Siku
chache baada ya Burundi kutangaza maamuzi ya kujitoa kwenye Mahakama ya
makosa ya uhalifu ICC, Umoja wa Ulaya umetangaza kuitenga serikali ya
Burundi kwenye masuala ya fedha za kikosi chake kilichotumwa nchini
Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika kusimamia amani nchini
humo (AMISOM).
Umoja
wa Ulaya, ambaye ni mfadhili mkuu wa Burundi unachangia 20% ya bajeti
ya taifa hilo, umeamua kuchukua vikwazo dhidi ya serikali ya Burundi,
inayotuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kukataa mpaka
sasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani wake.
Serikali
ya Burundi imeendelea kutengwa katika ngazi za kimataifa, na kutuhumiwa
uhalifu mbaya dhidi ya binadamu, Umoja wa Ulaya unataka kuzuia moja ya
sehemu kuu zinazoipatia serikali ya Burundi fedha za kigeni.
Umoja
wa Ulaya umechukua uamuzi wa kutopitisha tena mishahara ya askari wa
nchi hiyo wanaosimamia amani nchini Somalia kwenye akaunti ya serikali.
Uamuzi
wa EU unakuja wakati ambao uchumi wa Burundi umeendelea kudorora, hata
baadhi ya shughuli zinazoingiza mapato kwa serikali zimekwama kutokana
na hali mbaya ya kiuchumi
Ni
wiki tatu sasa tangu Umoja wa Ulaya kutuma fedha kwenye akaunti ya
Umoja wa Afrika ili kulipa mishahara askari wa kikosi cha Umoja wa
Afrika nchini Somalia (AMISOM).
Ripoti
kutoka Brussels Ubelgiji zinasema Umoja wa Ulaya umelipa tu malimbikizo
ya kipindi kinachoishia hadi Machi 16, 2016, tarehe ambayo Umoja wa
Ulaya uliiwekea vikwazo serikali ya Burundi, kwa mujibu wa Ibara ya 96
ya Mkataba wa Cotonou.
Tangu
wakati huo, Umoja wa Ulaya ulisimamisha misaada yake ya moja kwa moja
kwa serikal ya Burundi. Ni Euro milioni 5 tu za mishahara ya askari
5,500 wa Burundi wa kikosi cha AMISOM zimekua zikipitishwa kwenye hazina
ya serikali ya Burundi.
0 comments:
Post a Comment