Tuesday, 4 April 2017

Kimenukaa..Sumaye Afunguka Haya Mazito Kuhusu CCM..Adai Wanamuomba Atoke Upinzani.Fahamu zaidi hapa.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema uamuzi wa Serikali kumnyang’anya mali zake likiwamo shamba la Mabwepande, Dar es Salaam ni njama na hila za CCM kumdhoofisha kisiasa baada ya kuhamia Chadema.
Amesema Oktoba mwaka jana, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, chini ya Waziri William Lukuvi ilimnyang’anya shamba kwa madai ya kulimiliki muda mrefu bila kuliendeleza.
Akizungumza juzi kwenye kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA), mkoa wa Geita kujadili hali ya demokrasia nchini, Sumaye alisema hata wakimnyang’anya mali wasitarajie kuwa atafilisika na kamwe hatarudi CCM.
Sumaye aliyekuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo, alisema licha ya kunyang’anywa shamba hilo, ataendelea kuishi na maisha yake hayatabadilika na akaahidi kupambana usiku na mchana kuhakikisha CCM inaondoka madarakani.
“Mimi walininyang’anya shamba langu, nikawaambia nyang’anyeni, mimi ndiyo sasa naingia kwenye mapambano sawasawa,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Wako marafiki zangu kule CCM wakahoji kwa nini nisirudi CCM badala ya kuteseka kiasi hicho. Na mimi jibu nililowaambia ni moja tu, nimetoka CCM kazi yangu iliyobaki ni kuiondoa CCM madarakani na si kurudi CCM.”
Alifafanua kuwa mateso wanayopata wananchi ndiyo wanayopata viongozi wa juu wa Chadema ambao baadhi yao wameanza kuteswa kwa kunyang’anywa mali zao akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyenyang’anywa nyumba anayoimiliki kwa asilimia 75.
Alisema licha ya Mbowe kunyang’anywa nyumba hiyo ambayo hakuitaja, alisema Serikali ina mpango wa kumpora pia shamba analolima kilimo cha kisasa.
Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Sumaye ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema Taifa, alisema uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia vyama vya upinzani kufanya mikutano kwa wananchi, ni kinyume na Katiba ya Tanzania na haijawahi kutokea hali hiyo tangu vyama vingi vilipoanzishwa.
Alisema kwa katazo hilo, hakuna mtu atakayeanzisha chama cha siasa kwani kuanzisha chama lazima ifanyike mikutano ya hadhara kutafuta wananchi, lakini kwa hali hiyo hakutakuwa na usajili wa vyama.
“Hata Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mtungi anajua hilo kwamba demokrasia imekandamizwa. Nasi hatuogopi kumwambia Rais ambayo si ya kufanya kwani hana ruhusa ya kuvunja Katiba kwani aliapa kuilinda na kuitetea,” alisema Sumaye.
Aidha, alisema kama hali itaendelea hivyo pamoja na hali ngumu ya maisha ya Watanzania njia itakuwa nyeupe ya Chadema kuingia madarakani, na hivyo aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele kuipinga Serikali na kutetea demokrasia.
Baadhi ya wananchi walisema hali ya maisha ni ngumu na imefikia hatua ya wanaume kutelekeza familia zao kwa kushindwa kuzihudumia.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) jimbo la Geita, Mary Paschal alisema kuna familia zimetelekezwa na wanaume kwa sababu ya maisha magumu.
“Akina mama wengi tumekuwa wahanga wa maisha magumu, wanawake tunahangaika sana kwani akina mama tunapoomba matumizi wanaume wanachukua suruali na kuondoka bila kuaga,” alisema Mary.
Awali Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita, Neema Chozaile alisema lengo la kongamano hilo ni kujadili hali ya demokrasia nchini ambapo alisema demokrasia inataka kupotezwa kwa kunyimwa uhuru wa habari, kujieleza na kutoa maoni.
Alisema Serikali iliyopo ni ya kwanza kujitokeza kubinya demokrasia nchini kwa kunyima uhuru hasa wa vyama vya siasa kujieleza kwa wananchi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wabunge CCM Wameitaka Serikali Kutoa Majibu Sahihi Bungeni kuhusu Utambulisho wa Mtu Aitwaye Daudi Bashite.Fahamu zaidi hapa.

Dodoma.  Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.

Sakata hilo liliibuka juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini hapa.

Wabunge tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani ambacho hufanyika kabla ya mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha na inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi wameshakumbwa na adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.
Mpashaji mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Pamoja na kelele za watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu, si Baraza la Mitihani (Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo au kuchukua hatua.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa ALIKIBA NEW SONG (WANIONEA).




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Utata Waibuka Mchanga wa Dhahabu..Yadaiwa Kama Madai ya Magufuli Yakiwa ni Kweli ..Tanzania Itavunja Rekodi ya Dunia.Fahamu zaidi hapa.

WAKATI Rais John Magufuli akiunda ya kuchunguza taarifa za makinika ya dhahabu kutoka migodini kama una asilimia 90 ya madini hayo, wataalamu wamebainisha kwamba kiwango hicho kikithibitishwa, Tanzania itakuwa imevunja rekodi ya kuzalisha tani 4,000 kwa mwaka, kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu dunia iumbwe.
Aidha, wamesema ili kujenga kiwanda cha kuchenjua dhahabu nchini takriban megawati 500 za umeme wa uhakika zinahitajika kwa kiwanda kimoja jambo Tanzania haiwezi kulifanikisha kwa nishati iliyopo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rais kuunda tume hiyo kuchunguza mchanga kwenye kontena 282 alizobaini alipotembelea bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni zikiwa katika mchakato wa kusafirishwa.
Akizungumza katika kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Azam,  Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Serikali wa kampuni ya Accacia, Assah Mwaipopo alisema Serikali ina haki ya kuhakiki, lakini haiwezi kutokea yanayosemwa yakawa kweli.
Mwaipopo alisema katika historia, inaonesha kuwa nchi inayozalisha dhahabu kwa wingi duniani ni Afrika Kusini ambayo inazalisha tani 600 hadi 400 na kiwango cha dunia kwa takwimu za mwaka 2015 ni tani 2,500 tu hadi sasa.
Alisema wanaosema kuwa mchanga huo una dhahabu asilimia 90 wanatoa tafsiri potofu na kubainisha kuwa hata miche ambayo wanavuna katika hatua ya kwanza dhahabu si asilimia 90.
Meneja huyo alisema ni vigumu kutorosha dhahabu hasa kampuni ya Accacia ambayo imesajiliwa katika Soko la Hisa la London, Uingereza na kusisitiza kuwa taarifa hiyo itaondoa utata.
“Mfano ukisema kontena moja lina asilimia 90 ya dhahabu ni kwamba kuna tani 18 za dhahabu katika kontena la tani 20; ni vigumu kwani kwa kontena 260 zilizo bandarini  unataka kuiambia dunia bandari ya Dar es Salaam ina tani 4,000, ni taarifa ya kushitua dunia,
“Haijatokea kwa mwaka mmoja dunia ikavuna tani 3,000, kwani nyingi sana ni 2,500 hivyo taarifa zinazosemwa si sahihi ila ngoja Serikali ijiridhishe,” alisema.
Mchakato
Mwaipopo alisema mchakato wa kuchimba dhahabu una hatua muhimu ambazo zinahitajika ili kupatikana dhahabu ambapo katika hatua ya kwanza dhahabu huwa kubwa.
Alisema katika hatua ya pili kemikali zinazovuta dhahabu hutumika ili madini hayo kutenganishwa.
Alisema uchenjuaji unahusu tani moja ya makinikia ili kupata gramu mbili, hivyo haiwezi kuwa kama inavyosemwa kwamba asilimia 90 ya mchanga huo ni dhahabu.
Mwaipopo alisema pia hutumia kemikali ya carbon kupata dhahabu kabla ya kufikia makapi ila kama ingewezekana wangeishia kwenye makinikia.
Alisema kemikali ya synite ni aghali na baada ya matumizi inapaswa kuharibiwa hivyo ni ngumu kuiingiza nchini.
“Katika kuchenjua tunapata gramu 0.02 ambayo inatoka kwenye tani moja kwani yale ni makapi tunayaita dhahabu athari,” alisema.
Alisema kibiashara ingekuwa heri mchakato wa dhahabu kuishia kwenye makinikia ila gramu 150 kwa tani na ukiibadilisha tani iwe gramu utapata gramu 0.02 kwenye wastani wa tani moja.
Mhandisi huyo alisema katika mgodi wa Buzwagi wanapata tani 18 za shaba ambapo kwa gharama ya soko haina tija kubwa.
Kuhusu gharama za kusafirishia, alisema si kubwa sana kwani kontena moja linasafirishwa kwa dola 2,000 za Marekani na kuchenjua haizidi dola 1,000 hivyo tani 3.6 itakayopatikana itarejesha gharama na faida.

Mahitaji
Akifafanua kuhusu kiwanda cha kuchenjua dhahabu nchini alisema kiuhalisia kiwanda hicho kinahitaji uwekezaji wa muda mrefu ambao utazingatia ukweli kuhusu makinikia yaliyopo.
Alisema uwezo wa migodi iliyopo nchini ni kuzalisha makinikia tani zaidi 50,000 na kuwa ili kiwanda kifanye kazi yanahitajika makinikia tani 150,000 kwa mwaka.
Mwaipopo alisema pia kiwanda kimoja kitahitaji umeme wa megawati 500 hivyo kwa Tanzania ni vigumu kupata umeme huo kwani uliopo ni wa megawati 2,000.
“Kama yupo mwekezaji anayetaka kuwekeza anakaribishwa, lakini ni vema akahakikishiwa uendelevu wa uwekezaji wake kwani kiwanda kinachofanya kazi hiyo ya kuchenjua makinikia kina thamani ya zaidi ya dola milioni 500,” alisema.
Alisema mgodi wa Buzwagi umeanza kwisha hivyo utakaobaki ni Bulyanhulu jambo ambalo linaweka bayana kuwa makinikia yatakuwa tani 30,000 kwa siku zijazo.
Mtaalamu  
Dk Elisante Mshiu alisema dhahabu ni dhahabu wakati unatumia ila kijiolojia inapatikana kwenye ukanda wa miamba.
Alisema Tanzania ina kanda sita ila kanda ya Ziwa Victoria zipo kanda nane mbili zikiwa Kenya.
Mshiu alisema nchini kanda maarufu ya dhahabu ni Sukuma Land   ambayo inahusu Buzwagi, Bulyanhulu na Geita.
Dk Mshiu alisema hoja ya Serikali kutaka mtambo wa kujengwa nchini ni lazima wataalamu washirikishwe ili kuuhakikishia umma kuwa makinikia yatakuwapo ya kutosha.
Kuhusu kontena za tani 20 bandarini kuwa na dhahabu asilimia 90 alisema ni kitu ambacho hakiwezekani kwani kwa uzito wa dhahabu hiyo magari yasingetembea.
“Yote yanayofanywa yanafaa kupewa nafasi ila kiuhalisia haiwezekani kontena la tani 20 likawa na asilimia 90 kwa uzito wa dhahabu gari haliwezi kutembea,” alisema.
Kamati iliyoundwa na Rais inaongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma na wengine ni Profesa Justinian Rwezaura,  Profesa Joseph Buchweishaija, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Yoweza, Dk Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela.
Aidha, Bunge kupitia Spika Job Ndugai litaunda tume ya kibunge kuchunguza sakata hilo la mchanga wa dhahabu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

VIDEO: Swali la kwanza la Mbunge Salma Kikwete (Mke wa Rais Mstaafu ) bungeni Leo.

Baada ya kuapishwa, Mbunge Salma Kikwete ameuliza swali kwa mara ya kwanza na kulielekeza OR-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Mkutano wa saba wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo Dodoma. Leo asubuhi kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu mbunge wa kuteuliwa Mama Salma Kikwete aliapishwa



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Chemical ft Centano -Queen Of Dar es Salaam.

https://my.notjustok.com/track/download/id/201907




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#BREAKING NEWS>>>MBWANA SAMATTA ANUNUA ‘PRIVATE JET’ NDEGE YAKE YA KIFAHARI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta mapema leo ametupia picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter na huku akishukuru  Mungu kwa kumwezesha kununua ndege ambayo itakuwa ikimsadia katika safari zake za masafa marefu ya ndani ya Bara la Afrika, Ulaya anakochezea soka na kwingineko Duniani.

Ndege hiyo ya kifahari ya kibinafsi ni miongoni mwa ndege zinazotumiwa na matajiri wakubwa Duniani hivyo kwa ununuzi huo, Mbwana Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kumiliki ndege hiyo.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.

Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo pia  inashiriki Michuano ya Europa League pamoja na ligi kuu nchini Ubelgiji.

Hata hivyo Mtandao huu wa MO Blog  inawapongeza wasomaji wake wote kwa kuendelea kushirikiana nasi lakini pia tuwaondoe hofu tu,  leo ni siku maalum  ya Wajinga. (Foolish day) hivyo habari hii ni ya kuchangamsha pekee.
Ndege ya Samatta aliyoitupia kwenye mtandao wake huo asubuhi hii

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#Breaking News>>Maalim Seif Atoa Tamko Zito Kuhusu Prof Lipumba.Fahamu zaidi hapa.

Jana  Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif alifanya mahojiano na kituo cha Television cha Azam two na kusema hamtambui mwenyekiti wa chama hicho Pro. Ibrahim Lipumba pamoja na uwamuzi aliochukuwa wakumuweka kando na nafasi yake kukaimiwa na Magdalena Sakaya.
Malim Seif alisema  hawezi kwenda ofisi za Buguruni kwa kuwa makao makuu ya chama hicho yapo Zanzibar na sio Dar es Salaam


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Monday, 3 April 2017

Umoja Wa Ulaya Waipatia Serikali Ya Tanzania Msaada Wa Bilioni 490.Fahamu zaidi hapa.

Na Daudi Manongi - MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa 2017/18.
 
Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
 
“Nadhani mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo”, aliongeza Katibu Mkuu huyo.
 
Pamoja na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na kuweka mkazo katika viwanda na kilimo.
 
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na nishati.
 
“Mkataba ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
 
Amesema kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi ya sera yanahitajika.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Babu Tale Afunguka Kuhusu Bifu lake na Erick Shigongo..Adai Shigongo Kamtishia Atamkomesha.Fahamu zaidi hapa.

Babu Tale Afunguka Kuhusu Bifu lake na Erick Shigongo..Adai Shigongo Kamtishia Maisha
Nimekuwekea hapa chini Babu Tale Akifunguka Mwanzo Mwisho..Bonyeza Play:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kimenukaa..Chadema Wakimbilia Mahakamni Kuzuia Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kinatarajiwa kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki kutokana na Bunge kukataa majina yaliyowasilishwa na chama hicho kwa ajili ya nafasi mbili za Chadema za wabunge wa Afrika Mashariki kwa madai kuwa chama hicho hakikuzingatia suala la jinsia. 
Kwa mujibu wa Chadema kanuni zinataka theluthi moja ya wabunge wote (9) wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania na siyo kutoka kwa kila chama. Kesi ya msingi itataka tafsiri ya theluthi moja.
Maamuzi hayo yamefikiwa leo usiku na kikao cha wabunge wa Chadema waliokutana mjini Dodoma.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Jack Wolper Adai Pombe Ndio Imemfanya Akawa Mnene.Fahamu zaidi hapa.

Kuna usemi unaosema kuwa ‘Wasanii ni kioo cha jamii’ ambapo wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inafuata maadili, leo April 3, 2017 nimeipata stori hii ya staa wa Bongo movies Jackline Wolper ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwaonya vijana juu ya unywaji pombe.

Wolper alikwenda mbali zaidi na kuwashauri vijana ambao hawatumii pombe wajiepushe nayo, Jackline Wolper anatueleza sababu za kuandika hivyo.

“Niliandika kuhusu pombe kwa sababu naamini pombe labda ndiyo inaweza kuwa ilinifanya nikawa mnene kutokana na mwanzo mimi nilikuwa sinywi pombe kabisa na nilikuwa sijui kitu kinaitwa pombe na hata mtu alikuwa akinywa, mimi namshangaa kabisa. Kwa hiyo ndiyo nikaandika vile pombe siyo nzuri kwa wasichana ambao ndiyo wanaanza kujifunza pombe na wana miili yao mizuri tu. Waache kunywa pombe.” – Jackline Wolper.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Shamsa Ford Acharuka..Kumsomea AL-Badil Aliyeiba Account yake ya Instagram.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya Shamsa Ford kuibiwa akaunti yake ya instagram
“Ikishindikana kabisa akaunti yangu kurudi kwa yule ambaye amenifanyia huo ujinga nitamshtakia Mwenyezi Mungu, mimi ni mtoto wa kiislamu, nitasoma Al-badil ili Mwenyezi Mungu anijibu kwa hili”- Shamsa Ford
Mshauri kwa neno moja.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Acha Kusingiziwa singiziwa Mimba..Fahamu Jinsi ya Kutambua Siku za Hatari za Mpenzi za Kubeba Ujauzito.Fahamu zaidi hapa.

Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. 

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka  sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi? 
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba. 
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni siku yai linashuka hivyo ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.
kama mzunguko wako ni  wa kawaida yaani siku 28 sasa chukua 28 toa 14 unapata 14 yaani siku ya 14 ndio hatari zingine ni siku ya 10,11,12,13,14,15

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka  ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike. kwa lugha ya kingereza soma hapa


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Serengeti Boys Wakaza Mbele ya Waghana.Fahamu zaidi hapa.

Serengeti Boys wamefanikiwa kulinda rekodi yao ya kutopoteza mechi nyumbani na pia kufunga angalau mabao mawili kila mechi ya nyumbani baada ya kutoka sare ya bao mbili kwa mbili dhidi ya Timu ya Vijana ya Ghana..


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wenger: Sijiuzulu Ng'oo, Wanaojiuzulu Huishia Kufa Tu.Fahamu zaidi hapa.

Arsene Wenger ametoa mpya na safari hii amesema haondoki kwani wanaostaafu mara nyingi hufa kwa wenye umri kama wake.
Wenger, 67, amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa Arsenal kwa kushindwa kuipa ubingwa na sasa iko nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kufungwa mechi nne kati ya tano ilizocheza.
Kipigo cha mabao 10-2 kutoka kwa Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndicho kilichochochea hasira za mashabiki kutaka aondoke.
Hata hivyo, Wenger ameonyesha hajali na akasema: “Sifikirii kustaafu. Wanaojiuzulu ni makocha vijana.” Pamoja na kwamba, mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini Bodi ya Arsenal inampa jeuri kocha huyo kwani imemwongezea mkataba wa miaka mwili. Alisema pia kuwa atatangaza hatma yake karibuni.
“Kwa wazee kama mimi, ukistaafu, utakufa,” aliongeza Wenger, muda mfupi kabla ya mpambano wa jana dhidi ya Manchester City. Wenger anafundisha Arsenal mwaka wa 21 sasa lakini katika miaka hiyo, hajawahi kuipa ubingwa katika miaka 13.
“Of course hata mimi inaniuma kukosa mataji,” alisema. “Nikiangalia miaka 20 kwa kweli inaumiza kuona hakuna mafanikio.
“Lakini ukiangalia klabu ya wakati huo na sasa, wakati nilipofika, wanachama walikuwa saba, lakini sasa kuna watu 700, mambo yanabadilika.”
Alisema: “Ninachukia kufungwa. Ninaelewa kuwa mashabiki wanachukia kila Arsenal inapofungwa lakini kikubwa ni kushikamana na kila mmoja na kila shabiki kuangalia timu yetu hadi mwisho wa msimu, hicho ndio cha kufanya.” 


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mbarawa Amaliza Mgomo wa Mabasi.Fahamu zaidi hapa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri majini na nchi na kavu (SUMATRA) Gilliard Ngewe amesema huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo nchini zitaendelea kama kawaida hapo kesho  baada ya wamiliki wa  vyombo vya usafiri nchini kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa Makame Mbarawa.
Makubaliano hayo yalifikiwa mapema leo baada ya wamiliki wa mabasi (TABOA), wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UWADAR) pamoja na wamiliki wamalori(Tatoa) kuzungumza na Profesa Mbarawa na kukubaliana kubadili kanuni na kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
Walikubaliana kuzifanyia marekebisho kanuni hizo ndani ya siku 14 na zipelekwe kwa wadau, pia zitenganishe makosa ya madereva na makosa ya wamiliki.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mbwana Samatta apanda thamani.Fahamu zaidi hapa.

Thamani ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imepanda katika soko la wachezaji duniani.

Thamani yake kwa imefikia kiwango cha Euro milioni 3 sawa na shilingi bilioni 7.1 za kitanzania kwa mujibu wa mtandao unaohusika na biashara za wachezaji duniani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Samatta kutimiza idadi ya kiwango cha magoli iliyokuwa ikihitajika ambapo ameweza kufunga mabao saba katika mechi sita za hivi karibuni akiwa katika timu yake ya Genk pamoja na mawili aliyoyapachika Botswana mchezo uliochezwa na Taifa Stars

Mabadiliko hayo yamefanyika mwishoni mwa mwezi Machi ambapo mshambuliaji huyo alionekana kung’ara katika ushindi wa bao 4-1 iliyopata klabu yake dhidi ya Lokeren na yeye akitupia bao mojawapo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Nay wa Mitego: Usalama wangu umekuwa mdogo, wanapanga kunipoteza.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa muziki wa hip hop ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Wapo’ Nay wa Mitego amedai kuna watu wanataka kumpoteza.

Wiki moja iliyopita rapper huyo alikamatwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo wake mpya ‘Wapo’.
Hata hivyo Rais Magufuli alitoa tamko la kuachiwa kwa msanii huyo na kusema wimbo huo hauna matatizo.
Rapper huyo Jumatatu hii amefunguka kwa kudai kuwa kuna watu wanamfuatilia kutaka kumpoteza.

“Usalama wa maisha yangu umekua mdogo kwasasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia.,” aliandika Nay wa Mitego Istagram.

Aliongeza, “Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni mwana muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod#Wapo,”

Rapper huyo hakuweka wazi ni nani anataka kufanya hivyo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Aliyetumbuliwa na Rais Magufuli Dk Mwele Malecela Ateuliwa Kuwa Mkurugenzi Shirika la Afya Duniani (WHO).Fahamu zaidi hapa.

Salamu za pongezi zimeendelea kumiminika kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.
Pia, Dk Mwele  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville. 
Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020, una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa. 
Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na usubi. 
Miongoni mwa waliomtumia pongezi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Sikika, Irenei Kiria ambaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: “Hongera Mwele kwa kupata nafasi hiyo ina maana ulipangwa kulisaidia Taifa letu ukiwa nje.”
 Mwingine ni Mhadhiri wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo aliyeandika katika ukurasa wake wa twitter akisema: “Nina furaha kwa uteuzi wa Dk Mwele kuwa Mkurugenzi wa WHO.Nahisi kusamehewa kwa kuikosoa Serikali baada ya kumuondoa Nimr.” 
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile yeye aliandika katika ukurasa wake akimpongeza Dk Mwele na kusema, “Nimezidiwa na furaha baada ya kupata taarifa kuwa umepata kazi kubwa katika ogani ya kimataifa. Mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguliwa. Katumikie vyema.” 
Dk Mwele aliondolewa kuwa Mkurugenzi wa Nimr na Rais John Magufuli Desemba 17 mwaka jana. 
Kuondolewa kwake katika nafasi hiyo kulifanyika siku moja baada ya kutoa ripoti ya utafiti wa magonjwa, ndani yake ikiwamo taarifa ya virusi vya ugonjwa wa Zika katika maeneo ya Morogoro, Geita na Magharibi mwa Tanzania. 
Taarifa ya Dk Mwele, ilieleza kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, asilimia 15.6 walibainika kuwa na virusi hivyo. 
Siku moja baada ya kutoa takwimu hizo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa na Dk Mwele aliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo kwamba ugonjwa huo bado haujaingia nchini.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ile Kesi ya Scorpion Mtoboa Macho Yafikia Hatua Hii.Fahamu zaidi hapa.

Mkazi wa Buguruni jijini hapa, Deus Johakim Magosa (45) ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi namba 303 ya mwaka 2016 ya kumjeruhi, kumtoboa macho na kumfanyia unyang’anyi wa kutumia silaha, Saidi Mrisho inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini, leo alinusurika kutupwa lupango baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga kumtuhumu kutoa ushahidi wa uongo.

Wakili Katuga alimtuhumu shahidi huyo  kutokana na kutoa majibu tofauti wakati akimuongoza kutoa ushahidi wake na maelezo aliyoyatoa awali Kituo cha Polisi cha Buguruni.
Awali shahidi huyo alisema mahakamani hapo kuwa hakuwahi kusikia popote kuwa Scorpion amehusishwa katika tukio la kumshambulia Said, lakini baadaye alipobanwa alisema ni kweli alisikia tetesi hizo kuwa mtuhumiwa huyo ndiye aliyefanya tukio hilo. Pamoja na mambo mengine aliyomhoji na kumbaini kuwa anatoa ushahidi wa uongo wakili Katuga
alipomgeukia hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Flora Haule  na kumwambia shahidi anazidi kuidanganya mahakama hiyo na kuitaka mahakama hiyo imchukulie hatua kwa mujibu wa kifungu cha 164 cha ushahidi hapa nchini (Tanzania Evidence Act).
Shahidi huyo alionekana kuwa katika wakati mgumu baada ya wakili huyo kuwaita askari polisi na kuwataka wakae tayari kumchukua shahidi huyo.
Hata hivyo kutokana na ufinyu wa muda hakimu Flora aliahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 18 mwaka huu na kumuacha shahidi huyo aondoke na kumtaka kufika tena mahakamani hapo tarehe iliyopangwa bila kukosa ambapo Scorpion naye alirudishwa mahabusu mpaka tarehe hiyo.
Mwandishi wetu alizungumza na mmoja wa wanasheria mahakamani hapo kuhusu ushahidi wa uongo ambapo, mwanasheria huyo alisema unapobainika kutoa ushahidi wa uongo ukiwa ndani ya kiapo unaweza kufungwa jela kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Sunday, 2 April 2017

Shilole Ajivisha Pete ya Uchumba mwenyewe.Fahamu zaidi hapa.

STAA wa Filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ameamua kujivisha pete ya uchumba mwenyewe, kitendo ambacho kimezua minong’ono kwa watu wengi wakidai kuwa amevishwa na mtu ambaye hajamuweka wazi.

Akizungumza na Ijumaa, Shilole alisema kuwa aliwahi kuvishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ikapotea kitatanishi kisha Nuh akaoa mwanamke mwingine hivyo akaona kuliko kidole hicho kibaki tupu, akisitiri.

“Pete ile ya Nuh ilipotea, sijui huwa ni za mashetani? Nimeona ninunue nyingine niivae, hakuna cha mwanaume wala nini, mimi sijaona tatizo kuivaa na huenda ndiyo naiita ndoa,” alisema Shilole.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Darassa unaoitwa "Utanitoa Roho".




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

OFM Wamvaa Masogange ‘Kininja’, Siri Nzito Yafichuka Kuhusu Maisha Yake.Fahamu zaidi hapa.

KUFUATIA madai kuwa, mrembo mwenye figa matata Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anaishi na kigogo mmoja kwenye mjengo wa kifahari kule Makongo Juu jijini Dar na yale madai kuwa, anatumia madawa ya kulevya, kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu cha Global (OFM), kiliamua kumvaa kininja nyumbani kwake.
MADAI KWANZA
Madai ya mwanzo yaliyotua kwenye dawati la IJUMAA yalikuwa ni kwamba, eti modo huyo hufika nyumbani hapo mida ya usiku akiwa na mwanaume huyo ambaye hakuweza kufahamika kama ni yule Dick Sound aliyetajwa kutoka naye awali au ni mwingine. Aidha, kutokana na mrembo huyo kutopatikana kirahisi kwenye simu yake ya mkononi, gazeti hili likiwa na lengo pia la kutaka kuonana naye ana kwa ana kuzungumzia mambo mbalimbali ya kimaisha sambamba na mwenendo wa kesi yake ya madawa ya kulevya, liliamua kumfuata nyumbani kwake.
DAY 1 OFM KAZINI
Jumatatu, Machi 27, majira ya saa 12 jioni, OFM walifika nyumbani kwa Masogange na kugonga geti bila kufunguliwa hivyo wakakaa nje hadi saa 3 usiku lakini hakuonekana mtu yeyote kuingia wala kutoka.
DAY 2 OFM KAZINI
Mapema alfajiri ya siku iliyofuata Machi 28, makachero hao wa OFM walidamkia nyumbani hapo ambapo kuanzia saa 12 mpaka saa 1 usiku hakuna mtu aliyetoka wala kuingia.
OFM WAZAMA NDANI
Baada ya kuona kimya, OFM waliamua kusogea mpaka getini na kugonga lakini kwa muda wa dakika kumi walizogonga, hawakuweza kufunguliwa ndipo walipoamua kuingia ‘kininja’ kupitia kigeti kidogo ambacho hakikuwa kimefungwa.
Baada ya kuingia ndani na kubisha mlango wa nyumba anayoishi Masogange, alitokea msichana aliyejitambulisha kama mdogo wake na baada ya salamu mazungumzo yalikuwa hivi; OFM: Tuna shida na Masogange, tunataka kuongea naye mambo ya kisanii.
Binti: Mh! Dada hayupo, ila ngoja nizungumze na dada yake halafu nawapa jibu… (anaingia ndani kisha muda mfupi anarudi na kuwakaribisha OFM ndani).
Muda mfupi baada ya OFM kuingia ndani, anakuja mwanadada mrembo mwenye figa kama ya Masogange na kujitambulisha kuwa ni dada yake na kuwauliza OFM walikuwa na shida gani.
OFM: (kwa kuzuga) Sisi ni wasanii, tumekuja hapa kwa ajili ya kazi, tunayo ngoma yetu ambayo tunataka Masogange ashiriki kwenye video.
DADA MTU:  Kwanza nani kawadairekti kuwa Masogange anaishi hapa?
OFM: Sisi ni wakazi wa maeneo haya.
DADA MTU: Oke, sasa ipo hivi Masogange hayupo, lakini pia hashiriki tena kwenye video, kwani nyie mmemuona mara ya mwisho lini? Si muda umepita? Ndiyo hivyo sasa tafuteni mtu mwingine.
OFM: Kwa nini hafanyi muziki?
DADA MTU: Hilo ni suala binafsi siwezi kulijibu, nafikiri tumemaliza, naomba muondoke.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, OFM walisikia sauti ya watu kutokea chumba kingine, hali iliyowafanya wahisi ni Masogange na mtu mwingine. Hata hivyo, kufuatia dada mtu huyo kuamuru OFM waondoke, zilikuwa zimebainika siri nzito za maisha yake ikiwa ni pamoja na kuishi kifahari kutokana na mandhari ya sebuleni ilivyo.
Pili, mbali na dada yake wapo wadada wawili wa kazi na kubwa zaidi ni kwamba, ule mjumba unaotajwa kuwa kapangishiwa, haishi peke yake bali kuna wapangaji wengine hivyo wale wanaodhani anaishi kwenye bonge la mjumba, mawazo hayo yafutike.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kimenukaa..Mengi Aichana Serikali ya Magufuli..Afunguka Mazito Jinsi Mambo Yanavyotakiwa Kuwa.Fahamu zaidi hapa.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 1 April 2017

Kimenukaa..Nay wa Mitego Akataa Ombi la Rais Magufuli la Kuubadili Wimbo wa 'Wapo' Adai Liwalo na Liwe.Fahamu zaidi hapa.

Msanii Nay wa Mitego ambaye mwisho wa wiki amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na kushukuru kukutana na Waziri mwenye dhamana na kusema kwa sasa hakuna anachoweza kubadilisha kwenye wimbo huo.
Nay wa Mitego anasema kwa sasa hakuna kitu anachoweza kubadilisha kwenye wimbo huo kwani haukuwa na lengo baya ila lengo lake lilikuwa ni kufikisha ujumbe ambao tayari anasema anaona umeanza kufika, sehemu husika. 
Nay wa Mitego anasema mapendekezo ambayo aliyatoa Mhe. Rais John Pombe Magufuli atayafanyia kazi.
"Nimeitikia Wito wa Mh Waziri. Nashukuru tumeongea mengi wanasema usikatae wito bali Kataa maneno. Haikua kwa ubaya, hakuna chakurekebisha kwenye Wimbo wetu wa 'Wapo' ila aliyo pendekeza Mh. Rais nitayafanyia kazi. Huu ni Wimbo Wenu mashabiki wangu Wote Tanzania na Duniani Kote. Wapo ujumbe umeanza kufika. Sina mlinzi wala bodyguard nyinyi ndiyo walinzi wangu. Hakuna atakae badilisha mtazamo wangu" amesema Nay wa Mitego


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Yanga wa Kimataifa Wafanya Kweli na Kuiondoa Simba Kileleni.Fahamu zaidi hapa.

YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sifa nyingi kwa mfungaji wa bao hilo, Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 70 baada ya kumtoka beki wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohamed kufuatia pasi ndefu ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa kike mwenye beji ya FIFA, Deonesya Rukyaa wa Kagera, Yanga ilipata pigo dakika ya 30 baada ya kiungo wake Mzambia, Justin Zulu kuumia mguu wa kushoto na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake kuchukuliwa na winga, Emmanuel Martin.

Zulu aliwekewa mguu na kiungo wa Azam FC, Himid Mao wakati anapiga shuti kuunga mpira uliorudi baada ya kuokolewa kufuatia krosi ya kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda.
Martin alikwenda kucheza wingi ya kulia na Niyonzima akahamia katikati kuchukua nafasi ya Zulu aliyekuwa akicheza kama kiungo mchezeshaji.

Mabadiliko hayo ambayo hayakuwa mipango ya mwalimu, yaligeuka msaada mkubwa kwa timu hiyo, kwani Niyozima alikwenda kucheza vizuri sehemu ya katikati ya Uwanja na Yanga ikaanza kushambulia.

Azam nao wakapata pigo dakika ya 43 baada ya mshambuliaji wake, Yahya Mohammed kuumia msuli baada ya kupiga shuti na kushindwa kuendelea nafasi yake ikichukuliwa na Mghana mwenzake, Samuel Afful.

Kipindi cha pili, timu zote zilirudi vizuri na zikaendelea kushambuliana kwa zamu, ingawa baada ya Yanga kupata bao dakika ya 70, wakaanza kucheza kwa kupoteza muda.

Ushindi huo unaifanya Yanga sasa ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 25 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiwaangushia nafasi ya pili mahasimu wao, Simba SC ambao kesho watacheza mechi ya 25 pia dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva/Juma Mahadhi dk90+2, Justin Zulu/Emmanuel Martin dk30, Obrey Chirwa, Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk54 na Haruna Niyonzima.

Azam; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Yahya Mohmmed/Samuel Afful dk44, Shaaban Iddi/Bruce Kangwa dk75 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Joseph Mahundi dk69.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mahakama Kuu Yamwamuru Msajili wa Vyama vya Siasa kutotoa ruzuku kwa Prof. Lipumba na kundi lake mpaka shauri litakapoamuliwa.Fahamu zaidi hapa.

Mahakama Kuu imemuamuru Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutotoa ruzuku kwa Prof. Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi, CUF, na kundi lake.

Zuio hilo ni mpaka shauri dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Uamuzi huo umefikiwa na Jaji Dyansobela baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa kwa hati ya dharura.

Jopo la Mawakili wa CUF, liliiomba Mahakama Kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali shilingi milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa chama kuhusu fedha hizo ikizingatiwa kwamba, Prof. Lipumba alishavuliwa uanachama.

Mawakili hao akiwemo Juma Nassor , wamesisitiza kwamba, mazingira yaliyopo ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia serikalini.

Aidha, wameiomba Mahakama Kuu kwamba amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya msajili kumtambua Prof Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa rufani ya kufanyiwa marejeo mbele ya Mahakama ya Rufani Tanzania.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa