WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Mei 23, 2016)
kwenda Lusaka, Zambia kuhudhuria Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (51st Annual Meeting of the Board of Governors of
the African Development Bank – AfDB) utakaofanyika kesho (Jumanne, Mei
24, 2016).
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo ambao utafunguliwa na Rais wa Zambia, Edgar Lungu utajadili masuala ya Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi.
Pia
utahudhuriwa na Marais Idriss Deby wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda na
Uhuru Kenyatta wa Kenya. Nigeria itawakilishwa na Makamu wake wa Rais,
Yemi Osinbajo huku Msumbiji ikiwazilishwa na Waziri wake Mkuu, Carlos
Agostinho do Rosário.
Watu
maarufu waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Kofi Annan,
Ashish Thakkar, John Kufuor, Mary Robinson, Mo Ibrahim, Nancy Lee,
Ngozi Okonjo-Iweala na Tony Elumelu.
Mkutano
huo utakaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha
Mulungushi (Mulungushi International Conference Centre) utahudhuriwa na
washiriki zaidi ya 5,000 kutoka nchi 54 ambao ni wanachama wa benki
hiyo, washiriki kutoka nchi 26 ambazo si za bara la Afrika (non-regional
member countries), wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wadau wa
maendeleo na wawakilishi wa asasi za kiraia. Wengine ni Mawaziri wa
fedha, biashara na uchumi na wataalamu kutoka vyuo vikuu.
Waziri
Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji,
wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.
0 comments:
Post a Comment