MWANAMITINDO, Sasha Kassim ameibuka na kusema kuwa hapendi sauti yake kufananishwa na ya Wema Sepetu kwani inaanza kumletea matatizo ambayo hakuyatarajia kwa maana ya usumbufu. Sasha aliongea hayo baada ya kuandamwa na watu akidaiwa kuhusika na utengenezaji wa sauti iliyokuwa ikisambaa mtandaoni kitendo ambacho alikana kukifanya na kudai kuwa hana mazoea wala maisha hayo ya kujianika kwa kutafuta kiki.
“Dah mimi sijahusika na sauti yoyote na wala sidhani kama sauti yangu inafanana kiasi hicho na Wema kwamba naweza kumuigiza mimi si wa hivyo jamani kitendo cha kuhusishwa na sauti hiyo kimenikera na naomba watu waache mara moja,” alisema Sasha.
GPL Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment