Ligi
ya Taifa na Wanawake itaanza Novemba Mosi, 2016 kama ilivyopangwa awali
kwa kushirikisha timu 12 zilizopangwa kwenye makundi mawili yenye
majina ya ‘A’ na ‘B’. Kila kundi lina timu sita.
Timu
za kundi A lina timu za Viva Queens ya Mtwara, Fair Play ya Tanga,
Mlandizi Queens ya Pwani pamoja na Mburahati Queens, Evergreen Queens na
JKT Queens za Dar es Salaam wakati kundi B zimo Marsh Academy ya
Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Majengo Women ya Singida, Sisters FC ya
Kigoma, Kagera Queens ya Kagera na Panama FC ya Iringa.
Mzunguko
wa kwanza wa ligi hiyo utachukua takribani wiki tatu kwa makundi yote
yaani hadi Novemba 20, mwaka huu na mzunguko wa pili utaanza Januari 4,
2017 hadi Februari mosi, mwakani.
Michezo
ya kwanza kwa kundi A itakuwa ni kati ya Viva Queens na Mburahati
Queens utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara; wakati
Fair Play itacheza na Evergreen ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga ilhali JKT Queens ya Dar es Salaam itakuwa
wenyeji wa Mlandizi ya Pwani kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar
es Salaam.
Kwa
upande wa Kundi B michezo ya kwanza itakuwa ni kati ya Marsh Academy ya
Mwanza itayoonyeshana kazi na Majengo Women FC ya Singida kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Sister ya Kigoma itakuwa mwenyeji
wa Panama ya Iringa kwenye Uwanja wa Tanganyika mjini Kigoma ilihali
Kagera Queens itakuwa mgeni wa Baobab ya Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini humo.
Ligi
hiyo inakwenda kuanza ikiwa na mdhamini mmoja tu ambaye Kituo cha Azam
Tv ambacho kitaonyesha michezo yote bure kupitia king’amuzi chake cha
Azam.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangaza kuwa kungali na fursa ya
kudhamini ligi hiyo kutoka kwa watu binafsi na kampuni mbalimbali ambazo
zitapata kutangazika wakati mechi za ligi hiyo zikiendelea.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa ligi hiyo kwa upande wa wanawake
ambako si tu kwamba itakuza kiwango cha soka kwa wanawake nchini bali
inatarajiwa kuleta hamasa mpya katika mapenzi ya mpira wa miguu.
Pia
benchi la ufundi la timu ya taifa kuweza kugundua vipaji vipya
vitakavyojumuishwa kwneye timu ya taifa ambayo mwakani itaingia kwenye
programu ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake
kutoka kanda ya Afrika. Fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake
zitafanyika mwaka 2019 huko Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment