WAKATI mkoa wa Arusha ukiwa na upungufu wa walimu 788 sawa na asilimia
58.85 ya mahitaji ya walimu mkoani hapa, imebainika kuwa, walimu 261
wamebainika kuwa na vyeti feki.
Mkoa wa Arusha wenye shule za sekondari za serikali 162, una upungufu wa
walimu 197 wa Fizikia, 243 wa Kemia, 85 wa Bayolojia na 263 wa
hisabati. Kwa mujibu wa Ofisa Elimu-Taaluma wa mkoa wa Arusha, Eugene
Shirima kazi ya kubaini walimu wenye vyeti feki mkoani humo
imethibitisha kuwepo na walimu 261 vyenye vyeti feki hadi sasa wakiwemo
walimu wa masomo ya sayansi na baadhi yao wamelazimika kujiondoa kazini.
Hata hivyo, Shirima amefafanua baadhi ya walimu wamelazimika kukata
rufaa Baraza la Mitihani la Taifa na Idara ya Utumishi kupinga hatua ya
kuwaondoa kazini. Amesema mbali na walimu hao kubainika kuwa na vyeti
feki baadhi ya walimu wamelazimika kujiondoa wenyewe bila hata kutoa
taarifa kwa mwajiri wao katika halmashauri za wilaya ama kwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment