Rais Mteule wa Ufilipino, Rodrigo Duterte (pichani) aliyepewa jina la utani la ‘Digong’, anayejiandaa kuapishwa mapema mwezi ujao amegoma kuishi katika Ikulu ya nchi hiyo akidai kuwa kuna mizimu.
Rais huyo mteule ambaye tangu alipotangazwa kuingia madarakani ameshawashangaza wengi kwa uamuzi wake hasa wa kukataa maisha ya kifahari ya urais ikiwa ni pamoja na kudai atauza ndege ya kifahari yenye hadhi ya Rais na kununua magari ya huduma za dharura nchini kwake, ametoa msimamo wa kutoishi Ikulu alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni. Amesema kuwa alikuwa kuwa aliwahi kuwa katika Ikulu hiyo maarufu kama ‘Malacañang’ alipokuwa msaidizi wa Rais aliyepita na kwamba alikuwa akiona mizimu na mashetani mengi.
“Nilikuwa nikimfanyia kazi Rais Gloria Arroyo, kama mshauri wa kitaalam wa masuala ya sheria, siku moja aliniita majira ya saa nane usiku. Nilipelekwa katika eneo la kupumzika lenye michoro ya marais waliopita wakati nikimsubiri avae. Marais [kwenye michoro]walikuwa kwenye mapozi tofauti lakini wote walikuwa wakiangalia mbele. Upepo ulikuwa ukivuma. Lakini kila nilipokuwa nikiangalia picha wote walikuwa wakiniangalia mimi,” alisema.
Alieleza kuwa alianza kuona mauzauza usiku huo na kushindwa kuendelea kumsubiri Rais na badala yake aliondoka. “Put—ng ina. Lalabas ako dito. (Son of a bitch, I’m out of here). Nabuang na ni (It’s crazy),” alieleza kwa kifilipino na kutafsiriwa kwa kiingeza.
Duterte alikuwa Meya wa jiji la Davao kwa zaidi ya miaka 10, na sasa anatarajia kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi huu.
Alisema baada ya kuapishwa, angependa akaishi eneo lingine nyumbani kwake kama wafanyavyo watu wengine
0 comments:
Post a Comment