Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri
kwamba anatoka kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya
kufilisiwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani. Akiongea
katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho kinatarajiwa kuruka
Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na Mkongo
ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano alikuwa
ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu yakulala.
Jacqueline Wolper na Mkongo
Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.
Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka WCB.
0 comments:
Post a Comment