Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>WANAOKULA CHAKULA KIBICHI WAKO HATARINI KUPATA KICHOCHO, MINYOO NA MATENDE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Watu milioni 47 nchini wapo katika
hatari ya kupata magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele yakiwemo
Minyoo,Matende na Kichocho, Aidha watu milioni 12.5 wapo hatarini kupata
ugonjwa wa Trakoma huku milioni 4 wakiwa hatarini kupata ugonjwa wa
Usubi.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam
na Ofisa mpango wa kudhibiti magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi
kipaumbele(NTD), Oscar Kaitaba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari
juu ya mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele.
Kaitaba amesema kuwa katika wagonjwa
milioni 47 waliopo hatarini kupata matende, kichocho na minyoo, watu
ambao wapo hatarini kupata ugonjwa wa minyoo ni wale ambao wanakula
chakula ambacho hakijaiva.
Kaitaba ameongeza kuwa katika mpango wa
kudhibiti magonjwa hayo, Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu katika mkoa wa Dar
es Salaam kutakuwa na ugawaji wa dawa za kingatiba za Minyoo ya tumbo
,matende na mabusha ambazo zitatolewa katika vituo maalum
vilivyoteuliwa.
“Vituo hivyo ni pamoja na Stendi za
mabasi , masoko, hospitali, ofisi za serikali za mitaa, ofisi za Wizara,
taasisi na kambi za jeshi na magereza,”alisema Kaitaba.
Alitaja aina za dawa kinga ambazo
zitatolewa kuwa ni Albendazole na Ivermectim na kwamba walengwa ni
wananchi wote kuanzia miaka mitano na kuendelea isipokuwa wajawazito na
watu ambao ni wagonjwa mahututi. Aidha Kaitaba alisema wanatarajia
kufanya upasuaji kwa watu 400 wenye mabusha katika manispaa ya Ilala
ambao utafanyika katika Hospitali ya Pugu Kajiungeni hivi karibuni
0 comments:
Post a Comment