Jeshi
la Polisi Zanzibar limeahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Shariff Hamad kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wake.
Katika
barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba
ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo
yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano
itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.
Barua
hiyo ya Mei 26 imenukuu barua ya awali ya Mei 22, 2016 iliyomuita
mwanasiasa huyo makao makuu ya polisi Zanzibar kwa mahojiano kuhusu,
“masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa visiwa hivi.”
Kutokana
na hatua hiyo, Maalim Seif aliyetarajiwa kuwasili jana saa 3 asubuhi
Zanzibar kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa aliahirisha safari
hiyo na kuwasili Saa 10 jioni kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya kichama kuanzia leo katika wilaya saba za Unguja.
0 comments:
Post a Comment