Thursday 6 October 2016

#Picha>>>>Waziri Mkuu alipotembelea wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba mkoani Dodoma.Fahamu zaidi hapa.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.


Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.
 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jumatano, Oktoba 5, 2016wakati alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.
 
Alisema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu ushindani wa soko.
 
“Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,” alisema.
 
Pia Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na kupanua biashara.
 
Alisema tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Picha: Ofisi ya Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabasaba Oktoba 5, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016.

0 comments:

Post a Comment