwa kwenye kamati nalisikia na kulisoma kwenye magazeti.”
 
“Sina uhakika ni lini wamefikia uamuzi huu wa kuniita na hata kama wamefikia uamuzi huo, sijaletewa barua rasmi.”
Baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo wa kuitaka Ofisi ya Bunge iwaandikie barua viongozi hao, juzi baadhi ya wabunge walihoji kauli ya Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, kwamba azimio la chombo hicho cha kutunga sheria kumtaka Makonda kufika mbele ya kamati kujieleza kuhusu tuhuma za kuudharau mhimili huo, halikufuata utaratibu.
 
Hatua hiyo iliamsha hasira kwa baadhi ya Wabunge na kuomba mwongozo kuhoji kwa nini Katibu wa Bunge ametoa kauli ambayo inakinzana na makubaliano ya Bunge.
 
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara na mwezake wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (wote Chadema) walihoji kuhusu kauli ya Dk. Kashililah.
 
Waitara alisema, “Asubuhi ya leo ( juzi) nimetumiwa ‘clip’ ya sauti ya Katibu wa Bunge akikosoa uamuzi wetu hapa na pia gazeti la Habari Leo, Ukurasa wa 25, kuna habari imeandikwa.
 
Katika taarifa hii, Katibu wa Bunge anasema maazimio ya Bunge yalikosewa na hayakufuata utaratibu,” alisema na kuongeza kuwa: “ Kwa maana nyingine, hatatekeleza kile tulichokubaliana.”
 
Mchungaji Msigwa wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alieleza kuwa hajafurahishwa na kauli ya Katibu wa Bunge.
 
Alisema Katibu wa Bunge amekosea kwenda katika vyombo vya habari na kudai chombo hicho cha kutunga sheria kimekosea kwa kuwa anafanya kazi ya Bunge na kwamba hajaajiri wabunge na anapaswa kufuata maagizo yao.
 
Hoja ya kutaka kina Makonda washughulikiwe iliwasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) katikati ya wiki na ilijadiliwa na kuungwa mkono na wabunge wote, wakiwamo mawaziri kwa kusema ‘ndiyo’.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MAN UNITED YASHINDA NA KUJING'OA NAFASI YA 6 KWA MUDA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kwa muda, Man United wametoka katika nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Watford kwa mabao 2-0.


Mabao hayo yamefungwa na Anthony martial na Juan Mata aliyefunga la kwanza na kuifanya Man United ifikishe pointi 49 hadi katika nafasi ya tano.


Matokeo ya mechi zijazo kama ile kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham inaweza kuirejesha Man United kwenye nafasi ya sita tena!


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Msami Baby feat Chemical unaoitwa "So Fine".

Download wimbo wa Msami Baby feat. Chemical - So Fine.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa Alley unaoitwa "Bonge la Demu".

Download wimbo wa Alley   Bonge la Demu.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Kassim Mganga ft. Nyota & Kilimanjaro Band (Njenje) - SOMO.

Download wimbo wa Kassim Mganga ft. Nyota & Kilimanjaro Band (Njenje) - SOMO


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mavugo akamilisha kipigo kwa Prisons SIMBA 3 VS 0 PRISONS (FULL TIME).Fahamu zaidi hapa.

Simba yaonesha nia ya kusaka ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara timu ya Prisons imecheza na Simba huku,Timu ya Simba ikionekana kumiliki mpira wakati wote.

Dakika 18, krosi ya Bukungu inagongwa na kumkuta Liuzio, anaweka kifuani na kuandika bao la kwanza kwa Simba leo na la kwanza kwake katika Ligi kuu Bara

Dakika 28 Ajibu anapokea pasi nzuri ya Mavugo, naye anamchambua kipa wa Prisons kama penalti na kuandika bao safi kabisa.

Dakika 68, Mavugo anaifungia Simba bao la tatu kwa Kichwa akiunganisha krosi ya outer ya Ajibu. 

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa 

Picha: TID Aanza Maisha Mapya Baada ya Siku 5 za Lupango, Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya..!!..Fahamu zaidi hapa.

Msanii mkongwe wa muziki TID ameamua kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya ikiwa ni siku chache toka aachiwe na mahakama kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 na kutakiwa kuripoti polisi kwa mwezi mara mbili baada ya kukiri kutumia Madawa ya kulevya pamoja na wenzake 12.

Muimbaji huyo ambaye alikaa lupango kwa siku tano kabla ya kuachiwa, amemtangaza mpenzi wake mpya ambaye jina lake halikutambulika mara moja.

“The Smile i needed to see after all the trouble i have been through. Million Dollar Smile, am i in Love again!,”aliandika TID Instagram huku akaiwa ameweka picha ya mrembo huyo hapo juu.

Aliongeza, “Watasema sana na kisha watalala kama kunipenda najua unanipenda sana ooohyeahhh,”.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Video..Askofu Gwajima Akimfufua Mtu Kanisani Kwake..!!..Fahamu zaidi hapa.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Spika wa Bunge Job Ndugai akemea wabunge kukamatwa Kibabe.Fahamu zaidi hapa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amekemea tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.

Akihitimisha mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda "kibabe".

Pia Ndugai amewatoa hofu wabunge kuhusu hadhi ya Bunge na kusema kuwa hadhi ya chombo hicho haijashuka, na kwamba Muhimili huo wa Bunge hauna mgogoro wowote na serikali wala mahakama.

Pia ameeleza madhara ya kukosekana kwa mbunge hata mmoja akisema kuwa yeye kama Spika anapoitisha kikao cha kamati fulani, ni lazima akidi itimie, vinginevyo kukosekana kwa mbunge hata mmoja kuna athari kubwa katika maamuzi ya kikao na Bunge kwa ujumla.

Hatua hiyo inafuatia malalamiko ya wabunge wa upinzani yaliyotolewa hivi karibuni juu ya utaratibu unaotumiwa na Jeshi la Polisi kukamata wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge, wakitolea mfano wabunge Tundu Lissu na Godbless Lema.

Malalamiko hayo yalifikia hatua ya mbunge Zitto Kabwe kutoa hoja akitaka kiti cha Spika kitoe maamuzi ya kulinda hadhi ya Bunge kutokana na kukamatwa kwa Tundu Lissu, hoja ambayo Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliipangua, jambo lililopelekea wabunge wote wa upinzani wasusie kikao cha Bunge cha jioni ya Februari 8, 2017.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Madaha Ajikosha, Ampa Tano Makonda..!!..Fahamu zaidi hapa.

MWANAMUZIKI Baby Joseph Madaha amefungukia uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda wa kuanza kudili na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya akisema kuwa, huenda ikasaidia mastaa wengi kubadilika. Akipiga stori na Ijumaa

hivi karibuni, Baby Madaha ambaye naye aliwahi kukwaa skendo ya kudaiwa kusafi risha unga kwenda Uarabuni, alisema kuwa anajua kweli mastaa wengi ni watumiaji na wasafi sharisha wa unga hivyo kitendo cha baadhi yao kutaitiwa, kinaweza kuwa mwanzo mzuri.

“Niliwahi kudaiwa kusafi risha unga lakini haikuwa kweli. Wanaouza na kutumia wanajulikana, hivyo mimi nimpe tu tano Makonda kwa hatua hii nzuri, naamini huko tuendako jitihada hizi zitazaa matunda,” alisema Madaha


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Video.Mbwana Samatta Azidi Kuwakuna Wazungu kwa Kiwango kikubwa cha Kufumania Nyavu..!!..Fahamu zaidi hapa.

Nahodha wa timu a taifa ya Tanzania , Mbwana Samatta amezidi kuwasha moto katika ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata wakiwa ugenini usiku wa Ijumaa hii dhidi ya Sint-Truiden.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Askofu Gwajima Kaachiwa Huru na Jeshi la Polisi.Fahamu zaidi hapa.

Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ameachiwa na Polisi leo jioni baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi mchana kwenye kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya.

Baada ya kuachiwa Askofu huyo aliandika yafuatayo kwenye mitandao yake ya kijamii “FREE AT LAST: Mungu awabariki wote mlioomba kwa ajili ya jambo hili, kesho nitakuwepo kwa ajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam. Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya hili”



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 9 February 2017

Huzuni Yatawala Mahakamani Wakati Daktari Akitoa Ushahidi Dhidi ya Scorpion.Fahamu zaidi hapa.

Daktari  Bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Christine Mataka ambaye alimpokea na kumhudumia, Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho na Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa shahidi wanne katika kesi hiyo upande wa serikali, ametoa siri nzito ya tukio hilo.

Dokta Mataka amesema alikuwa daktari wa kawaida kwa muda mrefu lakini alitunukiwa digrii ya pili (Master’s) na kuwa daktari bingwa wa matatizo ya macho miaka 14 iliyopita.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga bingwa huyo alisema macho ya Said hayakutobolewa kama inavyosemwa na watu kwenye vyombo vya habari isipokuwa yamenyofolewa na kuondolewa kabisa.

Majeruhi alifika hospitali macho yake yakiwa yamenyofolewa na kubaki hukohuko,hospitali hakufika hata na mabaki ya goroli.

Akielezea kitaalamu Dokta Mataka alisema kwa kawaida mtu anapotobolewa macho na kitu chochote ni lazima ukute goroli zikiwa zimepasuka na utete wenye utelezi unakuwa umetapakaa machoni lakini kwa majeruhi huyo goroli za macho yote mawili zilikuwa hazipo kabisa.

"Ukweli hiyo hali ilinishangaza sana kwa miaka 14 nikiwa kama daktari bingwa wa macho sijawahi kukutana na tukio kama hilo hivyo baada ya kupigwa na butwaa niliwapigia mabingwa wenzangu waje kujionea hali hiyo na tushauriane jinsi ya kufanya.

"Hata wao walivyofika wote walishangaa na kuniambia nao hawajawahi kukutana na hali hiyo.

"Nilimtibia majeruhi wakati huo huo nilikuwa nikimuongelesha na kumuuliza yaliyomsibu ambapo aliniambia wakati akinunua kuku pale Buguruni ndiyo akatokea mtu na kuanza kumshambulia.

"Nikamuuliza kama anamfahamu hiyo mtu aliniambia akimuona atamtambua.

"Baada ya matibabu nilimpeleka wodini na kumuandikia tarehe za kuhudhuria kliniki na nilimuambia kuwa katika maisha yake hawezi kuona tena hivyo ajifunze kuishi maisha ya mtu asiye na macho.

"Baadae alipoanza kuja kliniki aliniambia kuwa mama yake alikuwa akitaka kumpa jicho lake moja lakini nilimueleza ukweli kuwa hilo haliwezekani.

"Huwezi kulihamisha jicho halafu likawa hai hiyo huduma haipo hapa duniani.

Baada ya kutoa ushahidi wake mbele ha Hakimu Frola Haule kesi hiyo iliahirishwa mpaka Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo ambapo daktari bingwa wa tumbo ambaye nae alimtibu majeruhi huyo anatarajiwa kutoa ushahidi wake kwa upande wa serikali.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MASHABIKI YANGA WALIOSHA GARI LA MWENYEKITI WAO MANJI KITUO CHA SENTRO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Wakati Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akihojiwa katika kituo Kikuu cha Dar es Salaam, mashabiki wa Yanga wametoa mpya baada ya kuanza kuosha gari lake.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi kwenye viwanja kituo hicho. Wakati Manji akiwa anahojiwa, wenyewe walianza kuosha gari hilo la mwenyekiti wao.
Mashabiki hao waliendelea kuliosha gari hilo na baada ya hapo walianza kulifuta kuhakikisha linakuwa safi kabisa.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

DIAMOND AMWAALIKA RC MAKONDA NA WEMA SEPETU KWENYE 40 YA MTOTO WAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

DIAMOND AMWAALIKA RC MAKONDA NA WEMA SEPETU KWENYE 40 YA MTOTO WAKE


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

VIDEO: Yusuph Manji Arudishwa Ndani ya Polisi Baada ya Kutaka Kutoka.Fahamu zaidi hapa.

Mfanyabiashara Yusuph Manji leo amefika kituo cha polisi kati kama alivyoahidi jana baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu 65 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Yusuph Manji alifika asubuhi kwenye kituo cha Polisi cha kati ambapo baadaye alionekana akiwa anatoka nje ya kituo  kuondoka lakini ghafla akazuiwa na Polisi na kumwambia anahitajika ndani ten.
==>Litazame tukio zima hapo chini


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Picha: Askofu Gwajima Naye Kaamua Kwenda Polisi Leo Badala ya Kesho Kuitikia Wito wa Makonda.Fahamu zaidi hapa.

Askofu Josephat Gwajima mchana huu amefika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kuhojiwa baada ya kutajwa na RC Paul Makonda katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya.
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wanawasili kituo cha Polisi kati.
Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi
Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Video..Msukuma Azidi kumwashia Moto Makonda Bungeni,Awaambia Wabunge Wenzake Wamwachie Makonda Apambane Nae Mtaani Ili Amuonyeshe Fresh..!!..Fahamu zaidi hapa.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Serikali......Yampa Tundu Lissu DHAMANA Ya Milioni 20.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Sunday, 5 February 2017

Hatma ya Chege na Temba Sasa Hadharani..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema yuko mbioni kukata kiu ya mashabiki wa 'Chege na Temba' kwani bada ya kutoa ngoma yake ya Kelele za Chura, ngoma inayofuata ni yake na swahiba wake Mh. Temba kutoka familia hiyohiyo ya Wanaume.
Chege amelazimika kuweka wazi hatma ya Chge na Temba kutokana na kukumbana na maswali mengi ya watu mbalimbali wakitaka kujua ni lini wasanii hao watafanya tena kazi ya pamoja kutokana na temba kuwa kimya kwa muda mrefu.
Chege aliyekuwa akiitambulisha rasmi 'EXCLUSIVE' video yake ya 'Kelele za Chura' kwenye kipindi cha Friday Night LIVE cha EATV, alisema kwa sasa na yeye ameamua kutoa albam kwa kuwa anaamini albam zina soko, na kwa kutambua wabongo wame-miss albam kwa muda mrefu, sasa ameamua kukata kiu ya mashabiki.
Ameitaja albam yake kuwa itakwenda kwa jina la 'Sweet Sweet' na itakuwa na nyimbo 15, na kwamba kila kitu kimekamilika, na katikati ya mwezi huu itakua madukani

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni mdaiwa sugu wa kodi.....maofisa Ardhi wavamia ofisi, Watoa Notisi ya Siku 14.Fahamju zaidi hapa.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za  mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada  Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.

Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.

Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa