Msanii Matonya amewataka watanzania kudumisha amani na mshikamano
walionao sasa, kwani iwapo wataivuruga amani hiyo hawataweza kuirudisha
tena.
Akizungumza
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio iliyokuwa ikiruka moja kwa
moja kutoka Tegeta Jijini Dar es Salaam, Matonya amesema iwapo atafariki
dunia yeye kama msanii anawataka watanzania kudumisha amani hiyo, kwani
ni jukumu lao kuitunza.
“Tanzania tunaijenga katika misingi ya upendo, amani na umoja, tuepuke vita,tuitunze amani, kukiwa na vurugu hata haya tuliyoyafanya leo hayawezi yakakumbukwa, tuyatunze ili watoto na wajukuu zetu waje kusimuliwa baadaye”, alisema Matonya.
Matonya ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya katika muziki, ametangaza kurudi kwake hivi karibuni, huku akikikabidhi kipindi cha Planet Bongo kazi yake mpya ambayo itaanza kurushwa hivi karibuni kwenye vitue vya East Africa Televisiona na East Africa Radio.
Chanzo-Eatv

0 comments:
Post a Comment