Siku
chache baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani
Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi
unaomsafisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Kalanga alisema kuwa Lowassa
hamiliki shamba hilo la Makuyuni kwakuwa tangu Rais wa Serikali ya Awamu
ya Tatu, Benjamin Mkapa alipofuta hati ya umiliki wa shamba hilo kutoka
kwa raia wa Kigeni aliyemtaja kwa jina la Stein, bado halijamilikishwa
rasmi kwa wananchi na ndio ilikuwa hoja yake.
Alisema
kuwa maelezo ya Lukuvi hayakuwa na ukweli na kwamba alichanganya kati
ya shamba hilo la Mkuyuni na shamba la Manyara Ranchi ambalo hati yake
ilifutwa tangu mwaka 2000 na kukagawiwa kwa wananchi wa Monduli ambapo
Lowassa alisaini hati miliki yake kama muwakilishi wa wananchi wa Wilaya
hiyo kwakuwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya Ardhi
(Tanzania Land Trustee (TLCT).
“Jambo
la kushangaza ni pale Waziri alipochanganya shamba hilo na lile la
Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kugawiwa
kwa wananchi. Hati miliki ya shamba hilo la Manyara Ranchi ilisainiwa na
Lowassa ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Land
Trustee(TLCT),” alisema
Awali,
Waziri Lukuvi alieleza kuwa Shamba hilo la Mkuyuni linapaswa
kumilikishwa kwa wananchi lakini nyaraka zinaonesha kuwa hati yake
imesainiwa na Lowassa na kwamba Serikali itamnyang’anya na kulirejesha
kwa wananchi.
Juzi,
Lowassa aliahidi kuwasiliana na Mbunge huyo ili kufuatilia kauli
aliyoitoa Waziri Lukuvi dhidi yake kuhusu kujimilikisha shamba hilo ili
aweze kutoa ufafanuzi kwani hakuna ardhi anayoimiliki kinyume cha
taratibu.
0 comments:
Post a Comment