Thursday, 10 November 2016

#YALIYOJIRI>>>Picha:Nyumba mpya atakayohamia Rais Barack Obama baada ya kutoka White House.

Rais wa Marekani Barack Obama atapanga nyumba Washington, D.C baada ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani (White House) hapo mwakani ambapo rais mwingine wa taifa hilo ataapa kushika madaraka baada ya Barack Obama kumaliza mihula yake miwili ya uongozi.

Nyumba hiyo ilijengwa mwaka 1928, ina vyumba 9 vya kulala, vyumba 8 vya kuogea. Nyumba hiyo yenye muonekano wa kuvutia iliuzwa zaidi ya dola milioni 5 (TZS bilioni 10.9) mwaka 2014.

Rais Obama amesema kuwa yeye na familia yake watabaki Washington baada ya kutoka Ikulu ya Marekani (White House) Januari 2017.

“Tutaendelea kuishi in Washington D.C. hadi hapo Sasha (Binti yake mdogo) atakapohitimu sababu kumhamisha mwanafunzi shule katikati ya muhula ni ngumu” alisema Rais Obama.


 Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 
<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>

0 comments:

Post a Comment