Wakati vyuo vikuu vikikaribia kufunguliwa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imelaumiwa kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika huku yenyewe ikisema itahakikisha majina yanatolewa sanjali na tarehe za vyuo kufunguliwa.
Pia, HESLB imesema miongoni mwa vipaumbele vitakavyozingatiwa kwenye utoaji wa mikopo katika mwaka wa masomo 2016/2017 ni kwa wanafunzi wenye mahitaji makubwa, waliotoka kwenye kaya masikini, waliosoma shule za kata na waliotoka vijijini.
Kauli
hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kutupiwa lawama kwa kuchelewa kutoa
majina ya wanufaika wa mikopo kabla hawajaripoti vyuoni, hasa wanafunzi
wa mwaka wa kwanza.
Mkurugenzi
wa mtandao wa haki za wanafunzi (TSNP), Shitindi Venance alisema hadi
sasa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa
kwanza wa masomo 2016/2017, ambao wameomba mkopo bado hawajui ni kiasi
gani wamepewa.
Malalamiko
ya Shitindi yamerejea kilichotokea mwaka jana baada ya wanafunzi
kuripoti vyuoni, lakini majina yalipotolewa na bodi hiyo baadhi yao
hawakuwa wanu- faika hali iliyosababisha usumbufu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema miongozo ya utoaji wa
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni tofauti na mwaka
jana.
“Utaratibu
wa mwaka huu ni tofauti kwa kuzingatia wanafunzi wanaoanza masomo na
wale wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali,” alisema Badru.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kuwa majina ya wanufaika wa mikopo yataanza kutolewa
kwa kuzingatia tarehe ambayo chuo husika kinafunguliwa.
“Kila
chuo kinafunguliwa kwa mujibu wa tarehe iliyopangwa kwa hiyo na sisi
tunatoa majina kuendana na utaratibu wa chuo husika,” alisema.
Hata
hivyo, Badru alisema uta- ratibu wa kupanga viwango vya mikopo kwa
wanafunzi na kisha kutoa orodha ya majina ya wanufaika haihusishi bodi
ya mikopo peke yake.
Alisema
kabla ya kuidhinisha majina ya wanufaika na mikopo, lazima Tume ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TCU) iwe imeshatoa orodha ya majina wa wanafunzi ambao
imewadahili kwa kuzingatia vigezo vyao, halafu majina hayo yatumwe
vyuoni.
Alisema mzunguko wote huo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu ndiyo maana huchukua muda.
0 comments:
Post a Comment