Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji
Ussi Gavu amesema Zanzibar inahistoria ndefu ya uvumilivu wa kidini na
kuonya kwamba Serikali itawakuchulia hatua wale wote watakaolete
chokochoko za kidini.
Akizindua
jimbo mpya za ibada za Kanisa la Evangelistic Assemblies of God
Tanzania, Waziri Gavu alisema kwamba tofauti za imani ya dini kamwe
isiwe chanzo cha kuigawa jamii na mifarakano.
“Ndugu
zangu waumini, tofauti za dini isiwe chanzo cha mifarakano katika
jamii, tujiepushe na aina yoyote ya uchokozi au mgawanyiko, daima tuwe
wamoja wenye kuheshimu imani za dini nyengine” Alisema Waziri Issa Gavu.
Waziri
Gavu alisema kwamba ni jambo la aibu kuona watu wanagombana kwa sababu
ya tofauti za imani za kidini. Aliwataka wananchi kuendelea kutunza
amani na kuongeza upendo miongoni mwao.
Alisema
Serikali itaendelea kuheshimu imani za dini na kwamba kila mwananchi
anawajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi na kuonya kuwa Serikali
haitochelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaovunja sheria
za nchi.
Waziri
Issa Gavu alisema kwamba Zanzibar ina historia ndefu ya uvumilivu wa
kidini ambapo pia ina historia kongwe ya dini ya Uislamu na Ukristo.
Amewataka
waumini wa kanisa hilo kuungana na waumini wengine katika kuhimiza
umoja na mshikamano katika jamii na kusisitiza kwamba Watanzania
wanawajibu wa kuishi kwa kuheshimiana, lakini pia kuvumiliana.
Katika
hatua nyengine, Waziri huyo alisema Zanzibar imendelea kuwa sehemu
tulivu na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuitunza amani iliyopo.
Waziri
Gavu alisema kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka huu
ulifanyika katika mazingira tulivu huku waumini wa dini mbalimbali
wakiendelea na shughuli za ibada zao bila kusumbuliwa.
Katika
uzinduzi huo, Waziri Issa Gavu amewahakikishia waumini wa kanisa hilo
kwamba Serikali itanedelea kushirikiana nao ili kuona kwmaba kila
muumini wa dini anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na taratibu
za nchi.
Na Dk. Juma Mohammed, Zanzibar
MWISHO
0 comments:
Post a Comment