Wakati
mzunguko wa tano wa Ligi Daraja la Kwanza ukitarajiwa kuendelea kesho
Jumamosi na keshokutwa Jumapili, Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limeagiza makamishna na wakuu wa vituo kuzuia wachezaji
wote ambao hawana leseni kutocheza.
Hii
ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (16), inayosema: “Wachezaji wote
watatambulika kwa kutumia leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na
TFF. Mchezaji yoyote ambaye hatakuwa na leseni hataruhusiwa kucheza
katika mchezo husika.”
Kipindi
cha dharura amvacho TFF ilikitoa ni kwa mizunguko mitatu ya mwanzo,
lakini taarifa za makamishna zinaonyeha kuwa raundi ya nne bado kuna
timu zilikuwa zinatumikia leseni za muda ilihali walikwisha kutaarifiwa
kuwa leseni zao ziko tayari na wao wanakwama kuzifuata hapa TFF. Kuanzia
sasa hakuna sababu yoyote itakayotolewa na ikaeleweka kwa mchezaji
ambaye hatakuwa na leseni.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza, michezo ya Kundi A kesho
itakuwa ni kati ya Pamba ya Mwanza na African Sports ya Tanga kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Dar es Salaam kutakuwa na
‘Mbezi Derby’ ambako Kiluvya United itacheza na Mshikamano kwenye Uwanja
wa Karume, Ilala.
Katika
kundi hilo, Friends Rangers pia ya Dar es Salaam, itacheza na Lipuli ya
Iringa Jumatatu kwenye uwanja huo wa Karume, Dar es Salaam wakati
Jumanne Oktoba 25, 2016 Polisi Dar itacheza na Ashanti United ya Ilala.
Mchezo huo pia utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya Warriors ya Mbeya na Coastal Union
ya Tanga; Kemondo itacheza na Mlale ilihali Polisi Moro itacheza na
Kurugenzi ya Iringa wakati Jumapili Oktoba 23 KMC ya Kinondoni, Dar es
Salaam itacheza na Mji Njombe.
Kwa
upande wa Kundi C michezo yote minne itachezwa kesho Oktoba 22, mwaka
huu ambako Singida United itacheza na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa
Namfuta mjini Singida; Rhino itapambana na Alliance ya Mwanza kwenye
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku Mgambo JKT itakuwa
mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
0 comments:
Post a Comment