Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>>SIMBA Vs Yanga: Mabomu ya machozi yalindima Uwanjani.Fahamu zaidi hapa.

Mashabiki wa Simba uzalendo uliwashinda baada ya bao la Amissi Tambwe na
kumua kurusha viti uwanjani wakipinga bao hilo, kutokana na kitendo
hicho askari wa kutuliza ghasia waliamua kurusha mabomu ya machozi
jukwaani.
Mabomu hayo ya machozi yaliwafanya mashabiki wa Simba waliofurika
uwanjani hapo kuanza kukimbia hovyo kujinusuru na mabomu hayo huku
wengine wakitoka nje kabisa ya uwanja. Mashabiki baadhi wameumia
kutokana na vurugu hizo.
Kutokana na vurugu hizo mchezo huo ulisimama kwa dakika kadhaa kabla ya
mwamuzi Martin Saanya kutoa kadi nyekundu kwa nahodha wa Simba, Jonas
Mkude.
Awali baada ya bao la Yanga, mzee mmoja shabiki wa Simba aliyevalia jezi
nyekundu alitaka kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Yanga.
Kitendo hicho kiliwaudhi makomandoo wa Yanga ambao walimkamata na
kuanza kumpiga kabla ya askari wa kutuliza ghasia kuingilia kati
kumnusuru na kipigo hicho.
Kabla ya mechi kuanza Mzee huyo alikuwa amekaa katika mlango wa kuingilia vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji wa Simba.


Related Posts:
SAMATTA AMJIBU ROONEY, ATUPIA, NAYE ATUPIA, EVERTON, GENK ZAMALIZANA 1-1
Everton imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya.
Mshambuliaji mpya wa
Everton, Wayne Rooney amefunga bao lake la pili akiwa na Everton lakini
Mtanzania Mb… Read More
MBWANA Samatta Awapiga Chenga za Mauzi Mabeki wa Ajax na Kutupia Bao.
Mshambuliaji wa KRC Genk, Mtanzania, Mbwana Samatta akiwatoka wachezaji
wa Ajax katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu jana Uwanja wa
mazoezi wa The Ajax Future timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
Mbwana Samatta alifu… Read More
Aliyemvamia Mchezaji Wayne Rooney Uwanjani Asamehewa Kwa Amri ya Makamu wa Rais Samia Suluhu.
MMOJA wa mashabiki wa Tanzania waliofika kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaamamejitoa ufahamu na kumvamia mshambuliaji wa Everton, Wayne
Rooney kwa nia ya kumkumbatia wakati wa mchezo dhidi ya&n… Read More
KIKOSI CHA TAIFA STARS KINACHOIVAA RWANDA AU AMAVUBI KWAO KIGALI LEO.
Kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza leo dhidi ya Amavubi, hii ni kuelekea CHAN 2018 Kenya.
1. Aishi Manula
2. Boniphace Maganga
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Salim Mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mz… Read More
YULE KIUNGO WA ZAMANI YANGA ALIYEICHEZEA SIMBA, AMETUA MBEYA CITY.
Kiungo wa zamani wa Yanga na Coastal Union, Bakari Masoud ambaye ilionekana atasaini Simba, ametua Mbeya City.
Masoud amejiunga Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili na tayari kuanza kazi mara moja.
Kiungo huyo aliy… Read More
0 comments:
Post a Comment