Daktari
Bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Christine Mataka
ambaye alimpokea na kumhudumia, Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho
na Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa shahidi wanne katika kesi hiyo
upande wa serikali, ametoa siri nzito ya tukio hilo.
Dokta
Mataka amesema alikuwa daktari wa kawaida kwa muda mrefu lakini
alitunukiwa digrii ya pili (Master’s) na kuwa daktari bingwa wa matatizo
ya macho miaka 14 iliyopita.
Akiongozwa
na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga bingwa huyo alisema
macho ya Said hayakutobolewa kama inavyosemwa na watu kwenye vyombo vya
habari isipokuwa yamenyofolewa na kuondolewa kabisa.
Majeruhi alifika hospitali macho yake yakiwa yamenyofolewa na kubaki hukohuko,hospitali hakufika hata na mabaki ya goroli.
Akielezea
kitaalamu Dokta Mataka alisema kwa kawaida mtu anapotobolewa macho na
kitu chochote ni lazima ukute goroli zikiwa zimepasuka na utete wenye
utelezi unakuwa umetapakaa machoni lakini kwa majeruhi huyo goroli za
macho yote mawili zilikuwa hazipo kabisa.
"Ukweli
hiyo hali ilinishangaza sana kwa miaka 14 nikiwa kama daktari bingwa wa
macho sijawahi kukutana na tukio kama hilo hivyo baada ya kupigwa na
butwaa niliwapigia mabingwa wenzangu waje kujionea hali hiyo na
tushauriane jinsi ya kufanya.
"Hata wao walivyofika wote walishangaa na kuniambia nao hawajawahi kukutana na hali hiyo.
"Nilimtibia
majeruhi wakati huo huo nilikuwa nikimuongelesha na kumuuliza
yaliyomsibu ambapo aliniambia wakati akinunua kuku pale Buguruni ndiyo
akatokea mtu na kuanza kumshambulia.
"Nikamuuliza kama anamfahamu hiyo mtu aliniambia akimuona atamtambua.
"Baada
ya matibabu nilimpeleka wodini na kumuandikia tarehe za kuhudhuria
kliniki na nilimuambia kuwa katika maisha yake hawezi kuona tena hivyo
ajifunze kuishi maisha ya mtu asiye na macho.
"Baadae
alipoanza kuja kliniki aliniambia kuwa mama yake alikuwa akitaka kumpa
jicho lake moja lakini nilimueleza ukweli kuwa hilo haliwezekani.
"Huwezi kulihamisha jicho halafu likawa hai hiyo huduma haipo hapa duniani.
Baada
ya kutoa ushahidi wake mbele ha Hakimu Frola Haule kesi hiyo
iliahirishwa mpaka Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani
hapo ambapo daktari bingwa wa tumbo ambaye nae alimtibu majeruhi huyo
anatarajiwa kutoa ushahidi wake kwa upande wa serikali.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment