Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
Makongoro
Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende
(kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road
jijini Dar.
WAFANYAKAZI
wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya
Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata
pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi
Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni
(Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa
akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es
Salaam ambapo mauti yalimfika.
Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za
mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es
Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao
Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko. Bwana alitoa na Bwana
ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro
mahali pema peponi-Amina.
Makongoro
Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu
cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.
0 comments:
Post a Comment