Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>Waziri Mkuu Majaliwa Akwama Kuhamia Dodoma.Fahamu zaidi hapa.
SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia
rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge
vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema baada ya kufika Dodoma,
ataanza kuratibu utaratibu wa wizara mbalimbali kuhamia katika Makao
Makuu hayo ya nchi.
Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza vituo vya Polisi ili
kuimarisha ulinzi wakati serikali itakapohamia na hakuna mwananchi
atakayenyang’anywa ardhi yake kwa sababu yoyote ile.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Rugimbana alisema kama
mkoa walishauri ujio huo ufanyike mara baada ya kikao cha Bunge na
Waziri Mkuu ameridhia suala hilo.
Alisema Waziri Mkuu atakuwa Mratibu wa wizara zote kuhamia Dodoma na
kazi hiyo ataianza rasmi mara baada ya kuwasili mkoani humo.
Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu umefikia asilimia 90.
Alisema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme aliyekutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya mapokezi ya Waziri Mkuu.
“Awali tulisema atakuja Septemba Mosi lakini baada ya kushauriana
tumeona aje mara baada ya vikao vya Bunge kwani pilikapilika nyingi
zitakuwa zimepungua, kama serikali ikiamua kuja leo tutaipokea kwani
maandalizi ya serikali kuja Dodoma yamekamilika kwa asilimia 70,”
alisema.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>> Adam Malima Aliyekuwa Mbunge Mkuranga-CCM,akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo hilo,Ally Ungando Kimanzichana hapo jana
Aliyekuwa Mbunge Mkuranga-CCM AdamMalima,akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo hilo,Ally Ungando Kimanzichana jana
Mgombea Mwenza CCM,Samia Suluhu akihutubia umati wa wanachi katika mkutano wa kampeni Kimanzichan… Read More
#MICHEZO>>>Matokeo ya michezo ya jana ligi kuu Uingereza yako hapa.
Everton 3 - 1 Chelsea FT
Everton mfungaji ni @Steven Naismith aliefunga mabao (3) Dakika za (17, 22 na 82)
huku Chelsea mfungaji ni @Nemanja Matic ambae amefunga bao moja … Read More
Breaking News>>Mgombea Ubunge Jimbo la Lushoto Mohmed Mtoi afariki dunia.Fahamu zaidi hapa.
Mgombea Ubunge Jimbo la Lushoto, Mohmed Mtoi afariki dunia kwa ajali ya gari akitokea kwenye kampeni zake huko Tanga.
Mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema jimbo la lushoto ambaye pia ni mratibu wa… Read More
#YALIYOJIRI>>Mgombea Mwenza CCM Samia Suluhu akionyesha kadi za CUF na Chadema, kutoka kwa wanachama waliohamia CCM Ikwiriri, Rufiji.Fahamu zaidi hapa.
Samia Suluhu Mgombea Mwenza CCM akionyesha kadi za CUF na Chadema, kutoka kwa wanachama waliohamia CCM Ikwiriri, Rufiji.
Bi MwanahawaSaidi akitangaza kuhama CUF kurejea CCM,kwenye Mkutano wa Mgombea Mwenza … Read More
#Breaking News>>>Kumekucha MABIBO Ujioo wa SAID KUBENE hii leo atakuwa na mkutano maeneo ya MABIBO MPAKANI.
… Read More
0 comments:
Post a Comment