Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi katika Kampuni ya Simu ya TTCL, kuwaachia vijana kwa kuwa sekta ya mawasiliano hivi sasa ina ushindani mkubwa.
Akizindua
nembo mpya ya kampuni hiyo na mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE
jana, Profesa Mbarawa alisema wazee wamekuwa watu wa kuzungumza zaidi
ofisini, kuliko kufanya kazi na kubuni mbinu mpya zenye kuhimili
ushindani.
Mbarawa
alisema uzinduzi wa nembo mpya katika kampuni hiyo, hautakuwa na maana
ikiwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hawatabadilika na kutoa huduma
zitakazowavutia wateja.
Aliishauri
menejimenti kutoajiri watumishi kwa kujuana, bali watoe fursa kwa
vijana wenye uwezo wa kuhimili ushindani unaotokana na mabadiliko ya
teknolojia ya mawasiliano.
Aidha,
aliwataka vijana kutumia fursa hiyo kwa kuchapa kazi ili TTCL yenye
sura mpya ifike mbali kimaendeleo na kuwa kati ya kampuni bora zaidi za
mawasiliano nchini.
Aliongeza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua thabiti za kuboresha na kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini na kusimamia vyema huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ili zisaidie katika jitihada za nchi kujiletea maendeleo.
Alisema sekta ya habari na mawasiliano inagusa shughuli nyingi za maisha yetu ya kila siku, kijamii, kiuchumi na kimaendeleo na kuongeza kuwa hivi sasa huduma hizi sio tena jambo la ziada katika maisha ya kila siku bali ni huduma za msingi zenye kipaumbele cha juu katika maisha.

Akizungumzia
maombi ya wananchi ya kutaka kusogezwa mbele kwa siku ya kuzima simu
feki, waziri alisema Serikali haitasogeza mbele siku hiyo.
“Siku
ya Juni 16, mwezi ujao Serikali itazima simu na vifaa vingine vya
mawasiliano feki bila kuongeza muda, huu ni muda wa watu kujiandaa,” alisema.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo, Edwina Lupembe alisema TTCL
wakati wowote kuanzia sasa itaanzisha huduma ya usafirishaji wa fedha
kama zilivyo kampuni nyingine za mkononi.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema mabadiliko ya nembo
hiyo yametokana na kampuni hiyo kuongeza huduma zinazotolewa kwa
wateja.
0 comments:
Post a Comment