Hofu
ilitanda jana katika kiwanda cha MM Steel cha jijini Dar es Salaam,
baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mashine ya kusajili wapigakura kwa
mfumo wa elektroniki (BVR) inatumika kuandikisha wafanyakazi katika
kiwanda hicho. Kutokana na hofu hiyo, baadhi ya maofisa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwanasheria wa chama hicho,
John Mallya, Polisi na Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec), walifika kiwandani
humo na kufanya upekuzi ikiwamo kuondoka na baadhi ya vifaa vilivyokuwa
vinatumika. Baada ya kukubaliana pande zote, vifaa hivyo ambavyo ni vya
kuchukua alama za mikono, macho, scanner na kompyuta mpakato,
vilichukuliwa na Polisi ili baadaye vikakabidhiwe Nec.
0 comments:
Post a Comment