Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe
amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli ameonyesha kuwa hataki mchezo
kwenye serikali yake baada ya jana kutengua nafasi ya Waziri wa Mambo ya
Ndani.
Rais Magufuli jana ametengua uteuzi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mheshimiwa Charles Kitwanga baada ya kuingia bungeni na kujibu swali
linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa. Zitto Kabwe
amedai kuwa kitendo kilichofanywa na Rais ni kama kutuma salamu kwa
watendaji wake kuwa hataki mchezo.
“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja kuwa hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘no nonsense'” Zitto Kabwe.

0 comments:
Post a Comment