Saturday, 3 October 2015

#YALIYOJIRI>>>Edward Lowassa apokelewa Pemba na Maelfu.Fahamu zaidi hapa.

 MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Mhe: Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni na kufanyika uwanja wa mpira Tibirinzi Chake chake Pemba.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mumungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Mh. Edward Ngoyayi Lowassa amewataka wananchi kisiwani Pemba kumkataa na kutomchagua mgombea yeyote anayechezea amani ya nchi kwani nchi hii si miliki ya mtu bali ni mali ya watanzania wote, na kusisitiza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anapambana na umasikini kwa nyanja zote.


Mh.Lowassa aliyewasili kisiwani Pemba na kusindikizwa na vijana kwa pikipiki za Vespa na magari hadi hapa kiwanja cha Kibirinzi ambapo mkutano wa kampeni ulifanyika, aliwataka wananchi wa Pemba kumkataa mgombea anayetishia amani na utulivu, kwani ndiyo itakayoweza kusaidia kufikisha malengo ya kuleta mageuzi ya kweli katika nyanja zote za maendeleo, na kuahidi kuwa ataimarisha hospitali kila wilaya kwa kuweka vifaa vya kisasa.

Mh. Lowassa amesisitiza kuwa endapo atakuwa rais wa Tanzania, atahakikisha anabadilisha mitaala ya elimu kuwa ya kisasa ili kuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania.

Awali, mgombea mwenza Mh. Juma Duni Haji aliwataka Wazanzibari kushirikiana ili kufanya mabadiliko kwa amani na utulivu. Naye mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi, CUF Malim Seif Sharif Hamad ameendelea kusisitiza kuwa chama chake hakina mpango wa kufanya vurugu kama inavyodaiwa.

 MGOMBEA Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA UKAWA Mhe: Juma Duni Haji, akizungumza na wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni na kufanyika uwanja wa mpira Tibirinzi Chake chake Pemba.
 WAGOMBEA ubunge na uwakilishi wa majimbo 18 ya Pemba, wakinadiwa na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya CHADEMA chini ya UKAWA, kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Tibirinzi Chake chake Pemba.
 WAGOMBEA urais Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mgombea mwenza Juma Duni Haji (kulia), wakijadili jambo kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa Tibirinzi Chake chake, ambapo kulifanyika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mgombea urais wa Muungano wa tiketi ya CHADEM Mhe: Edward Lowassa.
 MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF chini ya UKAWA, maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, waliohudhuria mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe: Edward Lowassa na kufanyika uwanja wa mpira Tibirinzi Chake chake Pemba
 NAIBU Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI Mussa Kombo, akiwasalimia wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, waliohudhuria mkutano wa hadhara, uliohutubiwa na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, kupitia UKAWA Mhe: Edward Lowassa na kufanyika uwanja wa mpira Tibirinzi Chake chake Pemba.

0 comments:

Post a Comment