MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE.
Shirikisho
la Soka la Kimataifa(Fifa), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake,
likiwamo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa
usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System
Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa
mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.
FIFA
limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao
malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda
timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa
kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS
Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.
GPX
ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’
unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima
mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu
kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi
husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.
Kwa
mameneja wa usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL),
Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL)
watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja Usajili wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya
kujiunga na mtandao wa GPX.
0 comments:
Post a Comment