Kinda wa Azam FC Farid Musa anaendelea kufanya vizuri kwenye majaribio nchini Hispania akiwa na Club Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza ‘Segunda Division’.
Yusuf Bahkhesa ambaye ameambata na Farid Musa nchini humo amekuwa ikiipa www.shaffihdauda.co.tz updates za hapa na pale kuhusu yote yanayomuhusu Farid katika majaribio yake.
Kiwango cha Farid kimeivutia timu ya Tenerife na iko tayari kumsajili kwa mkopo wa miaka miwili.
Klabu ya Tenerife ya nchini Hispania imeshamfanyia vipimo vya afya Farid na ipo tayari kumsajili kwa mkopo wa miaka miwili endapo atafuzu vipimo vya afya.
Yusuf Bakhresa (kulia) ameambatana na Farid Musa nchini Hispania kushuhudia kinda huyo zao la Azam Academy akihudhuria majaribio yake katika kuhakikisha anapata timu ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Uwepo wa Farid nchini Hispania unamfanya akose michezo iliyobaki kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL)
Farid hakuwepo kwenye mchezo wa FA Cup wakati Azam ikifuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga Mwadui kwa penati 5-3 baada ya sare ya kufungana magoli 2-2. Akaukosa pia mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji, Azam iliposhinda 2-0.
Farid huenda akaiwahi mechi ya fainali ya FA Cup dhidi ya Yanga ambayo itakuwa ndiyo mechi yake ya mwisho ya mashindano katika msimu huu wa 2015-2016.
Club Deportivo Tenerife ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Segunda División yenye jumla ya timu 22.
0 comments:
Post a Comment