Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo amekiri
kuwa mtangulizi wake ambaye amefariki dunia, Didas Masaburi alifanya
kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya jiji hilo pamoja na
kulitambulisha katika anga za kimataifa.
Meya
Mwita ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika safari ya mwisho
ya kuuaga mwili wa Marehemu Masaburi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia
Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Binadamu
anapokuwa ameondoka huwa tunazungumza mema aliyoyafanya katika jamii
yetu. Mimi Sikuwahi kufanya nae kazi lakini nimekuta kazi ambazo
amefanya katika halmashauri ya jiji,” amesema.
Ameongeza
kuwa “Moja ya mambo ambayo sitasahau niliyoyakuta aliyoyafanya katika
utawala wake ni kuuleta mradi wa DMDP uliolenga kusukuma na kutaka
kuboresha maeneo ya miundombinu ya DSM, ukiona kazi aliyoacha mimi ndio
naendelea nayo sasa.”
Amesema
jambo lingine alilofanya Marehemu Masaburi enzi za utawala wake ni
kuleta miji mikubwa duniani kuja kuwekeza na kutoa misaada ya
kimaendeleo nchini.
Miongoni mwa majiji aliyoyataja Mwita ni jiji la Hamburg, Shanghai na Torotonto.
“Aliileta
hapa miji mikubwa duniani, mimi napata mialiko sasa katika nchi
mbalimbali na hii ni matunda ya jitihada zake katika kulitangaza jiji la
Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.” amesema.
Pia
Meya Mwita amesema kuwa, Masaburi alifanikiwa kutoa mamlaka na madaraka
ya kiutendaji kutoka serikali kuu hadi serikali za mitaa.
“Alipokuwa
akiongolea dhana kubwa ya kutoa madaraka kutoka serikali kuu kuja
serikali za mitaahili, alikuwa anamaanisha. Jambo hili si jepesi kwa
kuwa, halmashauri za mitaa bila ya kuwa na nguvu kubwa haziwezi leta
maendeleo mfano Kenya na Uganda halmashauri zake zinauwezo na mamlaka ya
kupanga maendeleo,” amesema.
Amesisitiza kuwa “Japo hakufanikiwa kwa kiwango hicho mawazo yake yataishi na mimi kama mrithi wake nitaendelea kuyaenzi.”
Marehemu
Didas Masaburi enzi za uhai wake aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya
Kivukoni, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT).
0 comments:
Post a Comment