LICHA ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika utoaji huduma wa magari yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART), Kampuni inayoendesha mradi huo, UDART imepiga marufuku usafiri wa bure kwa makundi mbalimbali wakiwemo askari polisi, walemavu, viongozi wa dini na hata walimu.
Imesema mageti yaliyokuwa wakiyatumia yafungwe na kila mmoja alipe. Udart imetoa taarifa hiyo katika waraka uliobandikwa katika kila kituo mwishoni mwa wiki na kufafanua kuwa kumekuwepo na ongezeko la makundi hayo, wakipita katika mageti hayo bila kulipa na pia kupokea simu kutoka katika makundi mbalimbali, yakiomba kupatiwa huduma hiyo.
Hilo limo katika waraka uliosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa na nakala kwenda kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Msajili wa Hazina na kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).
Katika taarifa hiyo, Mgassa alitaka waraka huo ufike kwa watumishi wote wa usafiri huo na hatua zichukuliwe haraka. Alisema watumishi waliopo katika vituo wanapaswa kuhakikisha mageti yanakuwa yamefungwa kwa ufunguo na hakuna anayeruhusiwa kupita bila kulipa.
Makundi hayo yalikuwa yakisafiri bila kulipa nauli katika mradi huo unaofanya kazi katika Barabara ya Morogoro na ile ya Morocco jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment