Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akihutubia wakati
akifungua mkutano wa wadau wa takwimu wadau wa maendeleo Endelevu Jana
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa maendeleo Endelevu
(SDG’S) ambao shabaha yake kubwa iliukuwa kuweka mifumo ya namna ya
kutekeleza mpango huo Jana jijini Dar es Salaam
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda akizungumza
katika mkutano wadau wa maendeleo Endelevu Jana jijini Dar es Salaam.
Hayo
yalisemwa Jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa
wadau wa maendeleo Endelevu (SDG’S) ambao shabaha yake kubwa iliukuwa
kuweka mifumo ya namna ya kutekeleza mpango huo.
Alisema
kuwa utoaji wa taarifa hizo ni makubaliano ya kidunia katika mpango wa
utekelezaji Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDG’S)
Alisema kuwa kuwa mpango wa awali uliokuwa ukijulikanana kama Mpango wa
Maendeleo wa Milenia MDG’S ulikuwa na malengo manane, huku yakiwemo
mapungufu kadhaa kama vile masuala ya kiuchumi ,Ajira,tofauti ya kipato
na mataifa mengine pamoja na Mazingira.
Aliendelea kufafanua kuwa Malengo Mapya 17 yaliyosainiwa hivi karibuni
huko newyork Nchini Marekani na marais kutoka katika mataifa mbalimbali
duniani,yamezingatia mapungufu hayo nakusema kuwa katika utekelezaji wa
Mpango huo wa miaka 15 hali ya kiuchumi,Ajira,Elimu,huduma ya Umeme wa
viwanda pamoja Ubora itaboreshwa zaidi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha Profesa Aldoph Mkenda
amesema serikali itachukua hatua ya kuzitafsiri taarifa na kuziweka
katika Lugha ya Kingereza na Kiswahili ili kusaidia wanachi kusoma na
kuelewa kwa urahisi.
Mpango
wa Maendeleo wa Milenia (MDG’S) umemalizika hivi karibuni na sasa
unatarajiwa kuanza Mpango pya wa Maendeleo Endelevu SDG’S ambao utaanza
kutekelezwa January Mosi 2016 na kufikia tamati mwaka 2030.
Baadhi
ya viongonzi mbarimbari na wananchi walio hudhulia mkutano huo leo
jijini Dar es Salaa.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii) Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa serikali imesema itakusanya takwimu na kuchapisha
taarifa kwenye mitandao ya kijamii ili wananchi waweze kutoa maoni juu
ya maendeleo ya Taifa Jana.
Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment