Jose Mourinho amewaasa mashabiki wa Manchester United kusahau yote
yaliyotokea miaka mitatu iliyopita wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya
David Moyes na Louis van Gaal na kuangalia namna ya kuirudisha upya
katika zama zake.
Mourinho amethibitishwa leo na Man United rasmi kuwa kocha klabu hiyo
akichukua mikoba ya Mholanzi Louis Van Gaal baada ya kusaini mkataba wa
miaka mitatu.
Mourinho anakabiliwa na mtihani mzito wa kuirudisha United katika
zama za ubora wake chini ya Sir Alex Ferguson na kurudisha tena imani
kwa mashabiki.
“Tunaweza kuingalia timu yetu katika sehemu mbili,” alisema Mourinho,
“sehemu ya kwanza ni miaka mitatu iliyopita na nyingine ni historia
inayobeba klabu hii.
“Nadhani ningependa kusahau kilichotokea ndani ya miaka mitatu
iliyopita, napenda kuangalia timu kubwa (Man United) ambayo ipo mikononi
mwangu kwa sasa na nadhani mashabiki wanachosubiri kusikia kutoka
kwangu ni kusema kuwa nataka ushindi. Nadhani wachezaji wanahitaji
kusikia nikisema- hivi, Nataka kushinda”.
“Najisikia vizuri. Nadhani hiki ni kipindi sahihi kuipokea klabu hii
kwa sababu ni moja ya vilabu ambayo unahitaji kujiandaa ili kuweza
kufanya vyema, ndiyo maana naiita klabu kubwa.
“Na klabu kubwa lazima ipate kocha mkubwa na nadhani mimi ni mmoja
wao, hivyo nina furaha sana kupewa jukumu hili, naweza kusema
nimefarijika sana kupewa heshima kuwa ya kuifundisha klabu hii”.
0 comments:
Post a Comment