Na: Lilian Lundo-Maelezo
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP John Cheyo amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ni Rais aliyesubiriwa kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Uhuru.
Cheyo ameyasema hayo alipokuwa akielezea juu ya utendaji wa Rais Magufuli tangu ameingia madarakani Novemba, 2015.
“Utendaji
wa Rais Magufuli umewashtusha watu wengi kwani hawakutegemea kwa muda
mfupi aliokuwa madarakani kama angeweza kuchukua hatua kubwa kama vile
kupambana na mafisadi, jambo ambalo limekuwa likiongelewa na viongozi
waliopita lakini kulikuwa hakuna matunda ya moja kwa moja,” alifafanua Cheyo.
Ameendelea
kwa kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa na adhima ya kupambana na
Mafisadi na kutatua kero za Taifa tangu akiwa kwenye kampeni huku
akisimamia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.
Vile
vile Cheyo amesema kuwa kero ambazo amekuwa akizitatua Rais Magufuli
zikiwemo ufisadi, uchumi tegemezi, mapato madogo na ukosefu wa vifaa
mahospitalini ni kero ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na kambi ya
upinzani kwa muda mrefu.
Hivyo
kuingia kwa Rais Magufuli madarakani kumeleta utatuzi mkubwa kwa kero
hizo ambazo zimekosa utatuzi kwa muda mrefu kutokana na viongozi
waliopita kutozichukulia uzito mfano Rais Magufuli alivyoweza kutatua
tatizo la vitanda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kipindi kifupi
ambapo hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala nchini katika hospitali hiyo.
Akielezea
suala la ufisadi nchini, Cheyo amesema kuwa ufisadi ni ugonjwa wa muda
mrefu ambao umepoteza fedha nyingi za nchi kutokana na mikataba mibovu
iliyokuwa ikisainiwa na viongozi wa juu.
Aidha
amempongeza Mhe. Rais kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuona
tatizo hilo lishughulikiwe kisheria na kwa njia maalum ili kukomesha
ufisadi nchini.
Cheyo
amewataka watanzania kugeuza mawazo yao na kuchukia rushwa kwa kukataa
kupokea na kutoa rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na inarudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
0 comments:
Post a Comment