Wakazi
wawili wa Manispaa ya Kinondoni wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa
kukutwa na miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yenye
thamani ya Sh milioni 61.
Walikutwa na miundombinu ya shirika hilo ikiwemo vifaa kwa ajili ya kuunganishia umeme.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 10
jioni katika maeneo tofauti ya manispaa hiyo.
Alisema
katika tukio la kwanza, maeneo ya Makumbusho, polisi wakishirikiana na
kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miundombinu ya Tanesco, walipata
taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo kwa watu wanaohujumu
miundombinu ya shirika hilo.
“Kikosi
kazi walifika eneo hilo katika nyumba ya Wilfred Baruti (45) mkazi wa
Makumbusho na kufanya upekuzi katika nyumba hiyo na vilipatikana vifaa
mbalimbali vinavyotumika kuunganisha umeme vya Tanesco,” alisema
Mkondya.
Aidha,
alisema pia polisi walikwenda katika nyumba nyingine ya Beatrice
Emmanuel (42) mkazi wa Salasala Mabanda Mengi walikofanya upekuzi na
kufanikiwa kukamata vifaa ambavyo ni nyaya aina ya drums mbili, rola ya
nyaya aina ya AICC ya umeme wa milimeta 50 ambazo hutumiwa na Tanesco
kituo cha Kilimahewa cha Kawe, wilayani Kinondoni.
Alisema upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment