Mshambuliaji
 wa Genk, Mbwana Samatta ataendelea kuendeshwa kwa kuwa alifeli katika 
mtihani ambao ungemuwezesha kupata leseni ya udereva nchini Ubelgiji.
Kama ilivyo kawaida katika nchi za Ulaya, wanaotakiwa kuendesha nchini humo lazima wafanyiwe mtihani.
Samatta alishindwa kufanya vema na kupata maksi ambazo ni sahihi ili kuweza kupewa leseni.
Kutokana
 na kushindwa, Samatta ataendelea kuendeshwa kwenda na kurudi mazoezini 
pia kwenye shughuli zake mbalimbali akiwa nchini Ubelgiji.
 








 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment