Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>>>ALLARDYCE AANZA KUWATIA HOFU ENGLAND NA UTEUZI WAKE WA KIKOSI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Sam Allardyce ameteua kikosi chake ya Timu ya Taifa ya England kwa
mara ya kwanza kabisa kitakachowavaa Slovakia kesho Jumapili, na tayari
watu wengi wameonekana kutofurahishwa.
Meneja huyo ameamua kubaki na wachezaji wengi ambao walionesha
kiwango kibovu katika michuano ya Euro, na hali hiyo imewaacha watu
wengi wakijiuliza kama kweli Allardyce ataonesha utofauti wowote dhidi
ya Hodgson kwenye timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji hao ni:
Hart, Walker, Cahill, Stones, Rose, Dier, Henderson, Lallana, Rooney, Sterling, Kane.
Bila shaka John Stones inaonekana kabisa atapata nafasi ya kuanza
katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa na kwenye kiwango bora kabisa
msimu uliopita na kufanikiwa kijiunga na Manchester City.
Hata hivyo wengi wanajiuliza juu ya uwepo wa wachezaji kama Henderson
na Kane kutokana na kiwango chao kisichoridhisha kwenye Michuano ya
Euro.
Drinkwater ameachwa tena
Washabiki wengi wanajiuliza inakuaje tena mchezaji kama Danny Drinkwater anaachwa halafu Henderson anachukuliwa.
Ni ukweli ulio wazi kwamba msimu uliopita Drinkwater alicheza kwenye
kiwango cha hali ya juu mno bila kusahau kwenye mechi hizi za awali za
msimu huu licha ya kutokuwepo kwa pacha wake N’Golo Kante ambaye
ametimkia Chelsea.
Angalia reactions za washabiki wa England hapo chini;
Related Posts:
Vikosi vya Yanga na Mbeya City vinavyoanza leo.
Hivi ndio vikosi vya Yanga pamoja na Mbeya City vinavyoingiaUwanja wa Taifa jioni hii kwenye menchi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
YANGA:
1. Beno Kakolanya
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Vicent Bossou
5. Na… Read More
KAZI YA SERENGETI BOYS GABON INAANZA JUMATATU, ANACHOAMINI SHIME HIKI HAPA.
Kocha
wa timu ya taifa vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime
amesema watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya Mali katika mchezo wao
wa kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa keshok… Read More
SERENGETI WAREJEA TAIFA STARS, WAIDHAMINI NA KUMWAGA SH BILIONI 2.1.
Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL), imeingia mkataba wa miaka mitatu kuidhamini
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wenye gharama ya shilingi bilioni
2.1 za Kitanzania.
Katika
pesa hizo, Serengeti watakuwa wakiipa… Read More
Waziri Mwakyembe aipongeza Klabu ya Afrika Lyon.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
ameupongeza uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon kwa kutumia
mchezo wa mpira wa miguu kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa
tembo.
Mtendaji … Read More
HANS Poppe: Yanga Musishangilie Ngoma Bado ipo Uwanjani.
Hans Poppe amewaambia Yanga wasijiamini na kuona kuwa tayari
wameshauchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kwa sababu tu bado
wana mechi nyingi mkononi, tofauti na Simba.
Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 62, sawa… Read More
0 comments:
Post a Comment