KAMPUNI
ya Sky Group Associates inayomiliki mgodi wa tanzanite wa TanzaniteOne,
imesema Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya amepotosha Bunge na umma
juu ya suala zima la ununuzi wa hisa kwa kampuni hiyo.
Akichangia
bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki, Millya alisema
Sky Group Associates iliyonunua hisa kwa Kampuni ya TanzaniteOne na
kumiliki kitalu C Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara,
haikufuata taratibu za ununuzi wa hisa hizo na kuwatuhumu baadhi ya
mawaziri kuwa walihusika katika kupindisha taratibu.
Aliwataja
mawaziri hao kuwa ni George Simbachawene na Jenista Mhagama, ambaye
hata hivyo alikanusha madai hayo ; na ametaka taratibu za Kibunge
zimlamzishe Millya, kukanusha au kuthibitisha madai yake.
Mbali
ya hilo, mbunge huyo aliituhumu kampuni hiyo kwa kuwafukuza kazi
wafanyakazi 201, bila ya kufuata utaratibu na kwamba inawanyanyasa .
Akizungumza
na mwandishi wetu, Mwanasheria wa kampuni hiyo, Kisaka Mnzava alisema
uongozi umesikitishwa na kauli ya Millya, kwa kusema alitoa kauli bila
kufanya utafiti wa kina.
Mnzava
alimtaka mbunge huyo, kujiridhisha kwa kufanya utafiti wa kina namna
hisa za TanzaniteOne zilivyouzwa kwa Sky Group, inayomilikiwa na wazawa
kwa asilimia 100.
Alisema
wamiliki wa hisa wanajulikana na kama anahitaji kuwafahamu, anapaswa
kwenda Mamlaka ya Usajili wa Leseni za Kampuni (Brela) kujiridhisha.
Alisema hakuna waziri wala kiongozi yeyote mwingine wa serikali, anayemiliki hisa katika Sky Group Associates.
Alisema kampuni imeshalipa kodi yote ya serikali, na kampuni hiyo sio ya mfukoni, kama anavyodai mbunge huyo.
Mnzava
alisema shughuli za uzalishaji zinasimamiwa kikamilifu kati ya Sky
Group na serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambao ni
wabia wa mgodi huo, na kwamba hakuna madini yanayoibwa kama mbunge huyo
alivyosema.
Alisema
hakuna njia ya mkato, iliyofanywa katika ununuzi wa hisa ; na hakuna
waziri yeyote aliyehusika katika kusaidia kupindisha taratibu, kwani
kila kitu kipo wazi.
Alisema
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu), Jenista Mhagama hana ndugu na mtu anayefanya kazi
TanzaniteOne.
Akizungumzia
kufukuzwa kwa wafanyakazi 201, mwanasheria huyo alisema waliofukuzwa
kazi ni wafanyakazi hatari kwa mustakabali wa kampuni, kwani ni
wachochezi na wenye hila za kutaka kuihujumu kampuni hiyo ili ilete
maafa.
Alisema kugoma ni kosa kisheria na kama mgomo haukufuata taratibu, sheria lazima zichukue taratibu.
0 comments:
Post a Comment