Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Kikosi kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao
makuu ya Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa
miundombinu ya serekali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi
lililotokea Mkoana Kagera septemba 10 mwaka huu.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika
kijiji cha Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi, Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho
kinawataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya
ujenzi.
“Hiki kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku
na mchana taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni
pamoja na mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa
waendelee kupata matibabu”alisema.
Alisema mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa
umekamilika kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano
maeneo yote watakayopita kujenga miundombinu ya umma.
Kiongozi wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi
hicho kimekuja Kagera kusaidia serekali ya Mkoa kurudisha miundombinu
yote ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya
kawaida.
0 comments:
Post a Comment