Watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi hatari, wameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Mbezi kwa Yusuf Makondeni katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi,
Lucas Mkondya, watuhumiwa hao waliuawa katika majibizano ya risasi na
Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha.
Mkondya
alisema wamepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kikundi cha
watu wenye silaha, wamejipanga kufanya tukio la ujambazi kwa kutumia
silaha kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitoka Benki ya Diamond Trust Bank
(DTB), tawi la Barabara ya Nyerere, ambaye angepita katika barabara hiyo
kwenda mkoani Morogoro.
Alisema
baada ya kupata taarifa hizo, polisi waliweka mtego na majambazi hao
wakitumia gari aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T970 DGZ
rangi ya fedha, walionekana wakilifukuza gari la mfanyabiashara huyo,
kisha kulipita na kumsimamisha kwa nguvu.
“Majambazi
wawili wakiwa na bastola walishuka katika gari hilo. Baada ya kugundua
kuwa wameingia kwenye mtego wa polisi, walianza kufyatua risasi kwa
askari wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao
walianza kushuka huku wakifyatua risasi kuelekea kwa askari,” alisema
Kaimu Kamanda Mkondya.
Alisema
kutokana na hali hiyo, askari walianza kujibu mashambulizi na kuwaua
majambazi hao na baada ya upekuzi, zilipatikana bastola mbili, moja ya
kijeshi aina ya Chinese ikiwa na risasi moja ndani ya kasha la risasi;
na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita
ya risasi yaliyookotwa katika eneo la tukio.
Miili
ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa ujambazi.
Katika
tukio lingine la Oktoba 17, mwaka huu saa 2:00 usiku katika maeneo ya
Tegeta Masaiti, watuhumiwa watatu wa ujambazi wakiwa wamepakizana kwenye
pikipiki aina ya Fekon yenye namba MC370 BEY, wakiwa na bunduki aina ya
shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walivamia duka la Abdallah Juma
(46), mkazi wa Tegeta na kupora fedha za mauzo na kuiba vocha za
mitandao mbalimbali, ambazo thamani yake haijafahamika.
“Polisi
baada ya kupata taarifa waliwafukuza majambazi hao, walipoona
wanakaribiwa na askari, walitupa chini begi walilokuwa nalo na
kutelekeza pikipiki yao kisha kukimbia, begi lilipopekuliwa lilipatikana
na silaha hiyo,” alisema.
Aidha, wananchi wenye hasira waliendelea kuwakimbiza majambazi hao na kumuua mmoja huku wengine wakikimbilia kusikojulikana.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Alisema
watuhumiwa hao, Ally Makwega (53) mkazi wa Tandika na Fabian Greyson
(39) mkazi wa Yombo walikamatwa Oktoba 4, mwaka huu saa 6:00 usiku.
Watuhumiwa
hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba MC292 AMD aina ya Boxer
rangi nyekundu, wanayoitumia kufanya uhalifu, wakiwa na funguo bandia 75
ambazo huzitumia katika kuvunja nyumba mbalimbali ya biashara za kulala
wageni, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.
Baada
ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya
uvunjaji wa maghala na kuiba katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na
Dodoma.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment