Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>>WAPINZANI WA YANGA CAF WAANZA KUTOA SABABU.Fahamu zaidi hapa.
TIMU ya soka ya Medeama ya Ghana,
imesema itakuwa shughuli pevu kukutana Yanga SC ya Tanzania katika hatua
ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sababu sasa inafundishwa
na kocha wao wa zamani, Mholanzi Hans van der Pluijm.
Mtendaji Mkuu wa Medeama, James
Essilfie amesema hayo baada ya kupangwa droo ya makundi ya Kombe la
Shirikisho, wao wakiangukia Kundi A pamoja na Yanga, TP Mazembe ya DRC
na Mo Bejaia ya Algeria.
“Yanga inafundishwa na Hans Van der
Pluijm, kocha wa zamani wa Medeama na kucheza nao itakuwa mechi nzuri,”
alisema na kuongeza; “Tumefurahishwa na makundi, timu nyingine katika
kundi zitasaidia kuonesha ubora wa Medeama.
Wengi walitilia shaka uwezo wetu
tulipopangiwa Mamelodi Sundowns (ya Afrika Kusini) katika hatua ya
mchujo, lakini tumethibitisha ubora wetu,” amesema Essilfie ambaye timu
yake iliitoa Mamelodi na kuingia kwenye makundi.
0 comments:
Post a Comment