Saturday, 10 June 2017

KIMENUKA..Zari Aamuliwa Kuishi na Watoto Wake Katika Nyumba ya Marehemu Ivan.

KAMATI ya watu wanne walioteuliwa kushughulikia namna ambavyo mali za marehemu Ivan Ssemwanga zitasimamiwa, imempa mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari Hassan, moja ya nyumba za marehemu huyo iliyopo nchini Afrika Kusini ili aishi na watoto wake.

Kwa mjibu wa mtandao wa Kenya moja, kamati hiyo iliwajumuisha Ritah Ssemwanga (dada wa Ivan), George Ssemwanga Pinto (kaka wa Ivan), Lawrence Kiyingi Muyanja maarufu King Lawrence (rafiki mkubwa wa Ivan) ambaye pia ni kiongozi wa kundi la matajiri wanaojiita (Rich Gang) na Zari Hassan (mke wa Ivan). Kwa pamoja kamati hiyo imekubaliana kwamba licha ya kumpa Zari nyumba hiyo, pia imempa madaraka ya kusimamia chuo cha Ivan cha Brooklyn, kilichopo Afrika Kusini.

Pia Zari ameamliwa kuishi na watoto wake katika moja ya nyumba za Ivan zilizopo Afrika Kusini na nyingine itapangishwa ili kusaidia familia hiyo kiuchumi, huku kamati hiyo ikiendelea na usimamizi wa jumla hadi watoto hao watakapofikia umri wa kujitambua wa miaka 18.

Kutokana na hilo, Zari ameondoka Uganda na kuelekea Afrika Kusini, ingawa bado haijajulikana kama ataishi katika moja ya nyumba za Ivan huko Pretoria, Afrika Kusini au ataishi na watoto wake kwenye nyumba ya mpenzi wake, Diamond Platnumz, aliyonunua jijini Johannesburg.

TOA MAONI YAKO HAPA

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Related Posts:

  • Rayvanny afunguka mema Sugu aliyomtendea.Msanii Rayvanny amesema Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni mtu ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika video yake ya ‘Zezeta’ ambayo ipo mbioni kutoka. Rayvanny Rayvanny amesema Sugu ndiye alimpa idea … Read More
  • Picha: Zari atua hospital kumjulia hali ex wake Ivan.Mama watoto wa Diamond, Zari the Bosslady ameonekana katika picha akimjulia hali ex wake Ivan Ssemwanga ambaye anadaiwa kulazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya moyo. Zari akiwa hospi… Read More
  • TANZIA: Dogo Mfaume Hatunaye Tena. Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu. Dogo Mfau… Read More
  • Wastara Awaburuza Wasambaza Filamu Bongo Kortini. STEPS Entertainments, ambayo ni kampuni ya kusambaza filamu Tanzania, imepelekwa mahakamani na Wastara Juma, anayeidai kiasi kikubwa cha fedha baada ya kukataa kumlipa, Risasi Jumamosi limeambiwa. Kwa mujibu wa chanzo, m… Read More
  • Sakata la Diamond Kudaiwa Mil 400 na TRA lafika Hapa. Siku chache tangu Mbunge wa Jimbo la Mikumi Professa Jay kupaza sauti yake kuhusu makadirio makubwa ya kodi anayotakiwa kulipa Mwanamke anayewika nje na ndani ya nchi  katika muziki wa bongo Flavor Diamond  Pla… Read More

0 comments:

Post a Comment