Saturday, 3 September 2016

#YALIYOJIRI>>>Afikishwa Mahakamani Kwa Kumuita Rais Magufuli ni Kilaza.Fahamu zaidi hapa.

ELIZABETH Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App.

Akisomewa mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho kilicho kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Wakili Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa huyo aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;

“….Rais kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… f****l** lile, kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”

Hata hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Mtuhumiwa alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.

Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.

#MICHEZO>>>>>ALLARDYCE AANZA KUWATIA HOFU ENGLAND NA UTEUZI WAKE WA KIKOSI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Sam Allardyce ameteua kikosi chake ya Timu ya Taifa ya England kwa mara ya kwanza kabisa kitakachowavaa Slovakia kesho Jumapili, na tayari watu wengi wameonekana kutofurahishwa.

Meneja huyo ameamua kubaki na wachezaji wengi ambao walionesha kiwango kibovu katika michuano ya Euro, na hali hiyo imewaacha watu wengi wakijiuliza kama kweli Allardyce ataonesha utofauti wowote dhidi ya Hodgson kwenye timu hiyo.

Baadhi ya wachezaji hao ni:

Hart, Walker, Cahill, Stones, Rose, Dier, Henderson, Lallana, Rooney, Sterling, Kane.

Bila shaka John Stones inaonekana kabisa atapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa na kwenye kiwango bora kabisa msimu uliopita na kufanikiwa kijiunga na Manchester City.

Hata hivyo wengi wanajiuliza juu ya uwepo wa wachezaji kama Henderson na Kane kutokana na kiwango chao kisichoridhisha kwenye Michuano ya Euro.

Drinkwater ameachwa tena
Washabiki wengi wanajiuliza inakuaje tena mchezaji kama Danny Drinkwater anaachwa halafu Henderson anachukuliwa.


Ni ukweli ulio wazi kwamba msimu uliopita Drinkwater alicheza kwenye kiwango cha hali ya juu mno bila kusahau kwenye mechi hizi za awali za msimu huu licha ya kutokuwepo kwa pacha wake N’Golo Kante ambaye ametimkia Chelsea.

Angalia reactions za washabiki wa England hapo chini;

#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima .Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe.Fahamu zaidi hapa.

RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana  jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama kuna  tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.

Rai Magufuli pia alimtaka Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni  na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo

#BURUDANI>>>Hatimaye Shamsa Ford Afunga Ndoa na Chidi Mapenzi.Fahamu zaidi hapa.

 STAA wa Bongo filamu nchini, Shamsa Ford amefunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo.


Sherehe za ndoa hiyo zilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Shamsa eneo la Sinza, Afrikasana jijini Dar es Salaam.
 
 Awali, Shamsa alidumu katika penzi na Dickson Matoke ‘Dick’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry na kisha  kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara ila baadaye waliachana na kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’  ambaye penzi lao halikudumu.

Friday, 2 September 2016

#YALIYOJIRI>>>>>Rais Magufuli Awasili Pemba Kwa Ziara Ya Kikazi Ya Siku Mbili.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani hapa.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo katika Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezulu Kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.

Akizungumza mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

"Mimi najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa uvumilivu na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pemba

02 Septemba, 2016
.


Rais Magufuli akitazama kikundi cha ngoma baada ya kutua Pemba ambapo pia ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba. Picha na Ikulu

#YALIYOJIRI>>>>Waziri Mkuu Majaliwa Akwama Kuhamia Dodoma.Fahamu zaidi hapa.

SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema baada ya kufika Dodoma, ataanza kuratibu utaratibu wa wizara mbalimbali kuhamia katika Makao Makuu hayo ya nchi.

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza vituo vya Polisi ili kuimarisha ulinzi wakati serikali itakapohamia na hakuna mwananchi atakayenyang’anywa ardhi yake kwa sababu yoyote ile.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Rugimbana alisema kama mkoa walishauri ujio huo ufanyike mara baada ya kikao cha Bunge na Waziri Mkuu ameridhia suala hilo.

Alisema Waziri Mkuu atakuwa Mratibu wa wizara zote kuhamia Dodoma na kazi hiyo ataianza rasmi mara baada ya kuwasili mkoani humo.

Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu umefikia asilimia 90.

Alisema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme aliyekutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya mapokezi ya Waziri Mkuu.

“Awali tulisema atakuja Septemba Mosi lakini baada ya kushauriana tumeona aje mara baada ya vikao vya Bunge kwani pilikapilika nyingi zitakuwa zimepungua, kama serikali ikiamua kuja leo tutaipokea kwani maandalizi ya serikali kuja Dodoma yamekamilika kwa asilimia 70,” alisema.

#BURUDANI>>>Ujumbe Huu wa Vanessa Mdee Kwa Jux wa Wakuna Wengi.Fahamu zaidi hapa.

Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ametumia fursa ya siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, ambaye pia ni Staa wa muziki wa R&B hapa Bongo, Juma Jux kumwandikia ujumbe muhimu kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda huku akiutaja wimbo wao wa pamoja, #Wivu kuwa ndiyo nguzo ya kukutana na kuanzisha uhusiano wao:

Kuoitia ukurasa wake Instagram, Vee Money ameandika;
When we first met I was an upcoming songstress with a fast tongue and one hit song on the radio. You … well you were pretty much the same. Your boy asked me if I would spit some bars on your song. I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a change of heart. Fast forward to 2yrs later, tumekuwa. You’ve got the biggest song in the country #Wivu and a multi million dollar brand #AfricanBoy and as for me well … kitu kimoja hakijabadilika though. Kwako sisikii. Lol! Lakini hayo yoteee ni mifano tu ya jinsi gani ukiwa na mahusiano na mtu anayekujenga kifikra na vinginevyo maisha yako yanaweza kukaa sawa. Siwezi kueleza ni jinsi gani uwepo wako katika maisha yangu yamenibadilisha na kunikuza na kuniboresha. All things are God’s design. Namuomba Mungu akuongoze and akupe maisha marefu sana sana sana. Maisha yenye mafanikio, afya bora na furaha tele. Una moyo wa kipekee sana tofauti na mtu yeyote ninayemfaham. Nasikitika kuwa mbali na wewe leo hii lakini unajua nikipata, umepata na tunazidi kwenda #Juu. Oh by the way kwa mashabiki wetu ngoma yetu ya kwanza ya pamoja inaitwa #Juu 😉 Basi nisaidieni kumtakia mpenzi wangu Heri ya siku ya kuzaliwa.

#YALIYOJIRI>>>Taarifa Ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Kufuatia Habari Iliyoandikwa Kwenye Gazeti La Tanzania Daima.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.

Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili ya kitaasisi ya hali ya juu. 

Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi.  Inaombwa kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.  

Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera. 

Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria,  ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni kumbukumbu zenu vizuri.

Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.

Jeshi letu linafanya shughuli zake ki weredi.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

#BURUDANI>>>>Producer Nahreel Aelekezea Jinsi Alivyokutana na Mpenzi Wake Aika.Fahamu zaidi hapa.

Tunapohitaji kuzungumzia moja kati ya couples za mastaa wa kibongo  zenye muonekano wa kupendeza kwenye macho ya mashabiki na jamii kwa ujumla,lazima utapata list ndefu yenye majina makubwa kama   DAIMOND na ZARI au JUX na VANESSA na wengine kibao


Ila moja kati ya Bombastic couple in town ni ya AIKA na NAHREEL kwa pamoja wanaitwa NAVY KENZO mara kadhaa tumemskia AIKA akielezea namna walivyokutana sasa kwa mara ya kwanza NAHREEL aeleza namna walivyo kutana yeye na mpenzi wake huyo,Nahreel aliongea hayo walipokua katika moja ya show za fiesta mara alipopata nafasi ya kuongea na wanafunzi huko bukoba.


“Aliwaambia wanafunzi, nilikutana naye shule, na mimi nikawaambia, na sasa tunatumia akili yetu ya shule kufanya mziki

#BURUDANI>>>>Video: Diamond na Ne-Yo washoot video ya wimbo wao ‘Marry You’.

Hatimaye Diamond na Ne-Yo wameshoot video ya wimbo wao, Marry You.

Video imefanyika jijini Los Angeles, Marekani. Wimbo huo ulirekodiwa kitambo baada ya Diamond kumfuata Ne-Yo Nairobi alikoenda kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika, msimu wa tatu.

Baada ya hapo wawili hao walikutana tena Marekani kumalizia baadhi ya vipande. Mwezi May, Ne-Yo na Diamond waliuimba wimbo huo pamoja kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwenye tamasha la Jembeka.

Tazama Video Hapa:

#YALIYOJIRI>>>CHADEMA Wagoma Kuhamia Dodoma, Wadai Hawana Mpango Huo.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wazo la kuhamia Dodoma halimo kwenye ajenda zake.
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema chama hicho hakina mpango wa kuhamia Dodoma kwa sababu hayo ni masuala ya kisiasa yasiyo na msingi kiuhalisia.

“Sisi makao yetu makuu yapo Dar es Salaam, hata katiba yetu ndivyo inavyosema, tutaendelea kuwa hapahapa. Hayo ni mambo ya kisiasa yasiyo na misingi ya kiuhalisia, hata mazingira hayaruhusu, kwa hiyo sisi tutaendelea kuwa hapa (Dar es Salaam),” alisema Dk Mashinji.

Chama cha ACT Wazalendo kilisema kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ni miongoni mwa ajenda zake.

#YALIYOJIRI>>>>>Kauli ya CHADEMA Kuhusu Hatua za NHC na Rasilimali za Mwenyekiti Mbowe.Fahamu zaidi hapa.

Kutokana na habari zilizoandikwa leo na vyombo vya habari mbalimbali nchini kuhusu tukio la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kwa madalali wake 'kuvamia' jengo lenye rasilimali za Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe;

Kwa kuwa habari hizo zimehusisha hatua hiyo ya NHC na itikadi au msimamo wa kisiasa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye ni mmoja wa wanahisa wa Mbowe Hotels Ltd ambayo ni mmiliki wa rasilimali hizo zilizovamiwa (Ofisi za Free Media na Club Billicanas) na waandishi wa habari wametutafuta kutaka kauli ya chama juu ya suala hilo;

Katika hatua ya sasa, tunapenda kusema kuwa Chama kitalitolea msimamo suala hilo baada ya kuwasiliana na kushauriana na wanasheria wa Mwenyekiti Mbowe ambao wanalisimamia na kulifanyia kazi suala hilo mahakamani.

Imetolewa, Sept' 2, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

#BURUDANI>>>>Je Kuwa MTU Maarufu Kunawezesha Kufanya Kila Kitu Kwenye Tasnia Mbali Mbali?...Fahamu zaidi hapa.

Imekuwa jambo la kawaida sana kwenye tasnia yetu kumuona mtu maarufu kutaka kuwa kila kitu katika jamii yetu ukimuuliza kwanini utasikia niliambiwa naweza so nikathubutu. Swali ni je kuwa maarufu kunawezesha kuwa kila kitu katika tasnia? Kama kawaida yetu reference kwa wazungu mtu atatoa mfano mbona Arnold aliweza kuwa mtunishaji misuli bora, mwigizaji bora na Governor hahahaha ukweli ni kwamba kila kitu alikipa nafasi na muda wake hakufanya vyote wakati mmoja. Focus yake kubwa ilikuwa awe bingwa wa dunia katika kutunisha misuli akatwa taji hilo.
Akaingia kwenye sanaa ya maigizo akatusua ulimwengu mzima, kuwa mwanasiasa akafanikiwa pia kuwa Governor wa California jiji kubwa kabisa marekani. Then, katoka kwenye siasa karudi kwenye movies .Amefanikiwa kuacha legacy sababu alitoa muda kwa kila career. @Sammisago ni presenter na blog yake ni moja ya blog kubwa zinazotembelewa na watu wengi.

Lakini cha kushangaza leo anataka kuwa mwanamuziki wakati dunia ya habari ndo kwanza inaanza na wale wenye focus walioanza mapema watafaidika zaidi. @divathebawse #AlaZaRoho ingetikisa Afrika kwa uwezo wako mkubwa lakini umekosa focus, muziki tena? @Idrissultan ni moja ya watu ambao ukisikiliza interview zake unaweza amini upeo wake kuhusu focus aliyonayo damn!

Tunakuwa na mtu zaidi ya @Kevinhart4real duniani. Lakini leo anataka kuwa kila kitu. Unakipindi cha radio ambacho ni masaa saba, unataka uwe bora kwenye comedy na kesho unataka kuwa bora kwenye filamu how many percent do you have as an individual? Is true that one can produce tremendously result when he/she does things partially?

 Leo wewe unachukuliwa kama presenter wakati wengine wanakufahamu kama comedian. Je, itawezekana kuruhusu watu wengine kuwa comedians kupitia wewe and wakaifanya 100%? Huu ni ubinafsi na kwann tunaifinya hii tasnia yetu? @Bongo5 chief editor anataka kutoa mixtape, sasa hivi tutawezaje kupata bloggers wakubwa wa kushindana kimataifa kama wote watakuwa wanamuziki?

Thursday, 1 September 2016

#MICHEZO>>>SAMMATA AMEFELI MTIHANI WA LESENI YA UDEREVA, ATAENDELEA KUENDESHWA HADI BAADAYE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta ataendelea kuendeshwa kwa kuwa alifeli katika mtihani ambao ungemuwezesha kupata leseni ya udereva nchini Ubelgiji.

Kama ilivyo kawaida katika nchi za Ulaya, wanaotakiwa kuendesha nchini humo lazima wafanyiwe mtihani.

Samatta alishindwa kufanya vema na kupata maksi ambazo ni sahihi ili kuweza kupewa leseni.


Kutokana na kushindwa, Samatta ataendelea kuendeshwa kwenda na kurudi mazoezini pia kwenye shughuli zake mbalimbali akiwa nchini Ubelgiji.

#MICHEZO>>>>ARBELOA KUTOKA MADRID AREJA LONDON, SAFARI HII AJIUNGA NA WEST HAM UNITED.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Beki wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa sasa rasmi amejiunga na West Ham United inayoshiriki Ligi Kuu England.


Ingawa dau lilikuwa halijawekwa wazi, Arbeloa ambaye aliwahi kuishi London wakati akiichezea Chelsea, amejiunga rasmi na West Ham, leo.

#MICHEZO>>>>NIGEL DE JONG AAMUA KWENDA UTURUKI, AJIUNGA NA GALATASARAY.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kiungo mkongwe kutoka Uholanzi, Nigel De Jong ametua Galatasaray ya Uturuki hadi mwaka 2018.

#MICHEZO>>>>HATIMAYE DIDA AMPUMZISHA BABA YAKE MZAZI KWAO KILIMANJARO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Hatimaye kipa namba moja wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’, amefanikiwa kumsitiri baba yake mzazi.



Dida alifiwa na baba yake ambaye aliugua muda mrefu. Jana wadau, ndugu, jamaa na marafiki upande wa mkoa wa Dar es Salaam walipata nafasi ya kumuaga.




Leo, mazishi yamefanyika matika eneo la Kibosho Munushi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

#MICHEZO>>>>TFF YAMTANGAZA KOCHA MKUU MPYA WA KILIMANJARO QUEENS.FAHAMU ZAIDI HAPA.



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka taifa ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens ambayo kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki mashindano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.

Uteuzi huo wa Nkoma unakwenda sambamba na wasaidizi wake, ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati Meneja wa timu hiyo, Furaha Francis. Mtunza vifaa ni Esther Chabruma maarufu kwa jina la Lunyamila.
Kabla ya uteuzi huo, Nkoma alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ambayo kwa sasa ipo kambi ndogo ya kwenye hosteli za TFF kujiandaa na kambi kubwa itakayofanyika Shelisheli kabla ya kuivaa Congo – Brazzaville kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo. 

Fainali hizo zitapigwa Aprili mwakani, nchini Madagascar.
Kilimanjaro Queens inatarajiwa kuanza mazoezi ya leo, Septemba mosi, 2016 ambako wachezaji watakuwa wanakwenda mazoezini Uwanja wa Karume, Ilala  na kurudi nyumbani hadi Jumapili ambako Jumatatu itasafiri kwenda Uganda kupitia Bukoba mkoani Kagera itakakoweka kambi tena ya siku nne. 

Septemba 8, mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo pia itakuwa njiani kwenda Uganda kwenye mashindano hayo yanayoratibiwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Kwa mujibu wa CECAFA, michuano hiyo itafanyika jijini Jinja na Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda.

Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016 kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.

Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.

Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.

Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa safari ya Uganda.

#MICHEZO>>>>FIFA YATANGAZA MFUMO MPYA WA USAJILI KUTUMIA TMS, MAMENEJA WAELEZWA CHA KUFANYA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE.
 
Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

FIFA limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.

GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.


Kwa mameneja wa usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.

#YALIYOJIRI>>>>Serikali Yashikilia Msimamo Kupinga ndoa za Jinsia Moja.Fahamu zaidi hapa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kushikilia msimamo wake wa kupinga ndoa za jinsia moja,kuongeza uwigo wa uhalalishaji wa utoaji mimba,adhabu ya kifo,kuweka sera ya kutonyonga wanaokutwa na adhabu ya kifo na uridhiwaji wa mikataba ya Kimataifa inayozuia masuala ya utesaji kwa kuwa masuala hayo yanaonekana kutoendana na Katiba na Sheria za nchi, Sera,mila desturi na tamaduni za watanzania ikiwa ni sehemu ya mapendekezo 72 yaliyokataliwa na Serikali wakati wa mapitio ya taarifa ya nchi ya ukuzaji na usimamizi wa haki za binadamu.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Mdemu ameyasema hayoleo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga kikao maalumu cha siku mbili cha wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu ambapo ameeleza kuwa Serikali ilipokea jumla ya mapendekezo 227 yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Mei 2016 chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review).

Mdemu ameongeza kuwa mapendekezo hayo kwa ujumla yalijikita katika majukumu ya Tanzania kwenye mikataba ya kimataifa ,Mifumo ya kikatiba na kisheria,miundombinu ya kitaasisi ya haki za binadamu ,masula ya kisera,ushirikiano na vyombo vya kikanda na kimataifa,utawala wa sheria,uendeshaji haki,masuala ya kulinda haki za msingi za binadamu kama vile haki ya kuishi,haki ya afya,haki za walemavu,watoto,haki ya habari na kujieleza,afya elimu mazingira haki za watu asilia na wakimbizi.

Hata hivyo, Tanzania ilikubali kutekeleza mapendekezo 130 tu kati ya 227 yaliyokuwa yanahusu mchakato wa Katiba,kuijengea uwezo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuhuisha Sera za nchi ili ziendane na malengo endelevu ya Dunia ,kuandaa taarifa za nchi za utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuziwasilisha kwenye vyombo vya vya umoja wa mataifa kwa wakati.

Vilevile Serikali iliahirisha jumla ya mapendekezo 25 ambayo yalijikita katika marekebisho ya sheria ya Takwimu, 2015, Sheria ya makosa ya mtandao, 2015,ukamilishaji wa Sheria ya Habari, Sheria ya vyombo vya Habari,uandaaji wa mikakati na mipangokazi ya utekelezaji wa msuala ya kuzuia ndoa za utotoni na za kulazimishwa ,upitishaji wa sera mpya mbalimbali ikiwemo ya kutoa vyeti vya kuzaliwa na usajili wake kuwa bure na masuala ya uchaguzi Zanzibar, kwa lengo la kuyapitia tena kwa kina na kushirikisha zaidi wadau ili hatimaye kuweka msimamo stahiki kabla mapendekezo hayo hayajawasilishwa tena Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa hatua za mwisho za kupitisha rasmi taarifa ya nchi katika kukuza na kulinda haki za Binadamu.

Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kulinda na kukuza haki za bindamu ikiwa ni pamoja na kupokea hoja na maoni ya wadau ili kuboresha taarifa ya nchi itakayowasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la umoja wa mataifa kabla au ifikapo tarehe 9 Septemba, 2016 na kuwataka watanzania wote kushiriki ipasavyo katika dhana nzima ya kukuza na kulinda haki za bindamu nchini.

Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za binadamu nchini mwao.

Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufungaji wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo.

AG2-Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakimsikiliza Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu wakati wa ufungaji wa kikao kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam.

#YALIYOJIRI>>>Cheyo: Rais Magufuli ni Rais aliyesubiriwa tangu kuanza kwa uhuru.Fahamu zaidi hapa.

Na: Lilian Lundo-Maelezo
Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais aliyesubiriwa kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Uhuru.

Cheyo ameyasema hayo alipokuwa akielezea juu ya utendaji wa Rais Magufuli tangu ameingia madarakani Novemba, 2015.

“Utendaji wa Rais Magufuli umewashtusha watu wengi kwani hawakutegemea kwa muda mfupi aliokuwa madarakani kama angeweza kuchukua hatua kubwa kama vile kupambana na mafisadi, jambo ambalo limekuwa likiongelewa na viongozi waliopita lakini kulikuwa hakuna matunda ya moja kwa moja,” alifafanua Cheyo.

Ameendelea kwa kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa na adhima ya kupambana na Mafisadi na kutatua kero za Taifa tangu akiwa kwenye kampeni huku akisimamia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Vile vile Cheyo amesema kuwa kero ambazo amekuwa akizitatua Rais Magufuli zikiwemo ufisadi, uchumi tegemezi, mapato madogo na ukosefu wa vifaa mahospitalini ni kero ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na kambi ya upinzani kwa muda mrefu.

Hivyo kuingia kwa Rais Magufuli madarakani kumeleta utatuzi mkubwa kwa kero hizo ambazo zimekosa utatuzi kwa muda mrefu kutokana na viongozi waliopita kutozichukulia uzito mfano Rais Magufuli alivyoweza kutatua tatizo la vitanda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kipindi kifupi ambapo hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala nchini katika hospitali hiyo.

Akielezea suala la ufisadi nchini, Cheyo amesema kuwa ufisadi ni ugonjwa wa muda mrefu ambao umepoteza fedha nyingi za nchi kutokana na mikataba mibovu iliyokuwa ikisainiwa na viongozi wa juu.

Aidha amempongeza Mhe. Rais kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuona tatizo hilo lishughulikiwe kisheria na kwa njia maalum ili kukomesha ufisadi nchini.

Cheyo amewataka watanzania kugeuza mawazo yao na kuchukia rushwa kwa kukataa kupokea na kutoa rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na inarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

#YALIYOJIRI>>>>Kamati ya Bunge yaibana Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi.Fahamu zaidi hapa.

Wabunge wameibana Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni katika kipindi kifupi kiasi ambacho hakilingani na kazi wanayoifanya. 

Kwa kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa lawama kwa kuchelewesha mikopo, kushindwa kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo kwa vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa 1,000. 

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele ya kamati hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na kwamba wanaweka mikakati mizuri ya kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi zaidi. 

Wakizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao walisikitishwa na kitendo cha bodi hiyo kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. 

Walisema isipobadilika katika utendaji wake, kuna haja ya Serikali kuivunja na kuchagua benki moja kusimamia shughuli hiyo. 

“Mnatakiwa kuongeza juhudi na mikakati ili kuhakikisha kwamba madeni yote yanakusanywa kwa wakati la sivyo naona kuna haja ya Serikali kuivunja bodi nakutafuta njia nyingine,” alisema Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Raisa Mussa. 

Mbunge wa Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka alihoji kwa nini pamoja na bodi hiyo kuwa na mameneja 18 na wafanyakazi wa kudumu 144, bado utendaji wao umekuwa siyo wakuridhisha.

“Kwa idadi yenu tulitegemea kupata ripoti inayojitosheleza na hata utendaji wenu ulitakiwa kuwa wa ufanisi zaidi,” alisema.

Akijitetea zaidi, Badru alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi yake lakini kwa sasa wamepiga hatua kubwa katika ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika wa mfuko huo.

“Kwa mfano Mei mwaka huu tulikusanya kiasi cha Sh2 bilioni na Juni tulikusanya Sh6 bilioni,” alisema. 

Aliongeza kuwa ipo mikakati mingi ambayo wamejiwekea katika kuhakikisha kwamba bodi hiyo inakusanya madeni kikamilifu kutoka kwa wadeni wake wote. 

“Kwa kupitia mikakati yetu, tumeweza kuongeza idadi ya wanafunzi ambao tunawapa mikopo kutoka 42,729 hadi 123,783. Katika kipindi hicho fedha za mikopo zimeongezeka kutoka Sh56 bilioni hadi kufikia Sh465.3 bilioni,” alisema.

#YALIYOJIRI>>>Video:Ndege za Kivita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Zikivinjari Anga la Jiji la Dar es Salaam Leo Hii.


VIDEO: NDEGE ZA KIVITA ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) ZIKIVINJARI ANGA LA JIJI LA DAR ES SALAAM HII LEO.

#YALIYOJIRI>>>>Umati wa Watu Wakesha Wakisubiri Kupatwa Kwa Jua.Fahamu zaidi hapa.

Umati wa watu umepiga kambi eneo la Rujewa, wakisubiri tukio la kupatwa kwa jua kipete linalotokea baadaye leo.
Katika eneo hili ambalo awali halikuonekana kuwavutia wapita njia hata kufaa kutumika kama sehemu ya kujiburudisha kutokana na shughuli ya uchimbaji mawe na upasuaji kokoto, usiku huu watu wamejaa huku watu wakijiburudisha.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia watu wakiingia na kutoka eneo hilo, ambalo wataalam wa anga wameweka mitambo yao kwa ajili ya kuratibu tukio hilo la kihistoria.

Mama lishe, wachoma nyama na wauzaji wa vinywaji vikali wapo kazini kuwahudumia watu waliofika kushuhudia tukio hilo.

“Kwa kweli tukio hili ni kukumbukwa, muda kama huu ninakuwa nyumbani lakini hawa watu  lazima wahudumiwe,” mamalishe Christina Mgaya.

Hata hivyo, uhaba wa nyumba za kulala wageni katika mji mdogo wa Rujewa umesababisha baadhi ya wageni kukosa sehemu ya kulala na kukesha eneo hilo.

#YALIYOJIRI>>>>Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba.Fahamu zaidi hapa.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufuatia mvutano wa kusimamishwa uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Profesa Lipumba kumuandikia barua Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akilalamikia kusimamishwa uanachama bila kufuata utaratibu huku akitaka kurejeshwa kwenye nafasi yake ya uenyekiti.

Ofisi hiyo imeutaka uongozi wa CUF kueleza kwa kina hatua ilizopitia hadi kufikia uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, na kwamba iwasilishe barua hiyo kufikia kesho majira ya saa 9:30 alasiri.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Monica Laurent amesema kuwa ofisi hiyo ilipokea barua ya Profesa Lipumba Agosti 29 mwaka huu ikiwa na malalamiko na kwamba wametaka uongozi wa CUF kutolea majibu.

“Tumeitaka CUF kutoa majibu kuhusu malalamiko ya Profesa Lipumba, ndipo sisi tutakapotoa majibu,” amesema Monica.

Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti mwaka jana akipinga uamuzi wa chama chake kumuunga mkono Edward Lowassa kugombea urais, amerejea na kudai kutengua barua yake ya kujiuzulu.

Baraza Kuu la CUF lililoketi visiwani Zanzibar hivi karibuni lilimsimamisha uanachama Profesa Lipumba pamoja na viongozi wengine 10 akiwemo Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya aliyekuwa Naibu Katibu mkuu (Bara).

Hata hivyo, Profesa Lipumba amepinga uamuzi huo akieleza kuwa kikao cha baraza hilo kililiwa batili.

#YALIYOJIRI>>>>Kauli 10 Nzito Alizotoa Mbowe, Akiahirisha Ukuta.Fahamu zaidi hapa.

Mbowe

 LEO mchana, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa, ametangaza uamuzi wa kuahirishwa kwa maandamano na mikutano ya chama hicho nchi nzima iliyopangwa kuanza kesho, anaandika Charles William.

Zifuatazo ni kauli kumi zilizotolewa na mwenyekiti huyo wa Chadema, wakati akitangaza kuahirishwa kwa operesheni hiyo maarufu kama Ukuta, iliyotawala vyombo vya habari vya ndani na nje pamoja na mitandao ya kijamii kwa zaidi ya mwezi mmoja.

1.“Tunajua uamuzi huu utawaumiza sana wafuasi wetu, na uamuzi huu umeniumiza sana hata mimi mwenyewe, lakini ni nani miongoni mwa viongozi wetu na wanachama wetu ambaye anaweza kuombwa kuahirisha jambo na viongozi wa madhebu na dini zote hapa nchini na akawakatalia?”

2.“Polisi na Serikali wajue kuwa, hatuahirishi maandamano na mikutano yetu kwa sababu ya mazoezi, risasi au mabomu ya polisi. Hatuahirishi kwasababu ya usafi wao, wanaofanya kesho na wala hatuahirishi kwasababu ya ndege za kijeshi zinazoruka, ila tumeamua kuwaheshimu viongozi wetu dini.”

3.“Tunawaomba wanachama wetu, wapenzi wetu na wapenda demokrasia kote nchini watusamehe na wakubali kuwapa viongozi wa dini hizi wiki tatu, watafute suluhu kwa kuonana na Rais na ikishindikana, hatutarudi nyuma. Tutaingia barabarani.”

4.“Tangu tulipotangaza operesheni Ukuta, jumla ya wanachama na viongozi wetu 230 katika maeneo mbalimbali wamekamatwa na kushitakiwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi na jumla ya viongozi na wanachama wetu 28 wapo rumande mpaka sasa pasipo sababu za msingi.”

5.“Haikuwa rahisi sisi kufikia uamuzi huu, hatukuwa tayari kurudi nyuma. Lakini viongozi wa dini na taasisi zinazoheshimika hapa nchini wametusihi. Mpaka Mama Maria Nyerere ameongea na Mheshimiwa Lowassa na kutuomba tuahirishe ili watafute suluhu ya suala hili.”

6.“Hatuogopi mabomu wala risasi za polisi, tuna uwezo wa kuandamana kwasababu tunazo mbinu za kufanikisha mipango yetu. Juzi polisi walitukamata na kuzuia kikao cha Kamati Kuu ila jana tumekifanya na wala hawajui tumefanyia wapi na saa ngapi.”

7.“Wakati tukifanya harakati hizi, tunaendelea pia kufungua kesi sehemu mbalimbali. Tundu Lissu na jopo lake tayari wameandaa mashitaka 15 ili tuweze kuyafungua katika mahakama zetu hapa nchini. Tutadai haki mahakamani na tutaidai barabarani.”

8.“Inasikitisha sana kuona taifa lina rais anayeomba watu wamuombee kila siku, ‘Niombeeni jamani’, lakini amekuwa akijaribu kuwakwepa viongozi wa dini kila wanapotaka kumuona ili kuzungumza naye kuhusu amri haramu ya kuzuia mikutano ya hadhara.”

9.“Viongozi wa dini walituomba wiki mbili au tatu ili wafanye mazungumzo na Rais Magufuli, sisi tumewapa mwezi mzima kabisa, ili wasake suluhu ili sisi kama vyama vya siasa tupewe haki yetu ya kisheria na kikatiba. Ikishindikana hakika sisi hatutarudi nyuma.

10.“Salum Mwalimu bado yupo rumande kwasababu za hovyo, Polisi wamekataa kumpeleka mahakamani leo wanadai wapo ‘busy’ eti wanazuia maandamano ya UVCCM, yalipangwa kufanyika leo. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa lakini hatutarudi nyuma.


#YALIYOJIRI>>>>Kuahirisha Ukuta, Polisi Wapumua.Fahamu zaidi hapa.

JESHI la Polisi limepumua baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuahirisha mikutano na maandamano yao, anaandika Pendo Omary.
Hatua ya kuahirisha mikutano na maandamano iliyotangazwa kufanyika chini ya mwavuli wa operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta), imepongezwa na Simon Sirro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kulikuwepo na vuta nikuvute kati ya Chadema na serikali kuhusu Ukuta hivyo kuzua taharuki na hisia za kutokea machafuko iwapo juhudi za kutafuta suluhu zingeshindikana.

Maandamano hayo yalitarajiwa kuanza kufanyika kesho lakini leo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho ametangaza kusitisha kwa kile kilichoelezwa, uchaguri wa taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuisha mazungumzo ya taasisi hizo na Rais John Magufuli.

“Nawashukuru sana viongozi hawa kwa uzalendo waliouonesha kwa kusimamisha mikutano na maandamano yao.

“Ila kuhusu kesho, wananchi wasishangae kuona magari yetu yakipita barabarani wakajiuliza kulikoni wakati Chadema wametangaza kutoandamana. Sisi kama Jeshi la Polisi bado tupo kwenye oparesheni zetu za kupambana na wahalifu,” amesema Siro.

Aidha, Sirro amesema oparesheni inayoendeshwa na jeshi hilo katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam inaendelea vizuri na mpaka sasa tayari linawashikilia watuhumiwa zaidi ya 20 baada ya kufanya msako mkali.

“Watu zaidi ya 20 wamekamatwa. Wengi wanaeleza namna wanavyolifahamu tukio (mauaji ya askari wanne), lakini wengine ni wahusika katika matukio mengine ya uharifu. Ukamataji bado unaendelea katika maeneo ya Vikindu na Dar es Salaam,” amesema Sirro.

#YALIYOJIRI>>>>Rais Magufuli Afungua Mkutano Mkuu Wa Wahandisi, Atembelea Kikosi Cha Anga Majumba Sita Ukonga.Fahamu zaidi hapa.

Na Sheila Simba-MAELEZO


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.

Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.

“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.

Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.

“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli

Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.

“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.

Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.

“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda

#YALIYOJIRI>>>>Deni Analodaiwe mh Mbowe na NHC Madalali Wavamia Ofisi za Tanzania Daima na Kuanza Kutoa Vitu nje.Fahamu zaidi hapa.

 Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa Tanzania Daima wako kwenye crisis kubwa kwasababu watu wanaodaiwa kuwa ni Madalali wa shirika la nyumba la Taifa la NHC wamefika ofisini kwao asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa vyao vyote nje ofisini.


Madalali wa NHC sasa wanatoa vitu nje kwenye ofisi za Mmiliki wa Tanzania Daima gazeti ambalo inahisiwa linamilikiwa na mh Mbowe.

Nadhani mtakumbuka siku kadhaa zilizopita mkurugenzi wa NHC ndugu Nehemia Mchechu alimtaja Mbowe kama miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo na kudai alishamuandikia notisi yakulipa deni notisi ambayo imeisha jana.