Monday, 31 October 2016

#YALIYOJIRI>>>SMZ yatoa onyo kwa watakaoleta vurumai za kidini visiwani humo.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu amesema Zanzibar inahistoria ndefu ya uvumilivu wa kidini na kuonya kwamba Serikali itawakuchulia hatua wale wote watakaolete chokochoko za kidini.

Akizindua jimbo mpya za ibada za Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, Waziri Gavu alisema kwamba tofauti za imani ya dini kamwe isiwe chanzo cha kuigawa jamii na mifarakano.

“Ndugu zangu waumini, tofauti za dini isiwe chanzo cha mifarakano katika jamii, tujiepushe na aina yoyote ya uchokozi au mgawanyiko, daima tuwe wamoja wenye kuheshimu imani za dini nyengine” Alisema Waziri Issa Gavu.

Waziri Gavu alisema kwamba ni jambo la aibu kuona watu wanagombana kwa sababu ya tofauti za imani za kidini. Aliwataka wananchi kuendelea kutunza amani na kuongeza upendo miongoni mwao.

Alisema Serikali itaendelea kuheshimu imani za dini na kwamba kila mwananchi anawajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi na kuonya kuwa Serikali haitochelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaovunja sheria za nchi.

Waziri Issa Gavu alisema kwamba Zanzibar ina historia ndefu ya uvumilivu wa kidini ambapo pia ina historia kongwe ya dini ya Uislamu na Ukristo.

Amewataka waumini wa kanisa hilo kuungana na waumini wengine katika kuhimiza umoja na mshikamano katika jamii na kusisitiza kwamba Watanzania wanawajibu wa kuishi kwa kuheshimiana, lakini pia kuvumiliana.

Katika hatua nyengine, Waziri huyo alisema Zanzibar imendelea kuwa sehemu tulivu na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuitunza amani iliyopo.

Waziri Gavu alisema kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka huu ulifanyika katika mazingira tulivu huku waumini wa dini mbalimbali wakiendelea na shughuli za ibada zao bila kusumbuliwa.

Katika uzinduzi huo, Waziri Issa Gavu amewahakikishia waumini wa kanisa hilo kwamba Serikali itanedelea kushirikiana nao ili kuona kwmaba kila muumini wa dini anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Na Dk. Juma Mohammed, Zanzibar

MWISHO

Unaamini Kuna Uchawi Katika Mapenzi? Soma Hii InakuhusuFahamu zaidi hapa.

BILA shaka msomaji wangu uko poa, kwa wewe ambaye unasumbuliwa na shida mbalimbali za kidunia, nakuombea kwa Mungu upate ahueni. Wiki iliyopita tulianza kujadiliana kuhusu mada hii kama inavyojieleza. Je, wewe unaamini kwamba kwenye mapenzi kuna uchawi? Unaamini kwamba kuna kitu kinaitwa limbwata? Je, ni kweli mtu anaweza kwenda kwa mganga na akafanikiwa kumpumbaza mwenzi wake akili? Nakushukuru wewe uliyetumia muda wako kunipa majibu ya jinsi unavyoyaelewa mambo haya.

 Majibu niliyoyapata yalikuwa katika makundi mawili; wapo waliosema wanaamini ni kweli kuna uchawi katika mapenzi, wakaenda mbali na kutoa mifano iliyowatokea au waliyoishuhudia na kuwafanya waamini kwamba kweli kuna uchawi katika mapenzi. Msomaji wangu mmoja kutoka Unguja, Zanzibar, alisema anao ushahidi wa jinsi mume wa rafiki yake alivyoendewa kwa mganga na kimada wake hadi akafikia hatua ya kutelekeza familia ya mke na watoto watatu, akahamia kwa kimada. Unaambiwa mpaka leo hasikii haambiwi, ameikana familia yake kisa kimada.

Kundi jingine lilisema haliamini katika uchawi! Kwamba mume kumsaidia mkewe kuosha vyombo, kufua, kupika, kumpa kila anachokitaka au kutii kila anachoambiwa, siyo lazima awe amerogwa bali akioneshwa mapenzi ya dhati, yupo tayari kufanya chochote ilimradi mwenzi wake afurahi! Kwa wale walionitumia ushuhuda kuhusu limbwata, wengine wakilalamika kwamba wenzi wao wamebadilishwa mawazo na wanawake au wanaume wa nje mpaka kufikia hatua ya kuwakana wapenzi wao wa awali kwa sababu ya ndumba, nataka waelewe kitu kimoja muhimu sana.

 Mapenzi ya dhati yana nguvu kuliko hata mauti, vitabu mbalimbali vya dini vinathibitisha hili. Kwamba, ukimpenda na kumuonesha mapenzi ya dhati mwenzi wako, naye akakupenda, mkashibana, hakuna nguvu inayoweza kuingia katikati yenu, iwe uchawi, ndumba au majini na kuwatenganisha.

Hata kama kuna mtu anautazama uhusiano wenu kwa husuda, hata akikesha kwa waganga kwa lengo la kuwatenganisha ili yeye apate nafasi, ni sawa na kazi bure! Penzi la dhati lina nguvu asikwambie mtu! Hata hivyo, mapenzi ya dhati yanapokosekana ndani ya uhusiano, uwe ni uchumba, ndoa au mahusiano ya kawaida, ni dhahiri kwamba hata vitu vidogovidogo tu, vinaweza kuwatenganisha mkaishia kusingizia uchawi!

 Kama hampendani, mtu anaweza kuingiza maneno ya kuwafitinisha tu, mkaachana. Kama hampendani kwa dhati, ugomvi mdogo tu, unaweza kuwatenganisha, kama ni ndoa ikavunjika, kama ni uchumba ukaishia njiani na mambo ya namna hiyo! Kwa hiyo jambo la msingi, siyo kukimbilia kwa waganga mambo yanapoharibika ukiamini mwenzi wako amerogwa na mpenzi wa nje. Unachotakiwa kufanya kuanzia sasa, kabla mambo hayajaharibika, ni kuhakikisha kila siku iendayo kwa Mungu, unaishi vizuri na mwenzi wako.

Mpende kwa dhati, kuwa mwaminifu, mjali, msamehe anapokosea, mtimizie mahitaji yake ya msingi na usichoke kumrekebisha kwa njia nzuri ili mwisho aje kuwa bora!

Mkiishi hivi, hata atokee mchawi kutoka kuzimu, wala hawezi kuvunja ndoa yenu wala wewe hutahitaji kwenda kwa mganga ili kumroga au kumpumbaza akili asikuache, mapenzi yako ndiyo yatakayokuwa uchawi tosha. Lakini ikitokea mkaishi kwa mazoea tu, hakuna mapenzi ya dhati ndani ya nyumba, kila mmoja anajiona yeye ni bora, kiburi, dharau, usaliti, maudhi, uongo na kero za namna hiyo zimetawala, uhusiano wenu hauwezi kwenda popote na ninyi ndiyo mtakuwa wachawi wa penzi lenu.

Hata ukihangaika kwa mitishamba na hirizi, kama humuoneshi mapenzi ya dhati mwenzi wako, ni kazi bure! Siku akimpata anayemjali na kumuonesha mapenzi ya dhati, itakula kwako. Ni hayo tu kwa leo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine murua.

#YALIYOJIRI>>>>>Waziri Kigwangalla Amesema Wanawake Wanaofanya Ngono Bila Kinga Kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi.Fahamu zaidi hapa.

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha Saratani ya mlango wa kizazi

Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa kwa kujaamiana.

Kigwangala amesema kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima, amewataka kutokufanya ngono mapema.

Amesema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili zikiwa zinakwenda taratibu sana.

Kwa upande wake Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio, kutokwa na majimaji yenye harufu kali, amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Aidha Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema, kupunguza idadi ya kuzaa watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi, ukifanya ngono watumie kinga.

Sambamba na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa( DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.

Kwa upande wake Sr. Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.

Lyinga amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi.

Chanzo: Michuzi

Dowload wimbo wa Ally Kiba unaoitwa "Risabela".Hapa hapa.

#YALIYOJIRI>>>>Rais Magufuli asema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Tanzania katika Afrika.Fahamu zaidi hapa.

Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

 Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika.
Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 31 Oktoba, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambako ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Rais Magufuli ambaye kabla ya Mkutano huo na waandishi wa habari amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, amesema takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.
Pia, Rais Magufuli amebainisha kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044.
"Naomba niwahakikishie kuwa uhusiano na ushirikiano wetu ni mzuri na utaendelea kuwa mzuri zaidi, na kwetu sisi Tanzania, Kenya ndio nchi ya kwanza kwa uwekezaji kuliko nchi zote za Afrika.
"Tunashirikiana vizuri katika uchumi, watu wetu wanafanya kazi pamoja, yapo makabila yetu ambayo yanaingiliana kwa shughuli zao za kila siku na hata wanyamapori wetu wanazunguka katika nchi zote mbili bila kujali mipaka" amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa Serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na Kenya ulioasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na amewakaribisha wafanyabiashara wengi zaidi wa Kenya kuwekeza nchini Tanzania.
"Kabla ya kuja hapa nimekwenda kutoa heshima katika kaburi la Mzee Jomo Kenyatta, kwa kweli nimeguswa sana na kazi kubwa iliyofanywa na wazee wetu, naomba niwahakikishie kuwa tunawathamini sana ndugu zetu Wakenya na tutaendelea kufanya hivyo" amesisitiza Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake na amemhakikishia kuwa Kenya itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Tanzania."Kwetu sisi Tanzania ni ndugu zetu, ni kaka na dada zetu tunao ushirikiano wa siku nyingi na wa kidugu na tutahakikisha tunauendeleza ushirikiano na uhusiano huu mzuri ulioasisiwa na wazee wetu" amesema Mhe. Kenyatta.
Rais Kenyatta amesema Tanzania na Kenya ni nchi zinazofanana kwa mambo mengi muhimu ikiwemo kubadilishana uongozi wa Serikali kwa njia ya amani na ameongeza kuwa katika mazungumzo yao wamekubaliana kuwa nchi hizi zitaendelea kuzisaidia nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazokabiliwa na matatizo mbalimbali.
Aidha, Rais Kenyatta amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara ya Bagamoyo (Tanzania) hadi Malindi (Kenya) pamoja na mambo mengine ambayo Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili (Joint Commission Cooperation) itayaainisha.
Baadaye leo, Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa katika Ikulu ya Nairobi aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta na Kesho anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na  kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi
31 Oktoba, 2016

#YALIYOJIRI>>>>>HAYA NDIO ALIYOZUNGUMZA RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS KENYATTA JIJINI NAIROBI LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.


Hotubu ya Rais Dkt Magufuli
Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta

#YALIYOJIRI>>>>Mpango wa Kuwalipia Faini Wafungwa wa Mchungaji Lwakatare na Mrema Wapigwa Stop.Fahamu zaidi hapa.

Serikali imesitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.

Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu za jeshi hilo.

Alisema wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.

Mrema alisema jana kuwa mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa.

#YALIYOJIRI>>>>Serikali yakanusha kuuza Kisiwa Shungi Mbili.Fahamu zaidi hapa.

Serikali  imewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Mafia na Watanzania wote kuwa Kisiwa cha Shungi Mbili kilichopo wilayani humo mkoani Pwani, hakijakodishwa wala kuuzwa kwa mtu yeyote kama inavyodaiwa na baadhi.

Badala yake, serikali imeingia mkataba na mwekezaji kwa ajili ya kufanya biashara ya hoteli ya kitalii ya hadhi ya nyota tano katika kisiwa hicho kwa kipindi cha miaka 20, uwekezaji ambao una manufaa zaidi kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopewa jina la Thanda, Meneja Mkuu wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini, Dk Milali Machumu alisema mwekezaji huyo ameingia mkataba huo na serikali kufanya biashara hiyo ikiwa ni sehemu ya kukiendeleza Kisiwa cha Shungi Mbili ambacho kilikuwa hakikaliwi na watu.

“Mimi niwahakikishie tu Watanzania kwamba serikali iliyoko madarakani chini ya Rais John Pombe Magufuli ipo makini na hizo tetesi za kuuzwa kwa kisiwa hiki mzipuuze, kwani kama mnavyoona pamejengwa hoteli ya kitalii kwa makubaliano na serikali na sio kuuzwa wala kukodishwa,” alisema Dk Machumu.

Alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo kutainufaisha serikali kwa kupata mapato kupitia kodi na kutengeneza ajira kwa wakazi wa Mafia pamoja na kuchochea maendeleo na pia wamezingatia sheria ya utunzani wa mazingira ya baharini.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Nunduma alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo kumetoa fursa nzuri ya ajira kwa wakazi wake na pia kutachochea kasi ya maendeleo kwa wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa hoteli hiyo, Pierre Delvaux aliishukuru serikali kupitia kwa Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dk Machumu kwa kuwezesha uwekezaji huo, ambao machakato wake ulianza miaka 10 iliyopita.

Delvaux alisema hoteli hiyo ina vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea, maeneo ya michezo kama tenisi pamoja na vitu vyote vya kufurahisha na gharama yake ni Dola za Marekani 10,000 (sawa na zaidi ya milioni 20) kwa usiku mmoja.

Pia alisema wamezingatia manufaa kwa wakazi wa Mafia na hivyo kwa upande wa ajira asilimia 65 itakuwa ni kwa wakazi wa kisiwa hicho.

“Leo tumeizindua rasmi hoteli hii, lakini itaanza kufanya kazi katikati ya Novemba mwaka huu,” alisema Delvaux.

Kisiwa cha Shungi Mbili ambacho ni sehemu ya Wilaya ya Mafia mkoani Pwani ni miongoni mwa visiwa 15 ambavyo ni maeneo tegefu vilivyopo katika Bahari ya Hindi na hairuhusiwa kufanya shughuli yoyote ya uvuaji wa samaki.

#MICHEZO>>>>YANGA YATUA MBEYA TAYARI KWA AJILI YA MECHI DHIDI YA CITY, MASHABIKI WAWAPA MAPOKEZI YA HESHIMA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 
Yanga wametua mjini Mbeya wakiwa tayari kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, keshokutwa.


Mashabiki na wanachama wa Yanga walijitokeza kwenye Uwanja wa ndege mjini humo kuwapokea vijana wao huku wakiwaonyesha heshima kubwa.
 Yanga inatarajia kufanya mazoezi leo chini ya Kocha Hans van Der Pluijm ili kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya Jumatano.

#BURUDANI>>>>Vanessa Mdee Aja na Muonekano Mpya Sasa Kama Bob Marley.Fahamu zaidi hapa.

 Vanessa mdee ameamua kuingia kwenye utamaduni mpya huku akiwashangaza mashabiki wake
Ameamua kuingia kwenye utamaduni wa watu wa Raggie kama bob marley na lucky dube
Baaadhi ya mashabiki wameonekana kutokubali na muonekano huu

#YALIYOJIRI>>>>Polisi azua GUMZO baada ya kumpigia saluti Profesa Lipumba.Fahamu zaidi hapa.

Kitendo cha askari polisi kumpigia saluti Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba imezua gumzo la kuhoji uhalali wake.

Askari huyo alionekana juzi akimpigia saluti Profesa Lipumba katika eneo la Buguruni ambapo mwanasiasa huyo alienda kushiriki zoezi la usafi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alipoulizwa kuhusu usahihi wa askari polisi kuwapigia saluti viongozi wa vyama vya siasa wasio wabunge alijibu kwa ufupi, “sio sawa.”

Kwa mujibu wa Kanuni za Jeshi la Polisi (PGO) namba 102, haiwataji viongozi wa vyama vya siasa wasio wabunge kati ya watu wanaopaswa kupewa salamu hiyo ya jeshi yenye kuonesha heshima.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Kapteni John Chiligati aliwahi kueleza Bungeni kuwa saluti ni ishara ya kuonesha heshima kwa kiongozi mkuu kwenye asasi za kijeshi.

Kapteni Chiligati alisema kuwa mbali na viongozi wa kijeshi, viongozi wengine wanaopaswa kupewa saluti ni wa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama.

Wengine ni majaji wote, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mahakimu wa mikoa na wilaya wakiwa kwenye mahakama zao.

Katibu Mkuu wa Chama Cha CCK, Renatus Muabhi alisema kuwa huenda askari huyo alipiga saluti kwa kupaniki kutokana na maagizo aliyopewa ya kumlinda Profesa Lipumba katika zoezi hilo.

#TANZIA>>>>Bondia Thomas Mashali afariki dunia.Fahamu zaidi hapa.

Radio Free Africa kipindi cha michezo asubuhi hii wametangaza kifo cha ghafla cha Bondia Thomas Mashali. Thomas ni bondia aliyeleta changamoto kwenye gemu na kuifanya ichangamke.

Chanzo cha Kifo chake inadaiwa kuwa kimesababishwa na kipigo cha wananchi hapa maeneo ya Kimara.

Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.

Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi.

Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta. Inasemekana kuwa hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

Chanzo: Bongo5

Sunday, 30 October 2016

#YALIYOJIRI>>>Basi La Abiria Lateketea Kwa Moto Kimara Stop Over Jijini Dar......Mtu mmoja Afariki, 16 Wajeruhiwa.Fahamu zaidi hapa.

Basi lenye namba za usajili T990 AQF mali ya kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, jana liliteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka, mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja).

Imeelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
 
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
 


Thursday, 27 October 2016

#YALIYOJIRI>>>>‘Rais Magufuli Ndiye Rais wa Kwanza Duniani Kuwa na Asilimia 96%’ Lemutuz.Fahamu zaidi hapa.

Kwa Mujibu wa Gallup Polls by British Institute of Public Opinion iliyofanywa Mwezi uliopita the FACT is utafiiti wao wa kisayansi unaonyesha katika Mwaka wake mmoja madarakani Rais Magufuli amefanikiwa kukubalika sana na Wananchi kwa 96%, utafiti ulifanywa kwa kutumia Mobile Survey through Wananchi 1,813.
– Kwa mujibu wa matokeo hayo Rais Magufuli, amefanikiwa kufanya yafuatayo kwa ufanisi unaokubalika na Wananchi wengi:- (1). Kuishinda Rushwa 75%, (2). TRA sasa ipo on the right track 85%, (3). Education has improved by 75%, (4). Mahakama zetu sasa zipo mstari unaotakiwa kwa 73%, (5). Afya improved by 72%, (6). Maji Safi kwa Wananchi 67%, na kubwa kuliko zote ni Wafanyakazi Serikalini na Mashirika yake sasa wamekuwa 95% kwa Accountability na Fast Response.
– Now Rais Magufuli sio Malaika, na sio siri kwamba Wananchi wote tulikubaliana kwenye uchaguzi uliopita kwamba Taifa letu lilihitaji mabadiliko na tulihitaji kumchagua Rais wa kutuletea mabadiliko, matatizo yetu makubwa ya Taifa siku zote yamekuwa ni Respect to the Rule of Law na Uchumi Mwalimu Baba wa Taifa the greatest ever alikuwa na mapungufu kwenye hizo two lines na zimetusumbua kwa muda mrefu sana hili taifa ni only now Rais Magufuli ameanza kuyatafutia ufumbuzi na matokeo yameanza kuonekana.
– Wananchi wengi hapa Mjini sasa hawana tena pesa za kuchezea kama zamani ambapo ilikuwa kawaidaa kukuta Kijana mdogo akiendesha gari la kifahari na akiwa na mabunda ya Mamilioni ya pesa kwenye gari lake, kuna Vijana hapa mjini walikuwa wakitengewa meza zao kwenye Vilabu vya starehe yaani haruhusiwi kugusa mtu kwa sababu wanatumia pesa nyingi sana wanapokwenda pale, Mikutano ya Bodi za Wakurugenzi wetu mingine ilifikia mpaka kufanyika Johannesburg, au Singapore ambapo wajumbe wa bodi waliruhusiwa kwenda na familia zao, Bandari yetu ilikuwa unakusanya Billioni 40 tu kwa mwezi badala ya Tsh. Billioni 300, na mengineyo mengi ambayo yalisababisha Taifa letu kuwa na tabaka fulani la wachache wenye pesa na wengi Masikini, katika Mwaka mmoja wa Rais Magufuli tumejionea mabadiliko makubwa sana na kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa letu wale walioitwa Vigogo au the untouchables sasa wapo Rumande Keko wanasubiri kesi zao.
– I understand that baada ya kuona hawana upenyo wa kuingilia au kutokea kwenye mfumo mpya wa sasa zaidi ya kutakiwa kufanya kazi zao kwa mistari ya Kisheria, Wapinzani wameamua kutumia Social Media na hasa Media kwa ujumla kumshambulia sana Rais Magufuli, kuna pahali wameanza hata kumsifia Rais JK kwamba ni bora zaidi, lakini hatujawasahu hawa ndugu zetu na tabia yao ya kubadilika badilika kama Kinyonga wakifuatia masilahi yao aidha ya Vyama vyao au binafsi, Waliwahi kutuambia kwamba CUF ni Chama cha Mashoga lakini walipotaka Umoja wa UKAWA wakajiunga nao, Waliwahi kumshambulia sana Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa mpaka walienda mbali sana na kutaka apigwe Risasi hadharani kwa Ufisadi, leo wamebadilika kwamba Ushahidi upo wapi kwa sababu amejiunga nao,
– Infact wameanzisha hoja moja dhaifu sana kwamba mbona Rais JK alikuwa anawaita Wapinzania na kuwasikiliza ushauri wao kwenye uongozi, sasa tunatakiwa kuwauliza kwamba mlikuwa mnamshauri Rais JK on what lines na huku wote tunakubaliana kwamba Taifa lilikuwa limeoza? Rais Magufuli awasikilize nini hasa kizuri mlichowahi kulifanyia Taifa hili huko nyuma? The Americans wanasema kama kuna Kiongozi mahali ameoza basi ni system nzima so kama as a nation tulikubaliana kwa kauli moja kwamba tunataka mabadiliko basi iilikuwa na maana kwamba 360 Degrees U turn ambayo ndio tunayoyapitia sasa yaani total mabadiliko, ninawaomba huko upande wa pili muwacheni Rais afanye aliyoyaahidi kwenye kampeni zake za kuomba Urais na Ilani ya CCM, subirini Mwaka 2020 kwenye uchaguzi unaofuata kwa sasa uchaguzi umekwisha.
– MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
Le Mutuz Nation

Serikali Yatangaza Matokeo ya Mtihani Darasa la 7......Bofya hapa Kuyaona.

Serikali  imetangaza  matokeo  ya  mtihani  wa  darasa  la  7 kwa mwaka 2016  ambapo ufaulu  umeongezeka  kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema  ya  mkoani Shinyanga
AU 

#YALIYOJIRI>>>Sumaye kunyang’anywa shamba na serikali, apewa notisi ya siku 90.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema hati ya shamba lililopo maeneo ya Bunju la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fredrick Sumaye liko katika hatua ya kufutwa na kwamba Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya Kinondoni Rehema Mwinuka ameshatoa barua ya notisi ya siku 90.

Lukuvi ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wandishi wa habari.

“Shamba la Sumaye hati yake iko katika hatua za kufutiwa,
Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ambaye anajukumu la kutoa notisi, ameshatoa notisi kwamba hajaendeleza eneo hilo kwa muda mrefu hivyo kwa mujibu wa sheria hati yake inatakiwa kufutwa,” alisema.

Alisema serikali haitofumbia macho wamiliki wa ardhi na mashamba ambao hawajayaendeleza kwa muda mrefu.

Pia, kufuatia ongezeko la matapeli wanaotumia nyaraka za kughushi za barua za toleo (ofa) zinazodaiwa kutolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi alitoa agizo hususani kwa wakazi wa jiji hilo wanaomiliki ardhi pasipo kuwa na hati miliki, kujisalimisha kwa kupeleka barua zao za ofa kwa Kamishna wa Ardhi ili wapatiwe hati halali.

“Wamiliki wote wanaomiliki ardhi kwa karatasi za ofa halali wazibadilishie ili wapewe hati halali, na atakaegundulika kumiliki ofa feki polisi watawakamata na kupelekwa mahakamani,” alisema.

Alisema asilimia 60 ya watu wanaopeleka kesi za migogoro ya ardhi wizarani, chanzo cha migogoro hiyo ni karatasi za ofa zinazotoka katika halamshauri za jiji na manispaa.

“Natoa miezi mitatu ili karatasi hizi zisitokee tena kila mtu alete barua ya ofa watapewa hati zao ndani ya mwezi mmoja ,wazilete kwa kamishna wa ardhi wa mkoa, baada ya hapo sitasikiliza malalamiko ya watu walioibiwa ardhi wakiwa na ofa ya namna hii.

“Tumieni miezi mitatu vizuri kubadilisha ofa,” amesema.

Hali kadhalika, Lukuvi alipiga marufuku vitendo vya uvamizi wa ardhi na mashamba vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, na kuwataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna shamba au ardhi isiyoendelezwa.

“Serikali ina laani uvamizi wa ardhi na mashamba unaofanywa na baadhi ya wananchi sababu baadhi yao yanamilikiwa kihalali na yana hati, serikali ipo na sheria zipo zitafanya kazi yake,” alisema.

#YALIYOJIRI>>>Mfalme wa Morocco aagwa na Rais Magufuli Jijini Dar es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI jana tarehe 27 Oktoba, 2016 ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.

Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23, Oktoba 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

#YALIYOJIRI>>>>Ripoti ya Mkataba wa Lugumi, Polisi Yafika kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.Fahamu zaidi hapa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projestus Rwegasira amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge ya kuhakikisha mfumo wa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole unafungwa katika wilaya za kipolisi 108 nchi nzima kwa muda wa miezi mitatu.

Zabuni ya kufunga na kusambaza mashine hizo za utambuzi wa vidole katika Jeshi la Polisi ulifanywa na Kampuni ya Lugumi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka, aliwathibitishia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa ripoti hiyo tayari imekabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kaboyoka alisema ripoti hiyo baada ya kukabidhiwa kwa Spika Ndugai ataipitia na baadaye kuiwasilisha kwa kamati hiyo ya PAC.

Juni 30, mwaka huu, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson baada ya kuahirisha Bunge la Bajeti aliiagiza serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ajili ya kuwadhibiti wahalifu na kuitaka Kamati ya PAC ifuatilie suala hilo.

Dk Tulia alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa yenye utata ya kuhusu zabuni yenye thamani ya Sh bilioni 37 ya kufunga mashine hizo katika vituo vyote vya Polisi baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited iliyotolewa mwaka 2011.

“Ninashauri serikali ihakikishe mradi huu unakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo…, mradi huu utasaidia Jeshi la Polisi kuwatambua kwa haraka watu waliohusika katika matukio ya uhalifu mbalimbali,” alisema.

Katika mkataba huo, Lugumi inatakiwa kusambaza na kufunga mashine hizo za utambuzi wa vidole katika wilaya 108 za kipolisi nchi nzima.

Hata hivyo, mashine hizo zilifungwa kwenye vituo 14 pekee wakati tayari kampuni hiyo ilishapokea kiasi cha asilimia 99 za malipo yake.

Katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2013/14 ilionesha kuwa pamoja na kampuni hiyo ya Lugumi kulipwa asilimia 99 ya malipo sawa na Sh bilioni 34, bado haijakamilisha mradi huo kwa muda wa miaka mitano sasa.

Aprili, mwaka huu, PAC iliunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo wa utata baina ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.

Wednesday, 26 October 2016

#BURUDANI>>>>Meneja wa Diamond Platnumz Amemposti Mtandaoni Meneja wa Alikiba.Fahamu zaidi hapa.

 Katika zile lugha za Kimitandao siku ya Jumatano hupewa ‘Kinashi’ cha ‘WCW’ (Woman Crash Wednesday) yaani kumposti Mwanamke aliyekonga hisia zako na kumuhusudu zaidi.

Kilichowashangaza Mashabiki wengi zaidi kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni bifu baina yao.

Leo meneja wa Kimataifa wa Muimbaji Diamond Platnumz, Sallam ‘Mendez’, amemposti Meneja wa Hasimu wao Kibiashara, Mrembo Seven Mosha kama #WCW wake.

#BURUDANI>>>>Ali Kiba Aikana Nyumba Inayoonyeshwa Kwenye Mitandao Kuwa ni yake.Fahamu zaidi hapa.

Ally Kiba aikana nyumba inayoonekana mitandaoni wakisema ni yake, hii ni alipokua akihojiwa kwenye moja ya radio maarufu nchini
.
"Aliyekwambia mi Nina nyumba nani, naishi nyumba ya kupanga hata ingekuwa yangu mi sipendi show off ni maisha yangu" alisema

#MICHEZO>>>>TAMBWE Atokea Benchi Na Kupiga Mbili, Yanga Yaua 4-0.Fahamu zaidi hapa.

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akishangilia baada ya kutokea benchi na kufunga mabao mawili, Yanga ikishinda 4-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Wafungaji wa mabao mengine ya Yanga leo, Obrey Chirwa (kulia) na Simon Msuva (kushoto)

#YALIYOJIRI>>>Asilimia 90 ya Wanafunzi kupata Fedha zao za Mikopo Kesho.Fahamu zaidi hapa.

Wakati baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu wakiendelea kusubiri kupata mikopo yao, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho, asilimia 90 ya wanufaika watakuwa wameshapata fedha zao. 

Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). 

“Taarifa niliyonayo ambayo nimepata asubuhi hii (jana), wachache sana wameanza kulipwa jana (juzi), lakini ulipaji utaendelea mpaka keshokutwa (kesho), tunatarajia kufikia asilimia 90 ya wanaostahili kulipwa watakuwa wameshalipwa,” alisema. 

Majaliwa ambaye ni mhitimu wa UDSM, aliwataka waombaji wa mikopo washirikiane na Wizara ya Elimu kwa kutoa taarifa sahihi ili kurahisisha ulipaji.

“Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi  wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo, taarifa zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” alisema.

Alisema upungufu wa wahadhiri waandamizi umesababishwa na masharti ya ajira za mkataba, unaowataka kuwa miaka 65 na maprofesa kuwa miaka 70.

“Hii inaathiri hali ya utoaji wa taaluma kwa fani za ‘Post-Graduates’. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya mafunzo,” alisema Majaliwa. 

Alisema licha ya juhudi hizo za Serikali, vyuo pia vinatakiwa kuwa na utaratibu wa kurithishana kazi ili kusiwe na pengo katika utoaji wa taaluma pale baadhi ya wahadhiri wanapostaafu.

Majaliwa ambaye pia alizindua kitabu kilichopewa jina la ‘From Lumumba Street to The Upper Hill and Beyond’, alisema Serikali itatoa ushirikiano katika utekelezaji wa mipango ya chuo hicho. 

Akizungumzia kuhusu masilahi  ya watumishi wa vyuo vikuu, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondoa malimbikizo ya madai kwa watumishi wote wa umma na sasa inakamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi ili kubaini watumishi hewa.

 “Serikali inaendelea na maboresho na kuimarisha masilahi kwa watumishi wote wa umma kupitia bodi ya mishahara na mara tutakapokamilisha, tutapanga upya mishahara na motisha kwa watumishi,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo alisema wizara hiyo imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu kwenye chuo hicho zikiwamo maabara. 

Awali, katika hotuba yake, Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala aliishukuru Serikali kwa kuanza kufanyia kazi baadhi ya changamoto zanazokikabili chuo hicho ikiwamo upungufu wa hosteli za wanafunzi.

#YALIYOJIRI>>>>Tanzania Yapata Mkopo Wenye Masharti Nafuu Wa Zaidi Ya Shilingi Bilioni 300 Kutoka Benki Ya Maendeleo Ya Afrika (Afdb) Na Serikali Ya Korea.Fahamu zaidi hapa.

Benny Mwaipaja, WFM, Seoul, Korea
TANZANIA, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Korea ya Kusini zimetiliana saini makubaliano ya pamoja kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme gridi ya Kaskazini Magharibi inayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Kigoma, yenye msongo wa kV 400 mbapo Serikali ya Korea imeahidi kutoa Dola za Marekani milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18, kwa ajili ya kugharamia mradi huo.
 
Hali kadhalika, Tanzania na Benki ya Exim ya Korea, zimesaini  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam.
 
Kwa upande wa Tanzania, Makubaliano pamoja na Mkataba vimesainiwa na Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) Waziri wa Fedha na Mipango kwa niaba ya Serikali, Oktoba 25, 2016 Jijini Seoul nchini Korea Kusini huku upande wa AfDB, aliye saini ni Rais wa Benki hiyo Adesina Akinwumi, na kwa upande wa Benki ya Exim, mkataba huo umesainiwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki hiyo Lee Duk-Hoon.
 
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano na mkataba huo, Dkt. Mpango amesema makubaliano na mkataba vilivyosainiwa vina manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.
 
“Wananchi wa Upande ule waanze kufurahia kwamba maendeleo yanakuja na hasa tunaposema maendeleo ya viwanda ambavyo ni lazima vitumie umeme, na kwamba mradi huu unatarajia kupelekwa hadi Mbeya” Amesisitiza Dkt. Mpango.
 
Dkt. Mpango, amesema kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa pia kwa kuwa serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Magharibi mwa Tanzania, kwa upande wa viwanda vya aina mbalimbali.
 
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji) wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania-TANESCO, Decklan Mhaiki, amesema mradi wa umeme wa Nyakanazi hadi Kigoma utakuwa na urefu wa kilometa 280 na utakapo kamilika utaondoa changamoto ya shirika hilo kuzalisha umeme unatumika katika ukanda huo wa Magharibi hususan Kigoma, kwa kutumia majenereta ambayo uendeshaji wake ni ghali na umeme wake si wa uhakika.
 
“Kuleta laini kama hii, kwanza itapunguza gharama kubwa, na umeme wa ziada utakao zalishwa tunaweza kuuza nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, upande wa pili wa Ziwa Tanganyika, lakini kikubwa ni kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika” ameongeza Bw. Mhaiki.
 
Akizungumzia mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka Jijini Dar es salaam, Dkt. Philip Mpango, amebainisha kuwa mradi huo unatarajia kuwa na tija kwakuwa utatatua changamoto ya majitaka kutuama mitaani hasa wakati wa mvua na kusababisha magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu.
 
Akifafanua kuhusu mradi huo, Mchumi ambaye pia ni  Afisa anayeshughulika na utafutaji wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Melckzedek Mbise, amesema kuwa mradi wa maji wa Ruvu  unatarajia kuongeza wingi wa maji Jijini Dar es salaam, utakaosababisha uzalishaji wa maji taka pia kuongezeka, hivyo mradi huo wa kuondoa maji taka umekuja  wakati muafaka.
 
“Mradi huu umekuja wakati muhimu na mkopo una masharti nafuu sana” Amesisitiza Bw. Mbise.
 
Naye Afisa Mkuu wa utafutaji rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Sabra Issa Machano, amesema kuwa  kati ya nchi 54 za Kiafrika zinazohudhuria mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Afrika, Mjini Seoul Korea, ni nchi nne tu zilizopewa mkopo na ufadhili ambazo ni Kenya, Uganda na Ethiopia, huku Tanzania ikipewa kiasi kikubwa zaidi cha fedha jambo linaloonesha kuwa Tanzania inakubalika Kimataifa.