Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Mgombea Ubunge ACT-Wazalendo amwombea kura Lowassa.Fahamu zaidi hapa.
Mgombea ubunge wa ACT - Wazalendo kwa Jimbo la Arusha Mjini, Estomih
Malla jana baada ya kupanda jukwaani alimwombea kura za ndiyo mgombea
urais Tanzania kupitia CHADEMA, Edward Lowassa.
Akihutubia
mkutano wa kampeni uliokuwa na lengo la kunadi pia sera na kumwombea
kura mgombea wa chama chake, Bi. Anna Mnghwira, katika Uwanja wa Stendi
Kubwa, mkoani Arusha alisema:
“Jamani naombeni mtambue kuwa mimi ni msomi ambaye nina shahada
(Hakuitaja ni ya nini), kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitumia elimu
yangu kwa faida ya familia yangu tu baada ya kufukuzwa udiwani na
Chadema, sasa naombeni mnichague ili niitumie pia kuwatumikia kwa
kuwaletea maendeleo yaliyoshindikana kupatikana kwa miaka mitano,”
“Mimi ni mkweli, nipeni ridhaa ya kuwaongoza na msisahau kumpa ridhaa
ya kuwa rais mheshimiwa Edward Lowassa, naamini hamtajutia kura zenu,”
alisema Malla.
Alipoulizwa baada ya kumaliza mkutano wake kwa nini amemnadi Lowassa
badala ya mgombea urais wa chama chake, Malla hakutaka kujibu bali
alipanda gari lake na kuondoka.
- Habari hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti MWANANCHI
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Wilaya 43 ziko Hatarini Kukumbwa na Njaa.Fahamu zaidi hapa.
Serikali imesema kuwa nchi ina hifadhi kubwa ya chakula kutokana na
mavuno ya msimu uliopita ingawa kuna wilaya 43 zenye upungufu wa chakula
kutokana na mavuno yao kuwa chini hali iliyosababishwa na mabadiliko ya
tabia n… Read More
#YALIYOJIRI>>>Mahakama Yaizuia NHC Kupiga Mnada Mali za Freeman Mbowe.Fahamu zaidi hapa.
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Ardhi imeliamuru Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kutouza au kupiga mnada mali za Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mpaka kesi ya msingi
itak… Read More
#YALIYOJIRI>>>>PICHA:Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.Fahamu zaidi hapa.
Msafara
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu
Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo
ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao … Read More
#YALIYOJIRI>>>>Polisi Wamhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob.Fahamu zaidi hapa. .
Maofisa
wa Polisi wamemhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kabla
ya hajakutana na waandishi wa habari kwa madai kuwa wamepata taarifa
mkutano wake huo ulilenga kumkashifu Rais John Magufuli.
Maof… Read More
#YALIYOJIRI>>>Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA.Fahamu zaidi hapa.
JUMUIYA
ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa
miezi mitatu kujua hatima ya wao kusaini Mkataba wa Kiuchumi na Jumuia
hiyo (EPA).
Uamuzi
huo ulifikiwa jana Ikulu Dar es Salaam na vio… Read More
0 comments:
Post a Comment