IVO na RAIS MUGABE
Kipa
mkongwe nchini aliyewahi kukipiga katika timu za Moro United, Yanga na
Simba, Ivo Mapunda, amesema atastaafu kucheza soka siku akisikia Rais wa
Zimbabwe, Robert Mugabe ametoka madarakani.
Ivo
ambaye anasubiri kwenda kucheza soka Kenya, amesema kwa sasa hana kabisa
mawazo ya kustaafu soka kama ilivyo kwa Rais Mugabe ambaye tangu aingie
madarakani Desemba 22, 1987, mpaka leo bado ni rais wa nchi hiyo.
IVO
Mlinda mlango huyo, pia amewahi kucheza Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia.
Ivo
alisema bado nguvu anazo, hivyo akistaafu soka kwa sasa atakuwa
hajakitendea haki kipaji chake, sasa anasubiri simu kutoka Kenya aende
akacheze soka.“Labda watu wanaotaka kujua nitastaafu lini, niwaambie tu
wasubiri siku wakimuona Mugabe anaachia madaraka ndiyo na mimi hapo hapo
nitaacha kucheza soka,” alisema Ivo.
Mugabe
ndiye rais anaongoza kukaa kwa muda mwingi zaidi madarakani huku
akiendeleza ubabe bila ya woga hata kwa nchi za Magharibi.
SOURCE: CHAMPIONI
Bonyeza Hapa CLICK HERE
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment